Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

KATOTO KA FORM FOUR Episode 1

25th Aug, 2025 Views 30



Kelvin alifika kwenye geti la Maramba Secondary School asubuhi yenye upepo mzuri wa bahari, akiwahisi wanafunzi wakipita pembeni yake wakiwa wamevalia sare zao za kijani na kahawia. Akiwa amejawa na matumaini na hamu ya kuanza kazi yake mpya, aliendelea mbele hadi ofisi ya mkuu wa shule, ambapo alipokelewa kwa tabasamu na Mwalimu Samuel, mkuu wa shule.

Mwalimu Samuel alimkaribisha Kelvin
rasmi, akimwonyesha maeneo muhimu ya shule hiyo na kumweleza taratibu zote za Maramba. Asubuhi hiyo ilipofika saa 1:30, kengere iligongwa na wanafunzi walikusanyika uwanjani kwa ibada ya asubuhi. Baada ya salamu rasmi, Kelvin alipata nafasi ya kujitambulisha mbele ya wanafunzi.

"Naitwa Kelvin, mwalimu mpya wa Baiolojia. Natarajia tutashirikiana kwa karibu katika safari yetu ya elimu," alisema kwa tabasamu na sauti ya kujiamini. Wanafunzi walimwangalia kwa makini, wakisikiliza kwa utulivu.

Baada ya siku mbili za kufundisha, Kelvin alipewa jukumu la kusimamia usafi wa shule kabla wanafunzi hawajaruhusiwa kuondoka. Wakati akisubiri wanafunzi kumaliza shughuli zao, aliwaangalia wakiendelea na shughuli zao, lakini macho yake yakatumbukia kwenye tukio moja la kushangaza. Aliona mwanafunzi mmoja akinywa maji akiwa ndani ya maabara, jambo ambalo lilimkera.

"Kwa nini unakunywa maji maabara?" aliuliza kwa sauti ya hasira huku

akimkaribia yule mwanafunzi. Huyu
mwanafunzi alikuwa amempa mgongo, na Kelvin hakuweza kuona sura yake.

Mwanafunzi huyo aligeuka taratibu, na Kelvin aliduwaa kwa mshangao. Mbele yake alisimama msichana aliyekuwa amevaa hijabu ya rangi ya nyeupe iliyomfunika kichwa chake kizuri. Macho yake makubwa na yenye rangi ya kahawia yalikuwa yamejawa na woga, huku uso wake ukiwa na rangi nyepesi iliyokuwa iking’aa kama vile mionzi ya jua la asubuhi. Hijabu yake iliongeza mvuto wa kipekee, ikimpa taswira ya msichana mwenye heshima na staha.

Kelvin alijikuta amezama katika mawazo ya uzuri wake wa asili, hali ilyofanya tukio la kugeuka lijirudie rudie kichwani kwa kelvin pia akihisi moyo wake ukidunda kwa kasi isiyoeleweka.

"Mwalimu... samahani..." msichana huyo alizungumza kwa sauti ndogo na ya aibu. "Nitakuwa mwangalifu siku nyingine."

Kelvin alirudi katika hali yake baada ya kuzama kwenye mawazo. Akajitutumua

na kumwangalia kwa utulivu. "Ah...
usijali... unaitwa nani?"

"Naitwa Briana," alijibu kwa sauti ya aibu, macho yake yakionyesha hofu ya kumkasirisha mwalimu.

"Sawa, Briana. Unaweza kwenda kipindi sasa," Kelvin alisema kwa sauti ya upole, huku akijaribu kuzuia mawazo yake yasizame zaidi. Lakini macho yake yalibaki yameganda kwa Briana, akiangalia jinsi alivyoondoka kwa adabu na utulivu, hijabu yake ikipepea kwa uzuri wa asili.

Wakati Briana alipokuwa anaondoka, Kelvin alihisi hisia za mchanganyiko zikimvaa. Hakuelewa ni kwa nini uzuri wa msichana huyu ulimgusa kwa namna hiyo, lakini alikuwa anajua jambo moja—Briana ni mwanafunzi wake kwa nini ahisi hivyo kasoma chuo kamaliza kakuta na wasichana wazuri wenye mashepu weupe warembo lakini wote hawajawahi kumgusa kama briana

.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

KATOTO KA FORM FOUR Episode 1  >>> https://gonga94.com/semajambo/katoto-ka-form-four-episode-1

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
never give up harmonize
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
VERY HANDSOME ?Lover boy??
VERY HANDSOME ?Lover boy??

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest