Bas bwana Robby akachukua chai akanipa nionje kwanza .......nikaonja.......akanipa na mkate nile.....nikachukua mkate nikala nikanywa na chai ....kwa aibu hivohivo nikajikaza......na yeye akachukua sles akala akachukua chai akanywa....
hahahaha Kama tupo kilabuni vile .....hahahaha....jmn siku mbili tu nishaanza kumzomea Robby yaan nimeshamzoea ingawa ninamuonea aibu balaa.......tulikunywa chai mpaka
Ikaisha ......waaao... nice sana ...lunch pia hakikisha kijiko ni kimoja tu ..Robby aliongea hahahaha๐คฃ.....nikawaza nimtoroke.... nikafanye mambo mengine....fasta nikanyanyuka nikachukua vyombo ili nipeleke jikoni ......
hii kazi ni ya Mwaj wewe kaa na mimi hapa ....Robby aliongea.....kaka Robby nataka nikaoge nasikia vibaya sana.....maji yapo tele hapo chooni si umeyaona Lkn ...kama hauna nguo ya kubadili utavaa taulo tu mama hakuna wa kukudhuru hapa sawa feel free...Robby alinijibu huku akiwa anajinyoosha.......
Tafadhali naomba unisaidie nguo hapo kwenye kabati ......niliinuka na kulifata kabati nikatoa suruali moja nyeusi na tishert nyeupe nikampelekea .....alivaa tisheti Kimbembe kikawa kwenye kuvaa suruali....hawezi na alikuwa amejifunika shuka tu amevaa kiboksa tu.....๐
Sikitu I hope hautanionea aibu kunipa msaada....siwez kuvaa suruali maana siwezi kusimama naomba unisaidie kunivalisha.....Robby aliongea huku akiniangalia na lile jicho la kurembuaโบ๏ธ daaah jmn mbona ananipa majaribu huyu Robby ......niliinuka na kufumba macho ili nisimuone๐คฃbangi hizi ..... kisha nikamsogelea nikaanza kuvuta lileshuka huku nikiwa nimeficha macho hahahahaha ...nina utahira mwingi aisee......
Nilivuta shuka baadae nikawa nampapasa nichukue mguu mmoja niuvalishe suruali nikafanikiwa......nikachukua na wapili ......basi nikaanza kuipandisha ile suruali wakati huo bado nimefumba macho ....katika kupandisha pandisha si nikajikuta nagusa dyudyu yake pale juu ya boksa ๐๐คฃ.....niliruka kama spaidaman ๐คธ.......samahani kaka.....nikafungua macho ...kumchek Robby muda wote alikuwa akiniangalia kwa macho ya dhati sana ...daaaaah ๐....nilifeel feelings moyoni mwangu Lkn ilikuwa ni ngumu sana kujionesha kwake......sikitu.....abee kaka......njoo.....nikamsogea kwa uoga....naomba univalishe .....bas nikamalizia kumvalisha Ile suruali yake...akaomba nimsaidie kumkalisha kwenye kile kiti chake cha kutembelea Alaf nimpeleke nje akaotee kajua........
nilimpeleka nje baadae nikarudi kumuandalia nguo kwaajili ya jioni kwenda kufungua sabato....nilimuandalia suruali ya dark blue na shati nyeusi nilizinyoosha mpaka nzi akigusa anakufa papohapo
.....nikamuandalia viatu vyeusi nikaweka tayari kwaajili ya jioni.....nilirudi chumbani kwangu cha kwanza nilichukua ile glass na kuikumbatia nikaibusu kisha nikairudisha kwenye shangazi kaja langu.....nilitafuta nguo ambayo taenda nayo kanisani Lkn niliishia kupata stress Tu maana sikuwa na nguo ya maana zaidi ya magauni ya marinda yaliyo pauka ya kijijini kwetu๐ฅ.......sikujali kabisa nikachukua gauni moja nikalipasi nikapanga marinda vzr nikalinyoosha maana halikuwahi kugusana pasi tangia linunuliwe hahahaha ......nilitoka nje kumsaidia Mwaj vikazi vidogo vidogo.......tulipika chakula cha mchana na cha jion kisha tukasaidiana kufua nguo na kufanya usafi pale nyumbani.....
mida ya saa saba mchana tuliandaa chakula mezani nikaenda kumuita Robby kwaajili ya Kula maana yeye ndie jukumu langu lililonileta pale kwao.......lete hapahapa nje tutakula hapa.....aliniambia....wakat huo alikuwa akifanya kazi kupitia laptop yake......nilipeleka sinia la chakula ilikuwa ni ugali kuku na tembele......Robby huwa halii mikono mara zooote anatumia kijiko hata ugali.....niliondoka chap ili asiniite kula nae .......
jion iliwadia saa kumi na moja ....nikasikia honi ya gari ...alikuwa ni Justine ....alikuja na kutukuta tunajiandaa kwaajili ya kwenda kanisani.......tulisalimiana pale......vipi mama ...za tangu jana .. aliniambia..nzuri tu kaka sijui wewe ......niko poa sana mrembo........heee ๐..kumbe mimi ni mrembo ..nilijiuliza huku nikiona aibu.......Justine aliondoka na kuelekea chumbani kwa Robby ......baadae walitoka wote na kuelekea kwenye gari mimi pia na Mwaj tulitoka tukapanda gari haooooo kanisani.......mama lulu alikuwa tayari ashatangulia maana yeye ni kiongozi wa kanisani.......tukiwa njiani......sikitu mama......lini utakuja kwangu kunitembelea......Justine aliuliza huku akiwa anaendesha gari .....siku yoyote kaka J......nitaletwa na kaka Robby....waao itakua vzr sana uje bwana utie baraka ndani kwangu......Robby aliniangalia Kwa jicho la msisitizo kisha akasema......huyu nitakuja naye soon tu maana anakaa ndani sana.....
Mwaj alifika kwao akashuka kisha sisi tukaendelea na safari kuelekea kanisani.......tulifika kanisani nilishuka kisha Justine akamshusha Robby na kutaka kumuendesha.......Kaka ngoja huyu sikitu afanye zoezi kuniendesha wewe pumzika... Robby aliongea....bas na komwe langu nikachukua Kigari na kuanza kuendesha kuelekea ndani kanisani.....tayari watu walikuwa weeeeengi wanasubiri ibada inaanza.....
Lkn nilipofika mlangoni alikuja binti mmoja hivi mzuri balaa ....alisogea na kumkumbatia Robby ๐ jmn nilikumis Robby unaendeleaje? ....salama.... Robby alijibu..Lkn usoni alionekana amepoteza furaha baada ya kumuona yule dada .....dada embu acha nikusaidie kumpeleka ndani...kale kadada kalinisukuma na kuchukua Kigari na kuanza kumuendesha Robby kumpeleka kukaa...nilibaki nimeduwaaa,๐ณ
ITAENDELEA
FULL STORY UNAIPATA KWA KULIPIA TSH 1000
NAMBA YANGU YA WHATSAPP NA KULIPIA PIA NI 0715906120 MTANDAO YAS JINA LA USAJILI FLORA.
   
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.