Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

VERY HANDSOME 🌸Lover boy💓💓04

25th Aug, 2025 Views 46


Asante 🙏 nilichukua huyo nikaondoka zangu nikamuacha yeye anaendelea kusoma ..
Kuna watu wanapenda kusoma mh huyu kaka atakua na akili sana,, mke wake atakuwa na mtu wa maana sana... Nilijisemea moyoni
Nilifika nyumbani ..

Niliwakuta wenzangu wamekaa wanaangalia TV.
Mwenzetu sasa hivi unakaa chuo hadi jioni unatafuta nini? Aggy aliniuliza
Nilikuwa najisomea kingine nilienda maktaba ili niazime kitabu...

Mh hebu nikione hicho kitabu Penina aliongea huku akinisogelea...
Mh mbona unanukia pafyumu tofauti na yako hii si pafyumu ya yule kaka Gerson..

Ulikuwa na Gerson au 🤔 Penina aliniuliza
Sikuwa nae mimi nimesema nilienda maktaba nimeazima kitabu nimerudi nyumbani...
Angel unamtaka Gerson? Penina aliniuliza
Swali gani 🤔 hilo Gerson ni mwanaume anayependwa na wengi kwahiyo wewe pambana kivyako uhakikishe unaingia mikononi mwake mimi sina huo muda habu naombeni nikalalee.....

Nilienda zangu chumbani nikaelekea bafuni kuoga nilivua nguo 👗 nikanusa ile pafyumu ya Gerson nilijikuta napata hisia ambayo sijawahi kupata, nikajikuta na mimi naanza kuwa na hisia za kimapenzi juu yake..

Pepo shindwa katika jina la Yesu ni nini hiki leo hii naanza kumpenda huyu kaka. Mkaka mwenyewe ni bonge la HB haendani hata na mimi ana akili sana mimi ndio nitamuweza hebu nioge nilale mie ...
Nilioga haraka nikarudi kitandani kujitupa lakini akili yangu haikuacha kumuwaza huyu kijana aliyeteka hisia za kila mtu ....

Nililala nilikuja kushtuka usiku saa mbili niliamka nikaenda sebuleni kula nilikuta Aggy amepika.....
Dada Penina yupo wapi? Nilimuuliza Aggy
Ametoka kaenda kwenye sherehe ya rafiki yake mjini....

Mh 😯 Penina naye mara hii ana marafiki yupo vizuri 😂 niliongea.
Nasikia watu wanasema unajipendekeza kwa HB Aggy aliongea.
Mh akina nani hao wanaongea jamani...
Wanafunzi wa darasani wanakuona mara nyingi una mfuata mfuata.

Kama ni rahisi kujipendekeza hivyo na wao wamfuate kwani wamekatazwa yaani mtu nishindwe kusoma kisa halafu yule nipo nae kwenye grupu moja na ndio mwenyekiti mimi ni katibu tutashindwa vipi kuwa karibu...
Sawa mama kwanza mimi najua hauna hayo mambo 😁.

Si ndio hapo mama mchungaji mie nakuwaga vipi na hayo mambo ila naomba umsisitize ndugu yako awe anasoma tupo ugenini hata mitaa hatujaizoea ndugu yako ashaijua au sababu anaona tupo mbali na wazazi .
Tulikula kila mtu akaenda kulala, Penina alirudi usiku saa sita akagonga mlango bahati nzuri alinikuta nipo macho najisomea kile kitabu nilichopewa na Gerson nikaenda kumfungulia mlango akaingia ndani..

Usiniambie kuwa umekunywa bia 🍺 we Penina mbona unanukia pombe....? Nilimuuliza
Jamani kidogo tu kwani mtu hutakiwi kuonja bhana halafu leo ilikuwa ni sherehe kwahiyo mtu usifurahie..
Mh sawa ila punguza starehe ndugu yangu..
Niache nikalale bhana.....

Itaendelea .
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

VERY HANDSOME 🌸Lover boy💓💓04  >>> https://gonga94.com/semajambo/very-handsome-lover-boy-04

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
never give up harmonize
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
VERY HANDSOME ?Lover boy??
VERY HANDSOME ?Lover boy??

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest