Siku moja Irene alienda kuwatembelea alimkuta Dala na shalon wakiwa nyumbani, walikaa pamoja na kuongea mambo mengi na dala kuhusu Shalon pamoja na malezi .
Dala na Irene walikuwa wamekaa nje na shalon alikuwa ndani anafanya homework.
" Hivi dada Irene mama yake shalon amefariki mwaka gani?
Irene alishangaa.
" Wewe nani kakwambia kuwa amefariki?
" Huwa najua hivyo.
" Mama yake Shalon hajafariki yupo hai .
" Kheeee sasa yuko wapi na mbona tangia nimekuja sijawahi kusikia akiongea na mtoto wake?
" Mmmmh Dala sio kila mtu anaweza kuwa na moyo wa kibinadamu wengine wana roho za kinyama. Hilda alimtoroka Shalon kipindi Max yupo nje ya nchi alisema hawezi kuwa na mtoto asiyeona kwenye ukoo wao hakuna mtu wa aina hiyo akamuacha kama zawadi kwetu.
" Masikini huyo mwanamke kweli ni shetani.
" Ni kweli. Dala ndio maana nazidi kuomba uwe msimamizi mzuri kwa Shalon azidi kuamini wewe ndio mama yake maana kwa umri aliokuwa nao ni ngumu sana kumueleza ukweli.
" Usijali dada Irene nakuhakikishia shalon hatakuwa kitu chochote mpaka mtakapo amua kumueleza ukweli.
" Tunakushukuru sana Dala yani bila wewe nadhani Max kichwa chake kingewaka moto yani angezeeka kabla ya umri wake.
Dala alicheka alafu akasema.
" Basi amenusurika kuzeeka lakini amekuwa na gubu hatari jambo dogo atalikuza mpaka watu tunatafuta kwa kujificha.
" Hahahaha pole sana ila mzoee tu . Unajua kuna kitu natamani kitokee kati yenu.
" Kitu gani?
" Uwe wifi yangu kwa Max.
" Unasemaje dada Irene?
Yani mimi na Max? Hapana kwa kweli sitaweza na nae kwanza mimi nipo kama msaidizi tu hapa sijafukiria hilo kabisa.
" Dala unajua mapenzi huwa yanaanza tu bila kutegemea.
" Hata kama ila kwa mimi na Max ni uongo haitakaa itokee.
Waliendelea kuongea kuhusu max huku wakicheka , kifupi ilikuwa kama kujichangamsha na kufurahi. Wakiwa wanaendelea kuongea mara simu ya Irene iliita , alichukua na kupokea.
Aliongea na mtu aliyempiga kwa sekunde chache kisha akakata simu na kumwambia Dala.
" Dala kuna mtu yupo hapo nje inaleta pizza hebu nenda kapokee alafu mpe na hii hela.
" Sawa.
Dala alitoka nje akamkuta kijana mmoja akiwa kwenye pikipiki.
" Habari.
" Salama.
" Nimeagiziwa nije kupokea mzigo wa Irene.
" Sawa.
Yule kijana alimkabidhi mfuko uliokuwa na bosi la Pizza kisha dala anamkabidhi hela.
" Asante sana mrembo hivi unaitwa nani vile?
" Yani unavyoniuliza ni kama vile unalifahamu jina langu alafu umelisahau.
Yule kijana alicheka .
" Basi tuache hayo niambie jina lako.
" Naitwa Dala.....
Dala alipojitambilisha tu jina lake mara gari ya max ilifika.
Dala alipomuona aliingia ndani na yule kijana akawasha pikipiki na kuondoka.
Max aliingiza gari aliposhuka tu kwenye gari alimuita dala kwa sauti ya juu.
" Eheeee kumekucha.
Alisema dala huku alimkabidhi Irene mzigo wake.
" Kwani vipi?
" Acha nikamsikilize.
Dala alienda alikoitwa huku akiwa anajua anaenda kugombezwa.
" Abeee...
Max alimsogelea huku akimuangalia usoni huku akiwa amekunja uso wake.
" Nilikwambia nini na unafanya nini?
" Kwani kuna nini?
" Usijifanye hujui , yule kijana mwenye pikipiki amefuata nini hapa?
" Alileta mzigo wa dada Irene mimibaifahsmiani nae kabisa.
" Mzigo wa Irene mbona mlikuwa mnaongea tena huku unatabasamu kwa mahaba.
Aliuliza Max kwa sauti ya kujiamini lakini ilimfanya Dala acheke. Pia Irene alisikia nae alishindwa kujizuia akaanza kucheka kwa sauti.
" Anacheka nini?
" Max mbona upo hivyo, unanionea wivu Dala?
" Unaongea ujinga gani, kwanini nikuonee wivu kwani wewe ni nani kwangu?
" Sio ujinga max kama hauna wivu basi utakuwa unamuonea. Nilimtuma akapokea pizza na kutabasamu mbele ya mtu sio kosa ni kawaida sana.
" Irene naomba isivunje sheria za nyumbani kwangu.
Alisema Max alafu akaondoka na kuwaacha dala na Irene wakimuangalia. Wote pamoja walianza kucheka
" Dala bwana achana na huyu ana jambo lake linamsumbua, nenda kamuite shalon tuje kula Pizza.
Dala alienda chumbani kwa Shalon akamkuta yupo na baba yake.
" Shalon aunty anakuita ukale pizza.
" Waoooo napenda pizza. Alisema Shalon huku akikimbia kuelekea aliko Irene. Dala aligeuka kumfuata Shalon lakini Max akamzuia.
" Dala hebu subiri. Dala alisimama na Max alimfuata alipo simama.
" Dala naomba ufuate sheria za hapa ndani sipendi tukiwa tunapishana kauli kila siku.
" Lakini sio mimi ni wewe na ma wivu yako sijui kwanini unanionea wivu ikiwa mimi ni po kwaajili ya kazi maalumu hapa kwako.
" Ooooh kwahiyo unataka nikuache ulande ovyo kama hayawani, uongee na wanaume ovyo ?
" Kwani kuongea nao kuna tatizo gani?
" Wewe unaona kawaida lakini kwangu sio sawa sababu watu wanajua wewe ni mama wa mwanangu yani kwa upande mwingine niseme ni mwa.... Sijui nitumie rugha gani kukuelewesha lakini tambua kama wewe ni mama kwa Shalon na mimi ni baba unafikiri watu wanasemaje hapo?
Dala alibaki mdomo wazi huku akimuangalia . Mara Irene alifika.
" Hivi nyie mtakuwa watu wa kugombana mpaka lini?
Wote kwa pamoja wakasema.
" Nani kasema tukagombana?
" Shalon kaniambia anagombana na kila siku huwa kinafanya hivyo. Mnajua hii sio nzuri kwa mtoto? Mmeshawahi kufikiria mnamtengenezea mazingira gani?
Max na Dala walinyamaza mara shalon alifika na kusema.
" Baba yake Alice anampenda mama Alice lakini baba yangu hampendi mama .
" Kwanini unasema hivyo mamy? Irene aliuliza
" Hawanipeleki shule wakiwa pamoja, alafu hawalali kitandani wote alafu......
" Hey wewe nani anakufundisha hayo? Max alimkatisha na kumuuliza binti yake kwa ukali.
" Watoto wa siku hizi sio ma mbumbumbu mnatakiwa mtafakari na kuweka kila kitu sawa.
Alisema Irene kisha akamshika mkono shalon wakaondoka wakawa acha dala na Max wakiwa wamesimama.
Full 1000
Whatsp 0784468229.
   
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.