Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

VERY HANDSOME 🌸Lover boy💓💓02

23rd Aug, 2025 Views 39



Vizuri naona wote sasa mpo kwenye makundi kesho naomba niletewe quiz yangu asubuhi na mapema makundi yapo nane kila la heri...
Lecture aliondoka tukabaki wenyewe..
Kundi namba moja mje basi tukutane tujadiliane... Penny aliongea
Kila mtu akasogea kwenye kundi lake ili kujadiliana maswali hayo..
Gerson alichukua peni akanakili maswali kwenye karatasi kisha akatugeukia...
Haya maswali nadhani sio magumu lecture kaelekeza hakuna asiyeelewa tumpe mtu mmoja akafanye kesho alete hapa kujadiliana ni kupoteza muda wewe shika....
Nani mimi 😳 niliuliza kwa mshangao
Ndio naongea na wewe............
Alinigeukia na kunipa karatasi ile....niliogopa maana sikuelewa lecture alivyofundisha halafu ndio kanipa karatasi ety niwawakilishe kama grupu nikaona aibu kusema kuwa sikuelewa lecture alivyofundisha ikabidi tu nipokee..

Unaitwa nani jina 🤔 aliniuliza, naitwa Angel 😇
Oh jamani Angel kesho atatuletea kazi yetu nyie tawanyikeni mjisomee...
Nilirudi kukaa nyuma ya kabisa huku kichwa kinaniuma nikajuta hata kwanini niliangukia grupu namba moja yaani ni la kijinga sijawahi kuona halafu magrupu mengine wapo bize wana jadiliana...
Niliinuka ili nichungulie wengine wanavyofanya nipate hata mawazo...
Jioni tulirudi nyumbani usiku nikawa bize nafanya zile hesabu..
Hivi ni kweli unazifanya hizo hesabu peke yako unaziweza,? Penny aliniuliza
Ndio nilimjibu kiufupi nikiashiria sitaki usumbufu aniache niandike....
Niliandika hadi usiku saa sita nikaamua nilale..
Asubuhi na mapema niliamka kumalizia kuandika ndipo nikaenda chuo....
Nilimuona Gerson amekaa kwenye moja ya bustani huku akichezea laptop 💻 yake nilimfuata na kumpa karatasi niliyofanya maswali...

Tayari nimemaliza nilimwambia aliichukua ile karatasi akaisoma kisha akaichana mbele yangu.....

Why umechana karatasi na huu ndio muda wa kukusanya nilimuuliza huku nikiwa nimekasirika..
Baadae vipindi vikiisha unifuate kwa sasa usiniulize maswali mengi kuna kazi naifanya hapa tafadhali nenda darasani..
Nilimkata jicho hilo nikaelekea darasani huku kichwa kinauma atajua mwenyewe mimi nimeandika yeye kachana na watu ndio wanakusanya sasa hivi 🤔 ... Nilijisemea moyoni nilienda kukaa nyuma kama kawaida yangu...
Baada ya lisaa limoja baada ya kipindi cha kwanza kuisha Lecture alikuja akiwa na yale makaratasi...
Alikuwa amechukia sana 😠 nikajua hapa kimenuka tayari..

Mwandishi ni Babie Love 0742133100
Hivi nyie ina maana kipindi naelekeza jana hapa hamkunielewa kwani ? Ndio madudu gani haya mliyoniandikia yani watu wamekaa vichwa vya watu nane mnapata mbili tu wengine ziro yaani ni kikundi kimoja tu ndio kimefanya vizuri ni kundi namba moja...
Moyo ❤️ wangu ukalipuka pah enhe tumekuwa namba moja tena wakati Gerson alichana karatasi yangu imekuwaje tena nilijiuliza..

Nadhani hawa ndio nilikua nao darasani sasa namuomba mwanakikundi mmoja wapo aje mbele atuelekeze mlifanyaje fanyaje hadi mkapata haya maswali yote...
Wote wa kwenye kikundi waligeuka nyuma nilipokaa niende nikafanye yale maswali..
Gerson akasimama na kusema kwa kuwa tulijadiliana na aliyeandika na madam Angel mimi nitaenda kuelekeza...

Itaendelea.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

VERY HANDSOME 🌸Lover boy💓💓02  >>> https://gonga94.com/semajambo/very-handsome-lover-boy-02

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
never give up harmonize
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest