Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

SINGLE DADY NA MAMA WA KUKODI* *SEHEMU YA KUMI NA SITA*

20th Aug, 2025 Views 148



Max alimuangalia Dala usoni aligundua bado ana wasiwasi.
" Mpenzi kuwa na amani sitaki uwaze sana ukajisababishia matatizo wewe na mtoto wetu alie tumboni.
" Max sina uhakika kama ninayo bado sijapima.
" Kwa maelezo uliyonipa wewe ni mama kijacho.
Dala alimuangalia huku akitabasamu.
" Sawa daktari wangu.
" Twende tukamuangalie binti yetu.
Walitoka chumbani pamoja wakaenda chumbani kwa Shalon walimkuta shalon bado Kalala.
Dala alikaa pembeni akawa anamuangalia usoni.
" Masikini amelia kwa muda mrefu sasa muone alivyopumzika kwa amani.
" Yani huyu hilda anataka kunisababishia nifungwe jela.
" Mmmmm mpenzi sitamani kusikia wala kuona unafanya kitu chochote cha ajabu bado tunakuhitaji sana hatutamani kuwa na maumivu mengine ya kukupoteza.
" Sawa mke wangu nimekuelewa muamshe mtoto umuandae nataka tutoke , acha na mimi nikaoge kwanza
" Sawa

Max alienda bafuni kabla hajaanza kuoga alisimama mbele ya kioo akawa anajiangalia kwenye kioo.
" Hilda sitamani hata kuiona sura yako ni bora ukae mbali na maisha yangu na ukiendelea kumsumbua binti yangu nitamtoa macho yake .

Baada ya dakika kadhaa kupita wote walikuwa wameshajiandaa kwaajili ya kutoka.
Walipanda kwenye gari wakati Max anaendesha gari shalon alianza kumsimulia baba yake kuhusu Hilda.
" Baba yule mama mwembamba kama miss aliniambia mimi ni mtoto wake nililia sana niliogopa alitaka kunichukua.
" Hawezi kukuchukua binti yangu sababu yeye sio mama yako .mama yako ni huyu hapa .
" Basi mpelekee polisi asije kuniiba tena"
" Sitaruhusu afanye hivyo kesho nitaongea na mkuu wa shule ili asifike tena pale shuleni.
" Sawa baba.

Wakati mtu na mtoto wake wakiongea Dala alikuwa akifikiria yake.
" Afadhali Max awe na msimamo huohuo hata atakapomuona Hilda awe mbogo asimsikilize kabisa. Sitamani Hilda aninyang'anye hii furaha, nime hangaika sana mpaka hapa tulipofika siwezi kuvumilia kama ikitokea nitawapoteza Hawa wapendwa wangu.
Max aligundua kuwa dala hakuwa pamoja nao alikuwa mbali sana kimawazo.
" Mpenzi unawaza nini?
Dala alitoka kwenye dimbwi la mawazo "
"Hakuna kitu mpenzi nipo sawa tu.
" Najua haupo sawa , swala la hilda zisikuumize kichwa hakuna kitakacho tuyumbisha yeye ni kama upepo tu uliopita kuchafua hali ya hewa, hii hali itakuwa kwa muda tu badae kila kitu kitakuwa sawa .

Walifika kwenye mgahawa mmoja maarufu sana pale jijini wakaenda kukaa kwenye moja ya meza iliyokuwa imejitenga pembeni.
Waliagiza chakula na kuanza kula. Max alijitahidi sana kupiga story za kuchekesha ili kuwafanya wachangamkie hususani shalon asahau kuhusu kilichotokea mchana.
Max alifanikisha kile alichotaka na kuifanya familia yake ifurahie mlo pia kujisikia vizuri.

Baada ya kumaliza kula walizunguka sehemu mbali mbali kuangalia madhali tofauti tofauti kisha baada ya hapo walirudi nyumbani.
Wakiwa kwenye gari shalon alipitiwa na usingizi ikabidi Dala ampakate.
Walipofika nyumbani max alishuka na kumbeba binti yake na kwenda kumlaza vizuri chumbani kwake. Alipo hakikisha amelala alizima taa nae akaenda chumbani kuungana na mpenzi wake.

Kesho yake asubuhi Dala aliamka akiwa hakusikia vizuri alikimbilia chooni kwenda kutapika , Max alimfuata na kusimama mlangoni akawa anamuangalia.
Dala alimaliza kutapika akasuuza mdomo wake kisha akasimama wakawa wanaangaliana usoni na Max.
" Inabidi twende hospitali.
" Nitakwenda jiandae kwaajili ya kwenda kazini.
" Mimi ni baba bora Dala siwezi kuwaacha familia yangu natakiwa kuhakikisha mnakuwa salama.
Dala alitabasamu kisha akasema
" Asante sana mpenzi kwa kutujali.
Max alimkumbatia kwa upendo mkubwa.
" Nakupenda sana Dala.
" Nakupenda pia.
Max alivunja kumbatio kisha akamuangalia dala usoni
" Haya niambie mke wangu utakula nini?
" Nitakunywa juice tu.
" Na nini kingine?
" Hiyo tu inatosha.
" Sawa ngoja nikawaandalie vipenzi vyangu.
Max alienda jikoni na dala akaamua kwenda kumuandaa shaloni.
Walipomaliza kujiandaa walienda kupaza kifungua kinywa na Max akaenda kujiandaa.
Alipomaliza kujiandaa alitoka sebleni.
"Mpenzi ngoja nimpeleke shalon shule pia naenda kuongea na mwalimu baada ya hapo nizltakuja kukuchukua nikupeleke hospitali.
" Sawa baby.
Dala aliagana na shalon kisha shalon akaondoka na baba yake.
Wakiwa kwenye gari shalon alikuwa akisisitiza baba yake kumwambia mwalimu Hilda asirudi tena kwenda kumsumbua.
" Usijali binti yangu kila kitu kitakuwa sawa kuwa na amani.
" Sawa baba kipenzi.

Walipofika shuleni Max akienda kuonana na mwalimu wa darasa wa shalon na kumuuliza kilichotokea jana na mwalimu alimwambia kila kitu.
" Yule mwanamke nib waajabu sana, mwalimu nakuomba sana huyo mwanamke asikutane na mwanangu.
" Sawa baba shalon nitajitahidi kuzuia hilo lisitokee tena.
" Nitashukuru sana mwalimu napenda binti yangu asije kuichukia shule kwaajili ya watu wa ajabu pia napenda awe na amani.
" Sawa

Baada ya max kumalizana na mwalimu aliondoka akaenda nyumbani kumchukua dala wakaelekea hospitali.
Wakiwa njiani alimpigia simu rafiki yake daktari na kumpa taarifa kuwa watafika hospitali muda sio mrefu.
Baada ya dakika chache walifika hospitalini walipokelewa na kupelekwa moja kwa moja kwa daktari, walipewa huduma ya haraka, dala alifanyiwa vipimo. Dakika chache badae daktari alikuja ba majibu ya vipimo alikaa kwenye kiti chake na kuwaangalia usoni.
" Vipi doctor? Max aliuliza
Doctor baliachia tabasamu kisha akasema.
" Hongera sana , Dala ni mjamzito wa wiki 3.

Offer offer offer
Soma yote kwa sh 800
0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

SINGLE DADY NA MAMA WA KUKODI* *SEHEMU YA KUMI NA SITA*  >>> https://gonga94.com/semajambo/single-dady-na-mama-wa-kukodi-sehemu-ya-kumi-na-sita

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest