Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

8--9 SEHEMU YA NANE* SINGLE DAD NA MAMA WA KUKODI ❣️

9th Aug, 2025 Views 94


Siku zilizidi kusonga maisha yalibadilika kwa Dala alikuwa anavaa anapendeza na alisimamia kila kitu kuhusu Shalon pia alikuwa anaongozaba na dereva kumpeleka shalon shule pia kurudi dala alienda kumchukua.
Walimu na wanafunzi walijua dala ndio mama mzazi wa shalon .

Siku moja Dala alikuwa hajisikii vizuri ilimbidi Max aende kumchukua shalon shuleni .
Kwakuwa alikuwa amechelewa kwenda shuleni alikuta wanafunzi wote wameondoka shalon alikuwa amekaa bustanini na mwalimu wake.
Max aliwafuata na kusalimiana na mwalimu .
" Baba shalon hongera sana kwa malezi ya binti yako.
" Asante. Alijibu max huku akiwa anatabasamu lakini hakujua hiyo hongera inatokana na nini.
" Shalon amebadilika sana yupo tofauti na mwanzo hata darasani amekuwa akielewa kwa haraka. Kuna baadhi ya mambo yanaweza kubadilisha maisha hongera kwako na mama Shalon.
" Asante mwalimu.

Max alimchukua mtoto wake wakaondoka lakini kichwani kwa max bado alikuwa anajiuliza kuna tofauti gani kwa Shalon? Kwakuwa miezi miwili iliyopita alikuwa bize hakuwa anafuatilia mwenendo wa shalon.
" Natakiwa kuona hayo mabadiliko ya Shalon.

Max alianza kumfuatilia shalon aligundua kuwa shalon amekuwa na tabia za tofauti sana . Akiwa nyumbani alikuwa akijishughulisha na kazi ndogo ndogo. Alikuwa akila anatoa viombo, anasafisha alipokula pia alikuwa na furaha sana .

Max alimuangalia Dala na kusema.
" Nilikuwa nakosea sana Dala natakiwa kumuomba msamaha kwa kutokumua mimi kwangu.
Kesho yake Dala alikuwa jikoni anamalizia kuandaa chakula cha jioni , Max alienda jikoni na kusimama pembeni yake.
" Niambie mama wa mwanangu.
Dala alishangaa maana hata siku moja max hajawahi kumuita hivyo wala kuongea kwa upole vile.
" Vipi kuna tatizo ?
" Kwanini?
" Kila siku najionea ujio wako mpya na hii ya leo sijawahi kuisikia.
Max alitabasamu kisha akasema.
" Dala kuna muda tunakuwa lakini hatujui kama tunakisea, nadhani hata mimi nilikuwa nakukosea.
" Ni kuhusu Shalon si ndio?
" Umejuaje?
" Ni siku ya pili sasa najiona unafuatilia na sura yako inakuwa imejaa tabasamu.
" Ni kweli nilikuwa nikiamini kutokana na
Mazingira tuliyokutana.

Dala alivua eplon akaweka pembeni kisha akasema.
" Max usihukumu mtu kabla haujaamua vizuri pia kuna vitu vya kufundishwa darasani na kuna vitu vya kufundishwa nyumbani. Kumbana sana mtoto na kumnyima vitu vyake vya msingi ni sawa na kumkatili . Hivi wakati unakuwa ulipelekwa maisha kama ulivyotaka aishi Shalon? Huku cheza na watoto wengine mtaani, hukuenda dukani?
" Hayo yote nilifanya na nilikuwa nanogewa na michezo mpaka nikawa nasahau kurudi nyumbani wanaanza kujitafutia mitaaani.
" Basi shalon nae alikuwa na haki ya kufanya hivyo.
Max alikuja kichwa na kujiona kuwa alikuwa anakosea kuingilia kwenye jambo ambalo hakuwa na ujuzi nalo.
" Dala kila kitu na kuachia wewe ila kukuwa na tatizo naomba unijulishe pia kama kutakuwa na jambo utahitaji usisite kuniambia.
" Sawa.
Kuanzia siku hiyo mara kwa mara Max alikuwa akitoka na Dalah pamoja na shalon walienda kutembea sehemu mbali mbali ikiwemo kwenye michezo ya watoto, kwenda kuogelea.
Max na Shalon walikuwa kwenye maji wakiogelea max akifundisha shalon kuogelea na Dala alikuwa kakaa pembeni akiangalia.
Shalon alitaka Dala aungane nao lakini Dala hakukubali alikuwa anaogopa sana maji.
" Njoo mama.
" Hapana shalon endelea kuoga na baba yako.
"Baba mwambie mama aje .
" Anaogopa kuzama hajui kuogelea.
"Si utamfundisha?
" Siwezi kumfundisha mtu mkubwa.
" Mfundishe bwana .
" Lakini hataki.
" Nenda kambembeleze.
Shalon alimuomba sana baba yake . Max alitoka kwenye maji na kumfuata Dala.
" Dala, shalon anawaumbua sana hebu fanya jambo moja .....
" Jambo gani? Aliuliza Dala huku akiwa kamtolea macho.
" Ingia kwenye maji.
" Hapana , bado nakupenda uhai wangu.
" Huwezi kuzama nitakuwa karibu yako , unaona shalon anaogelea.
" Amevaa vile vidude ili asizane sasa mimi nitasaidiwa na nini?
" Usijali nipo hapa nitakuwa msaada wako.
Dala alikubali , max alinyoosha mkono dala akampa mkono wake taratibu dala aliingia kwenye maji . Max aliushikilia vizuri na kusogea nae mbele alipokuwa shalon.
Dala alionekana kuwa muoga.
" Mama usiogope nipo hapa kwaajili yako . Alisema shalon huku akiushikilia mkono wa Dala.
Wote watatu walishikana mikono na kucheza kwenye maji .
Kadri Max alivyokuwa akimuangalia Dala alijikuta hali yake ilibadilika na akili yake ilihama.

*SEHEMU YA TISA*

Max akiwa bado ndani ya maji aliendelea kumtazama Dala. Kwa sekunde chache alihisi kama dunia imesimama. Kicheko cha Dala kilikuwa kimetulia, macho yake yalikuwa na mwanga wa furaha isiyo na mipaka. Alijikuta moyo wake ukidunda kwa nguvu zaidi, hali aliyokuwa hajaiona kwa muda mrefu sana.
“ Hii Sio kawaida, sitaki kuendeleza hiki kinachokuja kichwani kwangu. alijiambia moyoni huku akijaribu kugeuza macho yake kwa Shalon, lakini kila alipojaribu, macho yake yalivutwa tena kwa Dala. Wakati huo dala alikuwa hana abaloelewa alikuwa bize akicheza na Shalon .
Ilikuwa ngumu kwa Max kujizuia alitoka ndani ya maji.
" Kama mbona unatuacha humu.
" Nimechoka.
" Basi tusubiri, njoo utuchukue.
Ilikuwa mtihani kwa Max yani kwa hali aliyokuwa nayo bado Dala anataka akamchukue inamaana alitakiwa aushike mwili wa Dala. Kwakuwa hakuwa na namba ilimbidi arudi kumchukua . Alimshika mkono lakini hakutaka kumuangalia .
Walipotoka kwenye maji Max aliwaambia.
" Kabadilisheni nguo tunarudi nyumbani.
" Lakini bababina bado sijaenda kubembea?
" Kila siku unatembea shule hiyo inatosha .
Max aliondoka na kwenda kubadili , huku nyuma Shalon aliendelea kulalamika.
" Baba yako hajawahi kueleweka hata siku moja. Twende tukabadili nguo kipenzi.

Wakiwa wamerudi nyumbani, Max alikaa sebuleni kimya. Shalon alikuwa na Dala jikoni wakikaanga mayai.
Max Kila aliposikia sauti ya Dala ilimgusa kwa namna tofauti.
“Ni nini kinanitokea?” Max alijiuliza huku akijishika kichwa.

“Huyu ni Dala... msichana wa kawaida, aliyetoka kwenye maisha ya kawaida, amekuja kuwa msaidizi wa kulea mtoto wangu… sasa nakosa pumzi nikimuangalia? Hapana, Max, unapaswa kuwa na mke wa hadhi yako… mwanamke anayefanana na maisha yako na mnapendana kielimu.
Max aliwaza hivyo
Lakini upande wa pili wa moyo wake ulijibu kwa kejeli:

“Hiyo hadhi imekupa nini Max? Umekuwa mpweke, mwenye stress… lakini tangu Dala aingie hapa, hata Shalon amebadilika, na sasa hata wewe unacheka… unapata furaha ya kweli…”
Max alijikuta ana huna na hakujua awe upande upi wa mawazo yake

Kesho yake asubuhi max alichelewa sana kuamka . Alipotoka chumbani kwake alienda moja kwa moja jikoni. Alimkuta Dala akiwa na apron, akiwa amevalia dela lake na nywele zake ndefu alizibana . Alisimama mlangoni akawa anamuangalia jinsi alivyokuwa akimfundisha Shalon kupika maandazi.

Shalon alipomuona baba yake alimuita
" Baba njoo uone napika.
Max aliachia tabasamu na kusogea karibu yao .
" Habari za asubuhi.
" Salama .
" Naona mama na mwana mpo Bize.
" Ndio lakini tumeshamaliza.
“Max unataka chai au juice?” Dala aliuliza kwa tabasamu.

Max alifikiria kwa kwa sekunde kadhaa, kisha akajibu
“Juice inatosha… nataka kitu cha baridi.”
“ sawa mbona umelala sana leo?” Dala alimuuliza.
“Sina tatizo… nimechoka tu.”
" Pole , tangulia sebleni nitakuletea juice na kutafunwa.
" Sawa.
Max alienda kukaa sebleni baada ya sekunde kadhaa Dala aliandaa na Max akaanza kula . Lakini akili yake bado ilimuwaza Dala.
“Hatuwezi kuwa pamoja,” alijiambia kimoyomoyo, “siwezi kuruhusu maisha yangu kushuka kiwango… lakini… kwanini moyo wangu haukubali hilo?”
Hapa lazima nipingabe na moyo wangu.

Siku zilisogea Max akaanza kujitenga kidogo, akijitahidi kupambana na hisia zake. Alianza kutengeneza mazingira ya dala kumuogopa na hata kumchukua .
Siku moja alirudi kutoka kazini. Alikuta nyumba ikiwa kimnya alimuita shalon kimnya akaitwa Dala kimnya . Alirudi getini kwa mlinzi.
" Hawa watu wapo wapi?
" Shalon na mama yake wametoka.
" Ni kawaida yao kutoka nikiwa sipo?
" Huwa anampeleka Shalon kucheza na watoto wenzie.
" Kila siku?
" Mara moja moja.
Max alitulia kwa muda kama vile anatafakari kitu kisha akasema.
" Ni mbali sana?
" Sijui.
Alitoka akafungua geti na kusimama nje kama vile anawasubiri.

Baada ya dakika chache kupita dala na Shalon walitokea kwa mbali . Huku shalon akiwa anaruka ruka .
" Shalon ni baba yule.
" Anatusubiri?
" Ndio atakuwa akikumiss mkimbilie.
Shalon alikimbia kumfuata baba yake huku dala akitembea kawaida.
Kabla hajafika getini alikutana na gari. Ile gari ilisimama karibu yake.
Mwanaume mmoja alifungua kioo cha gari na kumuomba dala asogee amuulize kitu.
Dara alisogea karibu na gari ,wakati huo Max alikuwa katoka macho akimuangalia.
" Anafanya nini pale? Alijiuliza kama kwamba anaona wivu.

Dala alimaliza kuongea na yule mtu kisha wakaagana , Dala aliondoka huku akiwa anatabasamu .
Tabasamu la Dala lilimfanya Max aendelee kutafsiri mengine kichwani kwake.
Kila Dala alivyokuwa akipiga hatua kuwasogelea ndipo max alipozidi kushikwa na hasira .
Dala alipofika karibu alisalimia.
" Habari za saa hizi.
Max hakujibu alifyonza na kuingia ndani huku akiwa kabeba mtoto wake.
" Kheeee makubwa, kapatwa na nini tena ?
Alijiuliza Dala bila kupata jibu. Aliingia ndani alipofika sebleni alimkuta Max pekee yake.
" Dala njoo hapa. Aliongea Max kwa sauti ya amri.
Dala alisogea mpaka alipo.
" Ilimpeleka wapi mtoto wangu?
" Kucheza na wenzie na hiyo ni kawaida yetu.
" Acha uongo huwa unaenda na mtoto wangu kwa wanaume wako, unanifundisha nini mtoto wangu?
Dala alishangaa.
" Max mbona kama unanikosea heshima?
" Heshima unanikosea mwenyewe kwenye hii nyumba yangu sitaki mtu malaya kwani unakosa nini hapa? Kama mshahara nakupa , mdogo wako anaonesha na kila unachotaka unapata.
" Znanisumangia kwa unachinipatia? Umesahau hata mimi nipo hapa kwaajili ya kusimamia wewe, nyumba yako na mwanao?
" Sijakata lakini tabia zako mbaya ndio sizitaki.
" Tabia gani?
" Unatoka nje kwenda kuonana na wanaume zako . Yule ulisimama nae kwenye lile gari ni nani kama ulikuwa haulahisishi?
Dala alishindwa kuvumilia maneno makali ya Max alienda kujifungia chumbani kwake na kuanza kulia.

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

8--9 SEHEMU YA NANE* SINGLE DAD NA MAMA WA KUKODI ❣️  >>> https://gonga94.com/semajambo/8-9-sehemu-ya-nane-single-dad-na-mama-wa-kukodi
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

never give up harmonize
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest