Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:02

24th Aug, 2025 Views 4


Nilimtazama tu, sasa huyu ndiyo mpenzi wangu G. Ni mwanamke ambaye sio mvumilivu, ana pesa mbele sio mambo mengine, anapenda anachotaka muda na wakati huohuo kifanyike na kiwe. Ni binti mzuri sana ila ana mambo mengi ambayo mimi kama mwanaume naona kabisa kwa ndoa inakuwa ni ngumu sana hivyo nilihitaji muda zaidi.

Nilimshika mkono, na kusema “baby wangu G, wala hata sio hivyo. Nina hofu tu, nina ogopa sana sijui hata itakuaje. Lakini ukweli ni kwamba natamani kukuoa hata sasa hivi, hofu tu.”

Gabriella alinitazama na kutabasamu akisema “mpenzi unaenda kuwa baba, hili ni jambo zuri sana kwetu, unaenda kuwa baba fanya kwaajili yetu. Tutafurahi sana.”

Nilitabasamu tu, sikuwa na la kufanya mimi. Kila mmoja alikuwa anasubiri ndoa yangu kasoro mimi hapa, mimi peke yangu ndiyo nilikuwa natamani ndoa isiwe. Ningefanya nini mimi, zaidi ni kukubaliana na ukweli kuwa natakiwa kumuoa Gabriella mchumba wangu wa muda mrefu.

Kila kitu kilikuwa sawa kabisa, maandalizi, familia, mavazi, ukumbi, kila kitu kilikuwa ni sawa kabisa. Mpaka wasimamizi wa ndoa yetu walikuwa wapo pale. Na kila mtu alikuwa anafurahia siku hii. Siku ilifika sasa, mimi na Gabriella kufunga ndoa yetu takatifu kabisa. Watu walifurahi, hakika ilikuwa harusi nzuri sana, ya kisasa na yenye furaha sana. Sijui nikuambie nini kila kitu kilikuwa safi kabisa.

Kama ungepata nafasi ya kumuona Gabriella sasa, ni kama vile anatamani dunia yote ingekuwa inajua kuwa yeye leo anafunga ndoa. Alikuwa amechangamka, ana furahia sana, amecharuka nakuambia simu anapost, anaandika kile anataka unajua vile ilivyo kwa mtu ambaye ametamani kitu kwa muda mrefu sana na sasa amekipata, ndiyo ilivyokuwa kwa Gabriella, alifurahi sana.

Ilikuwa ndoa nzuri sana, kanisani palijaa furaha na palichangamka sana. Ninakumbuka mimi peke yangu ndiyo nilikuwa kama mtu ambaye nalazimisha furaha.

INAENDELEA..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:02  >>> https://gonga94.com/semajambo/loml-love-of-my-life-02

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest