Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

NILIZANI MWIZI KUMBE MMMH SEHEMU YA 60๐Ÿ’˜๐Ÿ’˜

9th Aug, 2025 Views 116



Nikamwambia mama sasa kwanini hukuwahi kuniambia mama yangu??, akanambia kwanini nikuambie mambo mabaya kama hayoo salma , nimesema leo kwa sababu ilitakiwa niseme
Nikamwambia mama nisamehe nilikuwa nakujibu vibaya kipindi kile akasema usijali ni kwenye Ukuaji m hiyo kawaida ...

"Mama naomba nikuulize kitu "

"Kitu gani tena salma??"

"Umesema baba aliondoka wakati una mimba yangu na subira jee?? Inamaana baba alirudi??"

"Mhu yaan wewe umewaza ninii??"

"Nataka tu kujua mama!"

"Baada ya miaka sijui 8 mana wewe ulikua na mkubwa kabisa hadi nilisha sahau kabisa kuhusu maradhi yako ndio baba yako alirudi , na kipindi hicho ndoa ilikuwa inaheshimiwa sana mwanamke ni kama mtumwa tu kwa mwanaume wake ,sio kama nyie hapo siku hizi mnasauti sie kulikuwa hakuna

Kwahiyo baada ya kuja ndio nilishika ujauzito wa subira na baada ya miaka miwili subira kufunga ndio baba yenu alifariki "

"Daah kwahiyo kwenye ,mimba ya subira haukupitia changamoto??"

"Zilikuwepo lakini sio kubwa, kwanza baba yenu alikuja anaumwa na alikuwa dhaifu ,sikujua miaka yote alikuwa wapi hata nilipo muuliza alikuwa mkali mi nikaachana nae ,alikua ananitegemea mie zaidi kumuhudumia kuliko kuninyanyasa japo manyanyaso yake hakuyaacha wala kupunguza kila alipo pata nguvu alinipiga hiyo ndio ilikuwa furaha yake "

"Mmmh mama pole sana"

"Pole wewe ambae , yaliku athiri kwa kiasi kikubwa mpaka umekuwa na hizo athari ,sikuwahi kufikiria kabisa japo nilikuwa nahisi tu "

Niliongea namama siku hiyo., yaan upendo wa ajabu ulizaliwa kwenye moyo wangu kuhusu mama yangu, nilitamani nitudishe siku nyuma niwe namtii namsikiliza yaan nimfanye ajivunie mimi...

Niliahidi moyoni nitamtafutia zawadi mama yangu kabla sijachelewa , tena kitu kikubwa kitakacho mpa furaha akitazama .

Alex aliniijia kesho yake asubuhi , Juma tano ilifika ya kurudi kule , nilienda mpaka mwa Doctor akamwambia alex kuwa Nahitaji.msaada wa kidaktari kwanza kabla ya shule , ili niamshe ubongo wangu ulio kuwa umelala kwa sababu ya yale matatizo yangu alex akasema nitafanya chochote we nambie tu

Akasema doctor kuna mtu nataka mkutane nae ambae atakuwa doctor wake kuanzia leo, aliikuja mbaba tu hivi nilitambulishwa anaitwa Doctor mack akasema nitakuhudumia kuanzia leo ,nikamuuliza kwahiyo nitajua kusoma akasema ndio utasoma na utaandika nikasema sawa

Basi tuliondoka na alex yule baba alituambia kesho yake nianze hayo mazoezi ya kuamsha ubongo ,

Alex akanambia salma mke wangu nataka nimtafutie mama mkwe wangu zawadi nimeumia sana nataka nimshukuru kwa kukupigania wwe mpak leo umekuwa mke wangu leo nimekuona leo nipo nawewe ,bila jitihada zake sijui ingekuwaje kama asinge kupigania !!"

"Alex ,sijawahi kujua sijawahi kumbe mama angu ndio alipitia hayo kwenye kunikuza""
Hata hivyo salma mungu ndio kila kitu embu ona Ulipona pona wakati ukiwa tumboni ukazaliwa kwa mateso ukaweza kuvuka na umekuwa mkubwa bado umepitia maswaibu mengine ya kutisha sanaaa
Kuna haja kubwa sana ya kumshukuru mungu salma"

Tuliongea mengi na alex wakati tunaenda nyumbani, akanambia kuna sehemu nataka twende kwanza kabla ya nyumbani nikamuuliza tunaenda wapi akanambia subiri utaona huko

Basi nilishanga tunakwenda kwenye Shop moja hivi ya magari akanambia embu chagua gari zuriiii unalo lipenda yaan litakalo kuvutia sanaa

Mungu wangu mi hata kuendesha sijui ujue Alex akanambia kwani nimekwambia Unajua kuendesha au hujui nimekwambia chagua

Nilizunguka karibu lisaa zima yaan kila gari naona nzuri naenda mpaka mwisho narudi tena mwanzo , wee nikawambia alex mie sijui ndo sijui au vipi yaan hapa naona yote mazuri kwakweli sijui nichague nini
Alex alicheka kweli akasema haya ngoja nichague mie yangu matatu afu unambie moja wapo ambalo utalipenda nikasema sawa

Basi akachagua yaan naona aliyoyaacha tu menyewe mbona mazuri zaidi , nilikuwa kama nina kiwewe aiyaaa
Nikawaza mi nina tamaa tu.hakuna loloteee

Nilichagua gari moja huwezi amini niliumia kuyaacha yale , hapo nawaza jamani yaan na mie naenda kuwa na gari yangu tena ki gari kikali hatari afu sio zile Boda boda yaan we unamiliki ki ISt afu unasema et una garii??
Hahha siwacheki jamani si unajua maskini akipata matako hulia bwata bwata bwataaa ndio mimi sasa yaan nilikuwa siamini kabisaa
Et namimi leo namiliki gari weuweeeee hahaha nilikuwa najiongelesha hatari yaan naongea maneno kama yote kucheka sasa hata sijui kwanini aisee

Baada ya kila kitu akalipia afu akanambia twende zetu hee sa na Gari yetuu?? , mwenzangu nilimuuliza hata sikuvunga alex alicheka akasema daah bora umeniulizia humu ndani
Embu twende bwana kwani mi nimekwambia hiyo ni gari yako
Woii ,nikasema embu kuwa Serious Serious bwana alex akasema kweli tenaaa hiyo sio yako
Alikuwa anaongea huku anacheka nikajua tu hiyo ni yangu ananitania nikajinunisha hapo , tukaenda zetu Home ..

Nilianza darasa kwa yule Doctor naingia Asubuhi mpaka sa 6 alex anakuja kunichukua Mi mawazo yangu ile gari nami nianze ku drive lakini sipewi hee wacha nimnunie alex yaaan nilinuna ile kidogo kidogo mpaka anisemeshe ndio najibu
Ye anacheka tu ananiuliza we una shida gani mbona umebadilika hivyo mi nasema hamna nipo sawa
Sa kusema nataka ile gari ndio hivyo tena naona aibuu atanicheka ...

Kule kwa Doctor nilikuwa nafanya maziezi ya Ubongo yaan naingizw kwenye mashine flani hivi humo ndani wanawasha mwanga mkubwa kweli mi nafumba macho

Ilikuwa ni zoezi la utambuzi wa namba, ilabu na zile Alfabet , yaan hiyo ilikuwa ni kuamsha ubongo , aisee wanajua wenyewe hukoo ila Niliona mwenyewe mabadiliko yangu makubwa sana

ITAENDELEA.....

NAMPENDA ALEX

SO3

Nilihudhuria yale mazoezi kwa mwezi mzima kila siku, yalikuwa ni mazoezi mbali mbali sana kuhusu kusoma na kutambua vitu vingine

Baada ya hapo , alex alikabidhiwa akaaambia haya mke wako huyo mtafutie mwalimu tu mi kazi yangu imeisha
Alex akanambia baada ya kutoka kwa doctor kuwa Mwalimu tayari nimekutafutia ile pumzika wiki moja ndio uanze shule ,mmmh vile nilikuwa na hamu ya kutaka kujua kusoma nyiee nilimwambia mume wangu hapana yaan mie nataka kesho nianze, hiyo wiki naona kama ni mwaka mzima utapita

Akasema sawa, baada ya kutoka pale , kwa doctor safari tulienda mpaka kwa mama, alex tu alinipeka huko akanambia nilikuwa nataka umalize hili ndio tuje huku
Mama nilimwambia yaan naona kabisa kichwa changu kimekuwa chepesi mama kuna vitu naona kabisa nimeongeza , mama nae alifurahi hatari

Akamwambia alex asante kwa kuwa mmoja wa familia yetu, alex akasema mama usijali ila naomba nikupe zawaidi yangu, hii ni ndogo sana mama lakini naomba uipokee kwa mikono miwili

Naomba tu nikwambie asate kwa kunibebea salma wangu na kunitunzia na leo kawa mama wa watoto wangu..
Mama alicheka tu akasema bwanaaa hilo ni jukumu langu akasema sawa
Basi nikawa naki muhe muhe alex anampa mama tenaa zawadi gani jamani aaah
Akamwambia twende nje mama zawadi ipo huku
Hapo mkumbuke jamani nyumbani kwetu sasa hivi pamekuwa pa kishua hatari sio kama zamani
Nguvu ya inno na alex walitoa bonge wa jumba Geti kubwaa, humo ndani Furniture za kisasa , kuna bonge wa Tv ukutani yaan pamekuwa kama zile nyumba tulikuwa tumezoea kuona kwenye Tv tu

Sasa ile wakati tunatoka namuona mtu kama dada yangu amesimama nje ya bajaji anaongea na ki vulana hivi afu kile kivulana kikageuka kuonesha na kidole getini kwetu

Hapo ndo nilikutanisha nae macho huyu si ni dada yangu nikamwambia mama huyu si dada jamani
Ndio yeye mama menyewe alishangaa kaja na watoto wake
Ilibidi sasa tuanze tena kupokea wageni anasema jamani nilijua hapa pameuzwa kumbe ni nyie pesa ya kujenga hivi mama umetoa wapi kwanza
Hakuna hata aliemjibu , ye si alituachaniza baada ya kuolewa huko na mwanajeshi akapata kazi yake yeye alisoma akaona sie ni mizigo na hakuwahi kusita kabisa alimwambia mama siku ukibaki peke yako nitakuhudumia mie siwezi kulisha watu wazima shule iliyowashinda , akimaanisha mimi..

Maneno ya kashfa ya dada ndio sababu mie niliondoka zangu nikaenda kupanga ili amuhudumie mama yake lakini badi alikuwa anasema yaan mie tu kila mara ndo nitume hela kama nimezaliwa peke yangu!!!

Mwisho akaacha na kupokea simu kabisa hata za mama, na sie wala hatukumpa taarifa kuwa tumejenga , nimeumwa mimi alipewa taarifa lakini hata kupiga tu simu kuulizia hali ilikuwa mtihani kwake

Haya sijui leo kaja kufanya nini, nilikuwa nimekaa kimyaa najiwazia tu mwenyewe huku namtazama , anajichekesha na mama yake

Nikamwambia mama mie naenda ,dada akasema mbona unaondoka hata hujanitambulisha jamani ,nikamwambia huyu ni mume wangu, nikamgeukia alex nikawaambia alex huyu ni dada yangu huku nikilitaja jina lake

Alex akasema nashkuru sana kukufahamu shemu wangu, dada et akasema umepata mwanaume kweli mi nilijua utaokota mjinga mwenzio jamaniiii
Hivi hayo ni maneno kweli ya kuongea mbele ya mume wangu, si hata angesubiri tukiwa wawilii au sisi kama familia tumezoeana sasa ndo anajenga picha gani kwa alex
.nami sikuwahi kumwambia alex kama mimi na dada yangu huwa hazipandi

Mama akamwambia wewe mama Sumaiya umeanza upuuzi wako sasa maneno gani hayo ,mi nikacheka tu
Alex akanambia basi twende zetu nikainuka dada akauliza et subira yupo wapi yaan hata hajui habari za ndoa zetu afu ni dada yetu mhu

Wakati tunatoka akasema alex aah hata zawadi ya mama tenaa sijui nitampa lini ,nikamuuliza zawadi gani kwanza akasema aah siri yangu

Nikamuita mama nikamwambia mkwilima wako analalamika hajakupa zawadi yake , mama akacheka akasema yaan ndo mambo ya wageni yameingiliana haya nipe baba yangu hata mie nilishangaa mnaondoka sijapata zawadi .

Tukatoka nje ya geti alex akawa anatuongoza, tulizunguka nyuma kule ya nyumba jamani sijaamini macho yangu yaan ile gari ambayo nilichagua ile siku ndio zawadi ya mama yangu afu mi nilijua yangu et hahaha niliona aibu na nilivyokuwaga nimenunaaaa kisa hiyo gari khaaa, yalinishuka yoteee

Mama yangu ndo kama achizikeee , sijui hata kama hii ndoto aliwahi kuiota jamani ,alifurahi alifurahii ,alex akamwambia mama naomba upokee hichi changu kidogo

Yaani mama ni mtu mzima tu lakini naamini angekuwa bint nahisi angagala gala hata chini

Dada nae akaja alishangaa kukuta gari, akamwambia mama et mi nitakuwa nakuendesha mana najua we mzee huna safari
Mi nikamwambia we si mke wa mtu ,unaenda kwako
Hakunijibu hata , alex aliingiza gari ndani ya geti

Akamuuliza mama , nikutafutie Dereva au nikutafutie mtu wa kukufunza??

Mama akasema weee naogopa , bora mtu aniendeshee , alex akasema sawa mama

Tukaondoka zetu, nilimpigia subira, nikampa mchapo dada ake kaja ,

Akanambia naenda kumuona kimbea ye si alitususaa , nikamwambia nenda shoga anguu ..
Subira alinipigia simu akanambia kuwa baada ya kwenda nyumbani amegundua dada kaachika karudi jumla nyumbani mh nikasema atajua mwenyewe ye si anaakili apambane

Sema dada yangu hana hata kauli nzuri ye kila mara kujikweza anajiona ni bora kuliko wote yaani

Mi nilianza zangu darasa, yaani nilikuwa makini mnoo hapo nilikuwa najifunza kusoma na kuandika, kama chekechea afu li mama kubwaaa na watoto wanne

Yaani kuna muda nilikuwa nacheka mwenyewe jamani vitu vya kusoma watoto wangu et nasoma mie mweeeh

Nilikuwa na bidii sana sikutaka kufel hata kidogo mungu mkubwa uelewa wangu ulikuwa chap

Hata siamini ile siku naweza kuunga maneno
Mama anakula hee naweza kusoma kitabu cha hadith uwiii Salma omar mieee, raha gani zizidi hii

Basi nilikuwa bango zoteee za barabarani nasoma ila ndo hivyo kwa kuunga unga kwelii

Ilipita miezi 6 tu mi najua kusoma na kuandika , alex akanambia nataka uende kusoma elimu ya shule ya msingi yaani la kwanza mpaka la 7 umalize jamani nilitoa macho mie miaka saba si nitakuwa nshakufa

Akanambia hapana utasoma kwa mwaka mmoja tu
Nilikubali kwa moyo mmoja huku upendo ukizidi kwetu , nilimpenda alex mpaka nikapitiliza aisee

Nilisoma kweli mwaka mmoja nikamaliza nikapata chet cha darasa la saba,
Nilipelekwa kuanza elimu ya secondary hapo nilisoma miaka miwili jamani nilihisi nazeeeka shule lakini nilikuwa nasikia raha walau namie najua hii inasomwa vipi, nilikuwa mwepesi sana kujua sijui kwa vile nilikuwa mtu mzima au ubongo ndio umaamka kweli kweli

Hapo watoto wangu nao wapo shule yaan mama anasoma watoto wanasoma nyiee mmh basi tu

Nilimwaliza nikapata cheti changu safi kabisa cha Fom4 , mungu ashukuriwe mnoo yaan nilikuwa na Division one kabisaaa
Alex akanipeleka chuo, mume wangu mungu akulinde nakupenda sanaaaa...

Nilienda chuo bwana,wakati nilipo kuwa mdogo ukweli nilikuwa natamani sana kusoma niwe kama dada yangu lakini sikuwahi kufanikiwa niliacha shule nikaingia mtaani ndoto zile zilikufa kabisa ,.

Lakini leo nipo naenda shule mhu eeh mungu , tena chuoo
Nilisomea uongozi wa biashara hicho ndio alex alitaka nisome , nilisoma kwa bidii zoteee kuhakikisha namfurahisha mume wangu

Alex alimambia tumezaa Watoto wanatosha hao wanne, sasa hivi tutafute maisha kwa ajili yao tu , kwahiyo kazi ilikuwa ni kusoma kusoma na mimi ,

Nilihitimu masomo yangu usimamizi wa biashara, siku ya Graduation nyie leo naongea naona kama kawaida lakini ukuu wa mungu nitausifu daima Nasema hivi daima Nitamsifu mungu wangu

Kwa ule usiku mmoja, umefungua maisha yangu kwa miaka yote ninayo ishi leo duniani
Ilikuwa bahati mbaya kuonana na alex ule usiku lakini leo naongea nipo nae ,nipo na mume wangu ambae nikisema tumetoka mbali namaanisha ni mbali kweli yaan mbali kwelii sio.utani

Mimi hata nikigeuka nyuma kutazama nilipo toka na alex wangu sipaoniii yaan napaona Kuleeeeeeeee ambapo macho ya kawaida hayaoni isipo kuwa macho ya rohoni
Mama mkwe wangu. Ananipenda yule mama kuliko kitu chochote , hata subira pia anapendwa ni mama mwenye misimamo mnoo

Nakumbuka ile siku ya Graduation Alex alinipa zawadi ya Gari akanambia mke wangu moyo wangu na mwili wangu vyote nimekupa hivyo ndio vitu vya thamani sana kwangu haya mengine ni kama vichombezo tu.

Gari alinipa ya bei mbaya kali hatari , wakati huu kuendesha gari ,nilikuwa tayari najua , nilifurahi mnoo nikamwambia alex wangu mungu atuweke sie tuzeeeke wote , tuone wajukuu zetu tukiwa sebleni kwetu
Alex akasema mungu atatia wepesi mke wangu naamini tutafika huko tu ..

Ni muda tu kila kitu huwa kinakuwa kwenye mstari , nilirudi nyumbani ni vyeti vyangu vyotee ,furaha Yote ..

Hapo nilianza maisha mapya kabisaaa, alex alikuwa na biashara nyingi mno lakini niliona mie hata hanipi Biashara nipo tu afu zile Restaurant zote nilimwachia Subira na zingine mama walikuwa wanasaidizana hapo subira alinunua kabisa inno alimchukulia
Kwa vile nilikuwa bize na shule sikuwa na muda huo ndio.manaa
Nilikaa nyumbani miezi minne
Siku moja alex akanambia mke wangu kuna kitu nataka ukaone nikasema nini tena akanambia nataka nifungue kampuni ya Usafiri wa anga, litakuwa shirika Binafs nawewe nataka ndie uwe msimamizi mkuuu
Heee nikasema we Alex Serious?? Akanambia mhuu nipo Serous hee kutoka kwenye Upishi mpaka kwenda kuwa C.E.O we huogopi ..

Gafla sanaa nilijikuta nimekuwa Boss lady ,kuna muda nilitamani sana Juddy angekuwa hai mana niliamini kabisa leo nipo hapa kwa sababu yake
Hii ndio ile wanaita kufa kufaana , kama juddy angempenda kweli alex akamtii na kumpa heshima leo mie ningekuwa mtaani huko nimeolewa au sijaolewa sijui

Naamini nisingejua kusoma wala kuandika, na wala nisingejua kama tatizo langu linatibiwa

Nilitamani Juddy angekuwa yupo hapa ananichukia tu lakini sio kuniroga

Niligeuka kuwa Mwanamke mwenye Nguvu sana Pesa na hata ushawishi , nilifanya kampuni yetu kuwa kubwa na kutambulika mataifa makubwa ya nje ,

Kwa miaka 4 tu niliweza kufungua tena usafiri wa majini , Tuliweza miliki meli mbili za mizigo na moja ya Abilia

Alex alimiambia kila siku salma wewe ,Unaakili sana sana sanaaa ..

Mama mkwe wangu kipenzi alienilelea wanangu alifariki , niliumia lakini ndio mipango ya mungu hiyo, nashukuru sana mungu sana sana sanaaa

Mpaka leo hii navyoandika hapa mama yangu mzazi yupo na baba mkwe wetu yupo japo umri wao umekwenda sana

Huwa nikipata muda kwa miaka mara moja nakwenda kaburini kwa Juddy walau kumuombea mana mimi nilimsamehe huko alipo awe na amali njema

Mwanae amekuwa sana huwa namtazama kwa mbali Felix anamtunza vizuri sana licha ya kuwa anawatoto wengine lakini Bint yake yaan mtoto wa Juddy bado amempa.maisha bora sanaaa sanaaa

Asanteni sanaaa kwa kuwa na mimi, na haya ndio safari ya maisha yangu ambayo leo nilitaka kushare na nyie ๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™

MWISHO.

All the best byeeeee.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

NILIZANI MWIZI KUMBE MMMH SEHEMU YA 60๐Ÿ’˜๐Ÿ’˜  >>> https://gonga94.com/semajambo/nilizani-mwizi-kumbe-mmmh-sehemu-ya-60
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

gonga94 official track
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest