Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:09

24th Aug, 2025 Views 3


Mimi nikafumba macho yangu kama vile nimelala, mke wangu alipoona hivyo aliingia bafuni, mimi nikageuka upande mwingine ndani ya moyo wangu nasema “Ooh Mungu wangu, ni nini hiki kimetokea, ni jambo gani hili?, kwanini umeruhusu ndoa kati yangu na Gabriella, ina maana nitateseka maisha yangu yote na ndoa hii nisiyoipenda kabisa. Mbona naona sasa ndiyo simpendi kabisa, sio mwanamke ninayemtaka mimi.”

Wakati huo Gabby alitoka bafuni, kisha alichukua simu yake na kwenda kukaa kwa kochi pale chumbani. Alikuwa ana amini mimi nimelala. Sasa anawasiliana na nani usiku wote huo na watu wanajua yeye yupo fungate.

Nitafanya nini?, inabidi niendelee kujifanya nimelala. Kukera inakera mwenzangu anatumia simu yake na mimi nipo tu hapo, tena kuna muda ana cheka. Ilikuwa kwa muda mrefu sana na baadaye alipanda kitandani. Sikufanya lolote mimi niliendelea kuwaza mambo yangu haga usingizi ulinichukua.

Asubuhi ilifika ambayo mchana wake tunatakiwa kusafiri. Kusema ukweli hii fungate naona kama isiwepo, nakereka tu na fungate, akili, moyo, mawazo yangu yote yapo kwa yule mwanamke. Hapo sasa mke wangu ameamka amevalia vizuri, ananiambia “baby unaona hii nguo nilinunua bei gani unajua?”

Nilimtazama na kusema “unajua mke wangu una matumizi ya ajabu sana haya bei gani?”
Akacheka na kusema “ushaanza hivyo mpenzi, pesa ikiwepo lazima itumike u know mimi kujibana siwezi na unajua.”

Nilitabasamu tu lakini ndani yangu nachukia. Mke wangu kununua nguo kwa laki 3 na kuendelea haoni shida na nguo ya ajabu, pochi ananunua bei za kutisha na ni vitu vya kawaida tu na hapo hataki ushauri.

INAENDELEA..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:09  >>> https://gonga94.com/semajambo/loml-love-of-my-life-09

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest