Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

MY CRAZY HOUSE GIR 9---10

23rd Aug, 2025 Views 38


9

Weekend moja ilifika Damian siku hiyo alikuwa nyumbani hakwenda sehemu yoyote alikuwa akizunguka kwenye mazingira ya pale ndani.
Kuna muda alikuwa bize kama anachati na mtu huku akitoa tabasamu . Vanessa alimuangalia na kutamani kwenda kumchukiza kidogo.
Alisogea sehemu aliyokuwa ametulia na kusimama pembeni yake, Damiani alifunika simu yake na kumuuliza
" Unataka nini?
" Nimeliona unatabasamu ndio maana nikaja .....
" Khaaaaa kwahiyo tabasamu langu limekuvuta au?
" Ningependa kujua unatabasamu kwaajili ya nini?
" Wewe mwezi mchanga hebu ondoka hapa na ukafanya kazi zako.
" Sawa kazi nitaenda kufanya lakini punguza ubinafsi nionyeshe hata kidogo na mimi niongee siku za kuishi au kama ni mrembo ni tone maksi zangu.
Damian akicheka kwa dharau kisha akasema
" Hivi unafikiri mimi naweza kuchukua mwanamke asiejielewa kama wewe mimi nachukua pisi kali yani mbwa hatuko, wewe unanichukuliaje wewe.
" Kwahiyo mimi siwezi kuwa mwanamke wako?
Damian alimuangalia Vanessa kwa mshangao kisha akaanguka kicheko kikubwa.
" Vanessa acha kunichekesha bwana mtu kama wewe sio type yangu hata kidogo siwezi kupita na wewe hata kwa bahati mbaya.

Kauli za Damiani kilimuumiza sana Vanessa lakini hakutaka kuonyesha kama kasirika. Aliamini kama Damiani atajua kasirika hiyo ndio itakuwa fimbo ya kumchapa kila siku.
" Unachosema ni kweli kabisa sababu hata sisi sio type yetu watu kama nyie coz tunajiheshimu hivyo hatuwezi kuwapa nafasi na playboy.

" Huna jipya sasa ngoja leo nikuonyeshe kuwa mimini mwanaume wa mjini.
Alimpigia simu kwa Doreen, binti mmoja mrembo mwenye muonekano wa kuvutia na maisha ya kifahari.
Simu iliita upande wa pili ikapokewa.
" Hallow baby.
" Hallow malaika wangu upo wapi?
" Nipo home
" Ok unajua leo nipo home alafu nimeboreka nahitaji kampani njoo nyumbani tafadhali.
" Mmmh....
" Hapana baby usinikatalie maana leo nimepanda vitu vya maana kwaajili yako hata jikoni nitaongoza nikupikie mwenyewe.
Damian alisema kwa sauti ya kuvutia, akimtania Doreen.
Lakini moyoni alijua Vanessa ndiye atakayepika, atasafisha, na kupamba meza. Yeye kazi yake ni kuvaa vizuri na kukaa kama mwanaume wa maana akimsubiria malkia wake.
" Sawa baby ngoja nijiandae nakuja sasa hivi.
" Asante mpenzi utanikuta nikikusubiri. Mwaaa.....
Damiani alikata simu kisha akanyanyua macho yake kwa pozi akamuangalia Vanessa.
" My crazy maid naomba uende ukadandiwe chakula kizuri ambacho nitakula mimi na mpenzi wangu pia hakikisha unapamba ile meza ivutie.
Vanessa alimteua mate kisha akatoa tabasamu la kulazimisha.
" Sawa boss.
" Nenda sasa inasubiri nini sasa?
Vanessa bado alisimama huku akitafakari kitu , Damiani alinyanyuka akaenda ndani alitembea kwa Madaha alikiona yeye ndio mshindi .

Baada ya kama nusu saa Damiani alishuka chini akiwa amevalia vizuri, amepiga perfume ya bei mbaya na, alikuwa amependeza mno. Alimwita Vanessa.
" Mgeni wangu anakuja. kila kitu kipo tayari?
" Ndio boss wangu.
"Mwanamke wangu akifika hakikisha hauonekani kwenye mazingira tutakapokuwa tumekaa la sivyo nitakurudisha kijijini kwenu ukapige jembe."
Vanessa alimuangalia kwa jicho la pembeni kisha akasema kwa tabasamu:
" Usijali boss wangu mgeni wako atahisi yupo peponi.
" Haya naomba uondoke hapa nenda kamalizie kazi zako.
" Sawa.
Vanessa aliondoka huku akionekana kuwa mpole na kutii amri.
" Pimbi wewe huwezi kunifanyia madharau , italipiza hizo dharau zako

NUSU SAA BAADAYE...
Doreen aliwasili na gari ya kifahari ambayo aliendesha dereva wake. Alivalia nguo ya kubana, mikoba ya designer, na uso uliojaa make-up ya kiheshima. Kifupi alipendwa sana na alikuwa mrembo mno.
wakaanza kupiga stori.
Damian alimkaribisha kwa bashasha na mahaba makubwa, mabusu motomoto . Waliingia sebleni Damiani akamfungulia Muziki wa taratibu ukawa unacheza. Damian alikuwa na uhakika wa hii mechi ya moja kwa moja.
" Karibu sana baby.
" Asante.
" Nimefurahi sana kukuona .
" Asante mimi pia nimefurahi.
" Sasa twende tukafanye wine .
" Sawa.
Walishikana mikono wakaenda kukaa.
" Vanessa leta wine kwaajili ya malkia wangu.

Baada ya dakika moja, Vanessa aliingia na glass mbili za juice kwenye tray.
" Nani kasema ulete juice?
" Wine hakuna imeisha ndio maana nikajiongeza nikatengeneza juice .
" Kwanini haikusema sasa?
" Ilikuwa ghafla sana sasa ningekumbukaje.
" Weka juice uondoke.
Vanessa alitengwa juice kisha akaondoka huku akiwa anatabasamu . Alienda jikoni akasimama mlangoni kama vile anasikiliza kitu.

" Karibu juice mpenzi. Damian alinyanyua grass moja ya juice akampa Doreen.
" Asante.
Damian nae alishika grass yake wakafunga chees. Damian alipeleka grass yake mdomoni kwa Doreen.
Doreen walikunywa kidogo , alishindwa kutimiza wala kuvumilia kuiweka mdomoni alisema palepale sebleni.
" Vipi, nini? Damian aliuliza .
" Kunywa hiyo juice.
Alijibu doreen huku akiangalia kutafuta maji. Damian wakijaribu bar kuonja alihisi mdomo unawaka moto.
Wakihangaika kusukutia na maji kutoa pilipili wakati huo doreen alikuwa akicheka hana mbavu.
" Vanessa njoo hapa. Damian aliita kwa hasira na mara moja Vanessa alifika.
" Umefanya nini Vanessa?
" Kwani kuna tatizo gani jamani?
" Kwanini umeweka pilipili kwenye juice?
“Samahani boss,” alisema Vanessa huku tabasamu,
“nimeweka pilipili kidogo, nilihisi mgeni wako ni hot kama wewe.

MY CRAZY HOUSE GIRL 10

Damian alibaki akimtazama Vanessa kwa hasira, huku Doreen kikohozi kikali huku akihema hema kutokana na pilipili.
Uso wa Damian uligeuka kuwa mwekundu kwa hasira na aibu mbele ya mrembo wake.
"Vanessa! Hii ni nini sasa?" Damian alifoka kwa sauti ya juu.
Vanessa alibaki amesimama, akijifanya hana hatia, huku tabasamu la kibabe likiwa mdomoni.
"Boss, pole sana, ilikuwa ni surprise. Nilidhani mgeni wako anapenda vitu spicy kama wewe. Si ulisema ni hot girl, nikadhani na ladha yake ni hot pia."

Doreen alikuwa bado anajifuta machozi kutokana na ukali wa pilipili mdomoni.
"Damian, huyu ni house girl au ni mchawi wako?!" alisema kwa hasira, huku akinyanyuka.
"Baby calm down, ntamfundisha adabu huyu. Vanessa Rudisha heshima yangu!"
Vanessa alipiga magoti ghafla, akainama.
"Boss, naomba radhi. Nitarekebisha juice nyingine tamu zaidi."
Damian alimkaribia kwa hatua mbili kali.
"Vanessa, ukirudia huu upuuzi tena, utaondoka humu ndani kwa makofi!"
Vanessa alijibu kwa sauti ya chini .
"Sawa boss, nimeelewa."

Damian alirudi kwa Doreen na kuanza kumfariji, akimletea maji baridi.
"Pole baby wangu. huyu mjinga nitamuadabisha.
Doreen akatikisa kichwa kwa dharau,
"Kwa kweli kama unakaa na wajinga hivi, tutaniweza kweli? Huyu alitaka kuniuwa kabisa.
Achana nae mpenzi hili nitalinaliza.
" Nataka umfukuze hapa ndani la sivyo mimi na wewe basi.
" Hilo lazima ila kwa sasa twende chumbani ukapumzike.
Damiani alimshika mkono wakaenda chumbani , alimkatisha kitandani kisha akatoka na kumfuata Vanessa jikoni.
" Vanessa hili bado halijaisha na hapa lazima uondoke.
" Sipendi maisha ya kutishiwa.
" Unafikiri nakutishia? Ngoja mgeni aondoke .

"Alafu Fanya ile menu niliyokuambia , nyama ya kusaga, wali wa nazi, na salad ya parachichi. Na usinichezee mchezo mchafu.
"Sawa boss wangu haitajirudia.
" Ukiwa tayari njoo unigongee.
" Sawa.
Damiani alivyoondoka Vanessa akasema
“Ngoja tu, mechi bado ina dakika tisini, Damian.”

Chakula kilipokuwa tayari Vanessa alipamba meza vizuri kuliko kawaida. Aliweka maua katikati, na mshumaa pembeni na vitambaa vilivyokunjwa kwa umbo la moyo. Kisha akaenda kuwaita.
Alisimama mlangoni na kusikiliza kama atasikia kinachoendelea huko ndani .
Baada ya muda akaanza kugomlango kwa fujo.
" Damiani nini hiki. Doreen aliuliza.
" Sijui ni nani? Alijibu Damiani huku akitoka juu ya kifua cha Doreen. Alivaa taulo na kwenda kufungua mlango.
" Wewe una matatizo gani lakini?
Damian aliongea kwa sauti ya chini.
" Si ulisema chakula kukiwa tayari nije kuwaita?
" Sasa ndio ugonge kama kichaa?
" Kwahiyo kugonga kwangu kumekuja dirisha au umekasirika nimewataka kwenye wakati wenu mzuri?
" Toka hapa.
Alisema Damiani kisha akafunga mlango na kurudi chumbani"
" Mpenzi twende tukakae kwanza.
" Sawa ila watambue watu wako wawe wastaarabu.
" Sawa mama.
" Hila huyu dada ni kichaa mazima ipo siku utaamini usemi wangu.

walitoka na kwenda meza ya chakula,
Damian alishangaa,
"Wow, this is impressive."
Doreen naye alipendezwa na alichokiona.
" Waoooo baby Kumbe unaweza kuwa romantic kiasi hiki?"
Damian alijitapa:
"Anything for you baby."

Walikaa mezani alianza kula, huku Vanessa akiwa jikoni akiwatazama kwa jicho la pili. Mara simu ya Doreen ikaita. Aliinyanyuka na kwenda kupokea pembeni
"Hello....hee? Upo hospitali? Aisee... okay okay nakuja sasa hivi."
Alirudi sebleni na kusema:
"Damian baby, rafiki yangu anaumwa natakuwa nimfuate hospitali."
" Lakini tule kwanza.
" Hapana baby acha nimuwahi.
"Hakuna shida baby, usijali. Nitumie message nikipaswa kufuata."

Doreen aliondoka kwa haraka huku Damian akimsindikiza hadi nje.
Vanessa alipotoka jikoni na kusimama nyuma ya Damian akasema kwa sauti ya utulivu .
"Mgeni wako kaondoka kabla hata hajamaliza mpambano. Pilipili ni mbaya lakini inasaidia sana kushikisha adabu watu majeuri

Damian aligeuka kwa hasira,
"Vanessa! Unataka nini kutoka kwangu? Mbona unaniandama kila siku?"
Vanessa akasogea karibu na kumtazama kwa macho ya kujua siri:
"Unaniogopa Damian. Unajifanya kunidharau, lakini mimi najua... kuna kitu ndani yako kinanikubali."
Damian alitikisa kichwa kwa hasira, akijaribu kujizuia.
"Vanessa... unacheza na moto. Na ukikolea hutapata mtu wa kukuzima."
Vanessa alicheka taratibu,
"Sawa boss... basi acha nitafute kibiriti."
Aliondoka akaenda zake chumbani huku Damian akiwa amebaki na hasira.
" Hivi anajikuta nani hapa na mbona anajiamini sana?

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MY CRAZY HOUSE GIR 9---10  >>> https://gonga94.com/semajambo/my-crazy-house-gir-9-10

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
never give up harmonize
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest