Walifika kwenye sherehe Fariss alisimama pembeni.
" Nitakua hapa naomba uwe na nidhamu pia ninakupa saa moja ya kufurahia baada ya hapo urudi hapa tuondoke la sivyo nitaingia hapo katikati kukuchomoa kwa nguvu.
Salma alitabasamu
" Haina haja hata ya kutumia nguvu baba la baba nitakuja mwenyewe najua hutakiwi kukasirika sababu ya hili.
Waliagana kwa mabusu kisha Salma aliingia kucheza.
Sherehe ilikuwa imeshika kasi. Muziki wa singeli ulichanganywa na midundo na watu walicheza kwa raha, na vinywaji vilimwagika .
Salma alicheza kistaarabu sana hakutaka kusogelea na mwanaume yoyote alikuwa mkali sana pindi mwanaume alipotaka kumgusa.
Kijana mmoja akasema.
" Kwahiyo unatulingia sababu huyo bwana wako yuko hapa ?
" Ndio nimekuja na bwana angu kwahiyo una mtaka au?
" Kuwa na heshima nitakuvuruga sasa hivi.
" Jaribu uone kama Abuu hakufanya chapati ya kusukuma.
Yule kijana kusikia Abuu aliondoka taratibu.
Baadhi ya wadada walinyanyua na wengine wakiteta kwa sauti ya chini.
" Jamani ni kweli Salmakaja na mwanaume wake.
"yule ndio Fariss mwenyewe?"
"Ndiyo bwana mwenyewe huyo! Wewe si unaona tu magari anayokuja nayo?"
"Kumbe ameamua kumsindikiza mpaka kwenye shuhuri zetu? Huyo Salma anamloga nini mwanaume wa watu.
" Unafikiri ni bure hapo na pengine ni mume wa mtu katutelekeza familia sababu ya huyu msichana mshirikina.
Hayo ndiyo yalikuwa maneno ya baadhi ya mashoga zake Salma waliokuwa wamejikusanya kwenye kona moja .
" Dawa yake ni moja tu tutamchukulia huyo bwana ake atasikiliza kwenye bomba ngoja nifanye mpango wa kwenda bagamoyo kwa babu. Alisema msichana mmoja anaitwa Asha .
Sherehe iliendelea, Salma alienda kucheza nyimbo chache lakini kwa nidhamu. Alikuwa makini, hakutikisika hovyo kama zamani, alionesha heshima kubwa si kwa hofu, bali kwa kuheshimu ahadi aliyompa Fariss.
Baada ya muda kidogo msichana mmoja alimfuata Salma na kumvutia pembeni.
" Kuna nini wewe?
" Kuna mambo muhimu nataka kukwambia.
" Kitu gani?
" Mashoga zako walikuwa wanakusema bwana ako na Asha amesema anaenda bagamoyo kumroga ili awe wake.
Yule msichana aliongea yote walioongea na Salma hakuwa na subira muda uleule alimfuata Asha . Alimshika begani na kumvuta kwa nguvu.
" Umesema nini wewe dege lisiloliwa?
" Kwani nimesema nini?
" Unataka mwanaume wangu si ndio?
" Nani kakwambia?
" Usijifanye kuruka mnafiki mkubwa yani wewe Asha ni wakitaka kuniroga na kunichukulia mume wangu. Kwa taarifa yako yule mwanaume hawezi kuwa na kikohozi kama wewe usiejua kuoga kazi yako kuosha makwapa nongo zimekuja mwilini.
Asha na Salma wakitupiana maneno mpaka kukaribia kugombana.
Habari zilimfuka Abuu pamoja na mama yake wote waliingilia huo ugomvi.
Ugomvi ulikuwa mkubwa sana . Fariss hakujua kinachoendelea alisikia kelele tu.
" Mambo ya uswahilini bwana hakuna ustaarabu hata kidogo ona sasa wameibua ugomvi kwenye sherehe ya watu.
Mara akasikia watu wakisema.
" Asha kayataka sasa familia nzima inamkabili.
" Nae anamchokoza Salma kwani hamjui?
Fariss kusikia jina la Salma alimuuliza dada mmoja.
" Wanaogombea na hapo ni wakina nani
" Salma na familia yake wanamchangia Asha.
Fariss kusikia hivyo alijipenyeza katikati ya watu na kwenda kumtoa Salma wake.
" Salma haya mambo ndio niliyokuwa hayajazaa hizo sehemu haziwezi kuwa salama kwako.
" Nilikuwa natembea nafasi yangu kwako Fariss yule mjinga Asha anakutaka.
" Mmmh sawa lakini hukuwa na haja ya kujibishana nae sababu mimi simtaki.
" Wewe unaongea tu unafikiri angekuroga ungekataa wewe, ungemtaka kwa lazima.
" Makubwa haya sasa hakuna kuendelea kukaa hapa na sitaki uje tena kwenye haya mambo. Haya twende zetu.
Fariss alimshika mkono wakaondoka huku nyuma nako watu waliambulia ugomvi mama Salma na Abuu wakarudi nyumbani.
Waliwakuta Fariss na Salma wamefika nyumbani wamekaa kibarazani.
" Yule mtoto ana laana eee.
" Mama tulia hilo halijaisha Asha ataniambia nilichomkisea mpaka aninenee mabaya.
" Achana nae kesho tutaenda Chanika kwa yule mzee akalipe kinga kabla hajaenda kujifunika nyota yako.
" Mama nawe umeanza na imani zako , sisi wengine tuna Mungu baya halitupati kirahisi.
Fariss alishukuru Mungu kuwa Salma hafagilii mambo ya imani za kishirikina maana aliposikia mama Salma anaongelewa mambo ya Chanika alishituka.
" Salma mpenzi achana nao hakuna wa kuharibu uhusiano wetu.
" Wewe kijana unasema hujui uchawi wewe.
" Mama Mungu atatusimamia maana anaona dhati ya moyoni kwetu.
" Tatizo ubishi yakawakuta nipo hapa .
Alisema mama Salma kisha akafungua mlango na kuingia ndani.
" Mpenzi umeona madhara ya haya mambo? Niliona mbali ndio maana nilitaka uache.
"Sawa lakini halogwi mtu hapa....
Mara mama Salma alitoka.
" Samahani baba bado upo upo?
" Sina muda mrefu naondoka.
" Basi nilikuwa naomba hela ya kuanzia kesho asubuhi maana hela niliyokuwa nayo yote nimetunza kwenye sherehe.
" Jamani mama hebu nenda ndani mimi nina elfu mbili pale ndani nitakupa.
" Kheeee elfu mbili inatosha nini hakuna sukari, mafuta wala unga.
" Hakuna shida mama.
Fariss aliingiza mkono mfukoni akatoa elfu 20 akampatia.
" Mama hiyo utaanzia ila kesho nitakuja na vitu.
" Sawa mwanangu asante.
Mama Salma aliingia ndani Abuu nae akaomba yake.
" Shem na mimi naomba ya fegi.
" Jamani jamani hata wewe mwanaume unaomba hela badala ukatafute? Msibani kama ninewaletea atm hapa nyumbani huyu nae ni mtu anazitafuta. Umempa ile hela mwenzio anaenda kuvuta mibangi.
Salma alimtetea Fariss.
Fariss alitoa elfu kumi akampa Abuu.
" Ubarikiwe.
" Yani mnakera hamjui tu.
" Usijali mpenzi wangu nenda katulie ndani , kesho nitakuja kukuona pia sitaki uendelezwe ugomvi na wake watu.
" Sawa.
Waliagana baada ya hapo Fariss aliondoka lakini kichwa chake kilikaa mawazo mengi sana hakujua afanye nini ili amtoe Salma kwenye yale mazingira.
Kesho yake Fariss alifika mtaani kwa Salma na kupeleka vitu vya matumizi ya nyumbani.
Mama Salma alipokea viroba vya mchele, unga , sukari huku akipiga vigeregere.
" Haya sasa mkwe nunae na nina tamba nae mnao taka kwenda kuoga karogeni lakini mjue kila mtu na bahati yake . Badala ya kwenda kufunika nyota za wenzenu katafuteni kuosha fedha muongee na nyie muwe na bahati.
Siku mbili baadaye, Salma alipigiwa simu na Fariss.
"Naomba twende ukamjue mama yangu. Ana hamu sana ya kukuona."
Moyo wa Salma ulishituka.
"Mama yako?"
"Ndiyo, najua hujajiandaa, lakini usijali. Utakuwa sawa."
Salma alipata shauku na hofu kwa wakati mmoja. Alijua kwenda kuonana na mkwe sio lelemama hasa mama wa mwanaume mwenye uwezo kifedha na wenye elimu kama Fariss.
Farris ameenda kwakina Salma kakutana na mama mwenye hekaheka zake vipi Salma atakutana na mama wa aina gani na je mama Fariss atakubali Salma kuwa mkwe wake?
Full 1000
Whatsp 0784468229.
   
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.