Tulipo ishia Season one
Aliamua kukaa mbali na Masha huku kichwani akiwa na mawazo mengine kabisaaaa .....
"Usinambie unataka kumuweka karibu Abby"
"Natamani iwe hivyo mana nahisi kuwa na amani nikiwa nae kuliko Masha ,lakini sintafanya hivyo nataka tu kuwa huru na Masha"
,"nikuombe kitu, unajua tangu umeanza kumuongelea Abby, umefanya nimkumbuke sana Vicky ,nilimuona mara chache lakin nilimuelewa sana, kwakua wewe masha anakuelew sana Embu naomba unipelelezee huenda anajua hata ndugu yake mmoja na Vicky "
"Unataka kuoaa kakaaa, hahah"
Alberto alikubali ombi la Rahul akamwambia atamsaidia huku anamtania .....
TUENDELEEE....
Masha jioni kama kawaida alianda chakula anajua Mr Alberto anakujaa, bila kujua Rahul anamtafutia nyumba ..
Siku enyewe mama yake Masha akamchukua Glory mtoto wa Masha kwenda nyumbani kwa masha bila hata kumpa taarifa ..
Rahul alimpigia simu Alberto baada ya kupata nyumba haikuwa mbali na anapo ishi Vicky mitaa mitatu unafika mtaa anao ishi Vicky ,, mr alberto alitaka iwe karibu na Vicky โฆ.
โumepata haraka sanaa โ mr Alberto alimuuliza Rahul wakati anaingia ndani kuitazama nyumba
โ hahah kwa ajili yako hakuna kitu nitafanya taratibu โ
โ nyumba nimeipendaa sanaa Rahul nzurii ,, Feniture hpa wapii ni mbalii โ
โ we tulia MR ,, hapa mie kila kitu naweka sawa nilitaka tu uione nyumba kama utaipenda โ
โ nyumba nimeipenda sanaa,, unajua ninii Rahulii โโ
โ sijuiii!!โ
โ nataka Abigael ndio anisaidi kuchagua isiwe sehemu ya mbalii โ
โhahahh daaah mzeee umakamatikaa ,, embu jitahidi nimuone huyo mtotoo kama ni salama kiasi hichoo,,vipi kama baba wa mtoto wake akirudiiโ
โsitaki hata kulifikiria hiloo aisee nahisi tu kumpenda sana yule dada siwezi kujizuia ,, acha tu nikae mbali na masha ,, hata akitaka nafasi ya juu ofisni nitampaa ,, nisaidie tu kujua sehemu naweza pata feniture nzuri ,, nitakwenda mwenyewe nataka Abby anizoee kwanza ,,,nitakwenda leo kuongea na Masha kwa kinaโฆ.โ
Masha akati anamalizia kuandaa chakula mezani kwa ajili ya mpenzi wake Mr A lberto , mam yake akaingia muda huo yupo na glory
โ mamaaaa!!saa mbona mnakuja bila hata taarifaa aahโโ akautupia chini mwiko wa chakula alio kuwa ameushika kwa hasira tu ya kumuona mama yake
โhuna hata aibu mpuuzi wewe,, mwanao ana muda gani hajakuona eti ,, kila siku ananisumbua anamtaka mama yake,, haya wewe nenda kwa mama yako โ
โmamaaa we upojeee ???et upojee , nikwambie mara ngapi kuwa GROLY kwa sasa hivii sio mtoto wanguu mpaka mambo yangu yakae sawa kwanza, kwani hela ya kula siwatumii??,, nimewatelekeza ?? ,, mbona nina wahudumia mamaaa aah sijui mpojeeeโโ
โhaya tuuwe sasaa kama tunakukera sanaa embu kaa hapo weeโ
Mama masha akavuta kiti kamuweka mtoto nae akaketi pembeni ya mtoto , masha alipat hasiraa ujio wa mama yake pale aliuona kama nuksi
โ embu ona mamaaa basi naomba leo muondoke halafu nitawaita siku ingie pleas mama nahitaji kuwa mimi peke yanguu โ
Mama masha hakuongea tena alimuinua mtoto wakaanza kutoka nje โฆ.
Kwenye gari ya Rahul ndio alikuw na Boss wake baada ya mishe mishe zao , akamwambia ampeleke kwa masha nia akamuulize kuhusu mtu anae itwa Vicky na kuhusu swala lake la kuhamia kwake nia wavunje mahusiano yao โฆ
Boazi akafungua geti baada yah oni kupigwa na Rahul ,, na wakati huo ndio mama yake na Masha nae anatoka ,, Rahul akawahi kumuambia Mr Alberto akamwambia huyo ni mama yake mash mbna anamtoto wa Vicky bado??
EP 22
Mr alberto akauliza mama yake masha??? Ooh ..
Akafungua mlango wa gari akashuka haraka,, akamuit mama !! huku anacheka chekaaaa,, mama masha hakuitika kwnza hamjuii akamuangalia kwa uso wa mshangaoo , mr alberto akajishtukiaa akamwambia aahm naitwa Alberto ni rafiki wa mtoto wako masha mama
Mama masha kidogo uso ukopata tabasamu akahema ni wewe ndie mchumba wakee ?? Mr alberto akasema Hapana mama tunaurafiki tu wa kawaida hatujaafika huko kwenye uchumbaa
Mama masha akaona labda anamuogopa ndio maana anakana yeye kapata utambulisho kwa mtoto wake uwa ni mchumba wake ,, akasema sawa nashukuru kukufahamu"
Alberto akasema mama twende ndani ,, mama masha akakataa akasema mie jamani nimekaa sanaa wacha tu niendee ,,,
Masha alisikia honi lakini haoni mtu anaeingia na alishajiandaa kumpokea Alberto,, yaan alivyosikia tu ile hon akakimbia chumbani kapunguza nguo akabaki na kinguo chepesii kinaonesha maungo yake yotee na ndani hakuwa amevaa kituu yaan yupo kichelee ...
Akachukua glass ya juice akaketi kwenye sofa la seblen kabinukaa kiuno juu juu ,, alipo hisi mlango mkubwa unafunguliwa akaachia tabasam la kumpokea mr wake โฆ
Tabasam likapotea pyee baada ya kuona familia nzima imeongozana ,alikuwa Glory ,,mama yake , Rahul na Alberto mwenyewe ,, mama yake akaona aibuu kwa jinsi mwanae alivyokuwa vyumba vipo mbalii nguo hakuna Rahul akataka kutoka nje haraka maana anaona mali za boss wake ,, masha alikuwa kajikunja kwenye kochi aibuu imemvaa
Mama yake akatoa mtandio wake wa kijora aliokuwa amejitanda akawahi kumtupiaa ajifunge ,, alberto nae akamzuia Rahul kutoka baada ya kuona masha kapewa nguoo
โsamahani tumeingia bila hodii โ Mr Alberto akajisemesha , masha akabaki anacheka cheka akawakaribisha ,, ikabidi aanze tu kujichangamsha kwa mama yakee
Akaandaa chakula kwa wote japo alitaka iwe ni kwa ajili yao wawili ndo mana kafukuza wafanyakazi wake wotee ,, kasoro boazi tuu โฆ
โMashaa et ulikuwa na rafiki yako anaitwa Vicky ? yupo wapi siku hiziii?? โ Mr Alberto akamuuliza masha mda wanakula , masha alikuwa anakunywa maji ikafanya apaliwe na maji aliyokuwa anakunywaa ,, alimtazama Rahul jicho kalii moyoni akasema kwanini Habari za Vicky ghaflaa??
Wakatazamana na mama yake halafu akacheka kama sio jambo kwake
โvipi mbona umemuulizia kuna usalamaa??โ nae akamtupia swalii
โHapana na wish tu kujua vibayaโ Alberto nae akajibu kwa mtindo wa swali โฆ.
Rahul akaona bora aingilie mana yeye ndio anashida na Vicky sanaa
โ nimemuona mtoto wake hapa nikajua labda alirudii โโ Masha akasonya moyoni baada ya kauli ya Rahul ,, halafu usoni akaonesha huzunii
โyaan Vicky bwana mmh huyu mtoto aalishaga mtelekeza , nimemchukua mimi na ananijua kma mama yake sasa hivii ,, na nitamlea kama mwanangu sitaki aje ajua kama mimi et sio mam yake,, et baby si utaniruhusuuu??? โโ Mr alberto akashikwa na kikohozi cha gafla baada ya kuitwa baby wakati ameshalikataa hilo kwa mama yake
Masha kasema ooh mama nilisahu huyu anaitwa Alberto ni mpenzi wangu ndio mchumba wangu huyu niliekuwa nakuambia ,, mpenzi huyu ni mama yangu na huyu ni mtoto wa aliekuwa shoga angu nipo nae sasa hivi ukiniruhusu nitamchukua kuishi nae hapa kama wanguโ
Masha akapata na pakupitishia jambo lake humo humoo ,, Rahul alibaki kimyaa anafatilia mazungumzo ya masha kwenye akili yake mambo yalikuwa yanagongana et Vicky amtelekeze mtot wake na aende pasipo julikanaa??? Kwanni?
Amemuona Vicky mda mchache lakini akili yake ilikataa alichosema mashaa ,, akasema masha Vicky ninae mjua nina uhakika hawezi kuelekeza mtoto hata awe anapitia kipindi kigumu kiasi ganiiโฆโฆ.
ITAENDELEAA
KWETU morogoro.
   
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.