Katika historia ya Songea mkoani Ruvuma kuna nyota moja iliyong’aa kupita zote Nduna Songea Luwafu Mbano aliyeuawa kikatili na wajerumani mwaka 1906
Huyu hakuwa tu kiongozi wa kijadi, bali alikuwa ngome ya ujasiri, Jemedari asiyeogopa risasi, na mkakati wa kijeshi aliyewaongoza mashujaa wake hadi sekunde za mwisho za mapambano.
Nduna Songea Mbano hakuwa Chifu mkuu, lakini alishika nafasi ambayo wengi waliiona kama moyo wa uongozi wa Inkosi Mputa bin Gwazerapasi Gama.
Kati ya machifu 11 waliokuwa wasaidizi wa Inkosi, yeye ndiye aliyekalia kiti cha heshima Msaidizi Mkuu . Maelekezo yote kutoka kwa chifu yalipitia kwake, na taarifa zote kutoka mashinani zilikusanywa kwanza mikononi mwake kabla hazijamfikia Inkosi.
Lakini jina lake lilichomoza zaidi si kwa vyeo, bali kwa mapambano. Wakati vita vikilipuka katika eneo la Songea , Nduna Songea Mbano ndiye aliyebeba jukumu la kuwa jemedari mkuu.
Aliongoza askari wa kijadi katika mashambulizi, akiwatia moyo wenzake kwa maneno na kwa mfano wake wa kuishi mstari wa mbele.
Umaarufu wake ulivuka mipaka ukasikika kote katika himaya ya Wangoni, hadi watu wakaanza kumtaja zaidi kuliko chifu mkuu mwenyewe.
Huu ni ushuhuda kwamba historia mara nyingi huandikwa na matendo, si vyeo. Na matendo ya Nduna Songea Luwafu Mbano katika ujasiri, ushujaa na kujitolea vimebaki kuwa kioo kinachoakisi roho ya Majimaji hadi leo..
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments