Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:12

24th Aug, 2025 Views 2


Tunapanga vitu huku yeye na simu, akimaliza anaweka pembeni kidogo inaita mpaka nachukia sasa niliamua nijikaze kama alivyosema wapo kwenye matatizo. Dereva alipiga simu kuwa amefika, nilimuelekeza afuate mizigo na kisha tuendelee na safari. Unajua tangu tunaingia ndani ya gari, mpaka tunafika nyumbani mke wangu na simu tu. Sikupenda kabisa hii tabia. Lakini nitafanyaje na nimeambiwa tayari kuwa ana matatizo.

Nilishuka na mke wangu, kama ambavyo ipo nyumba ni mpya lakini kila kitu kipo vizuri kabisa. Madam ambaye tumeandaliwa pale nyumbani alitupokea. Niliingia ndani na mke wangu.

Hakuoga hata zaidi alibadilisha nguo tu, alinibusu huku anaongea na simu na kuondoka zake. Nilibaki nina mshangaa tu mke wangu.

Nilipokuwa chumbani nilipata wazo nimpigie simu mama yangu, nilimpigia mama, mama alipokea na alisema “hutajwi mwanangu, tumetoka kuzunguma kuhusu wewe sio muda hapa, eenh niambie safari muda gani?”

Nilitabasamu na kisha nilimwambia “ndiyo maana nimepiga nikujulishe kuwa hatujasafiri kuna changamoto kidogo.”
Mama alishangaa na kuuliza “nini tena?”

Nilielezea kwa udogo tu na mama alisema “ooh jamani, Mungu awasaidie sana, naimani litapita tu.”

Nilisema kwa upole “hata mimi naamini hivyo mama, basi mimi napumzika kidogo tutawasiliana wakati mwingine, msalimie baba.”

Mama aliniambia “amekaa hapa anakusikia, amekukumbuka tu.”
Nikacheka na kusema “nawapenda wote.”
Tukacheka.

Nilijilaza kitandani, ile nafumba tu macho yangu. Yule binti huyu hapa, ninamuona kila mahali, naona kabisa amechukua moyo wangu, akili yangu, mawazo ana miliki mpaka usingizi wangu.

Nilifumbua macho na kusema “Ni nini hiki, kwanini nakuwa hivi?”
Kabla sijajijibu simu yangu iliita. Niliitazama kwa muda na kutabasamu, alikuwa ni rafiki yangu. Nilipokea simu hii na kusema “kaka!!”

INAENDELEA..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:12  >>> https://gonga94.com/semajambo/loml-love-of-my-life-12

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest