Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

PAKA WA MAMA KIZIBO SEHEMU YA SITA.

24th Aug, 2025 Views



Miaka kadhaa nyuma kampuni ya Multnational Oil Productions Indusries iliomba kibali na ikaruhusiwa kuwekeza nchini kwa kujenga kiwanda cha kuzalisha mafuta ya kula ya aina zote kutumia mbegu za mafuta.

Wataalamu wa kampuni hiyo walifikia uamuzi wa kuwekeza katika sekta hiyo baada ya kutembelea mikoa karibu yote nchini na kukuta imejaa fulsa za uzalishaji wa mafuta ya kula.

Kwanza, walikuta zaidi ya nusu ya mikoa yote inazalisha karanga, alizeti, ufuta, nazi, chikichi na mboga za majani ambazo wangeweza kuzalisha mafuta kwa wingi.

Pili, walikuta kuna uhitaji mkubwa wa mafuta ya kupikia na hivyo kuwa na uhakika wa soko la ndani hadi nje ya nchi kuanzia jirani hadi mashariki ya mbali.

Tatu, wawekezaji walikidhika na nishati iliyojaa hapa kwetu; kiasi kwamba walikuwa na uhuru wa kuchagua kama watumie umeme, gesi au makaa ya mawe.

Hakuna ambaye kwa kusoma ripoti yao ya uwekezaji angeweza kuwaza kuwa juu ya uwekezaji wao kulikuwa na siri nzito iliyojificha.

Siri hiyo ilikuja kugunduliwa na kijana Bakari ambayo pengine kwa bahati mbaya alijumuishwa katika harakati ambazo mwanzoni ulikuwa kama mtihani kwake.

Siku hiyo ya Jumatatu asubuhi alifuatwa na gari ya bosi wake bwana Arsenal Patel kumuwahisha uwanja wa ndege. Alikuwa anaianza safari ambayo hakuwa anajua huko aendako alikuwa anaenda kufanya kazi gani. Alichojua ni kuwa anakwenda Mwanza na maelekezo mengine yangemkuta huko. Hii kwake haikuwa kawaida; alizoea kabla ya safari anapewa maelekezo yote kabla hajaondoka. Lakini safari hiyo alikuwa hajui cha kwenda kufanya, hakuambiwa atakuwa huko kwa muda gani na ataripoti kwa nani na wala hakupewa masurufu ya safari.

Bakari baada ya kutua uwanja wa ndege wa Mwanza alitoka nje Jengo la wageni akachukua simu yake kwa lengo la kupiga simu kumweleza bosi wake kuwa amekwisha wasili mjini Mwanza; lakini kabla hajafanya hivyo mbele yake akajitokeza kijana mmoja wa kiume mwenye umbo la kadiri akiwa kasuka rasta. Alimsogelea Bakari na kujitambulisha huku akiwa katandwa na tabasamu usoni mwake " Nadhani wewe ni Bakari..... " Yule kijana alisema huku akimpa mkono Bakari.

"Ndiyo mimi ni Bakari" Bakari alisema huku nusu akishangaa na nusu akiwa na mashaka.

"Mimi naitwa Samwel Reikiza. Huku wamezoea kuniita Jah Sam. Nimeagizwa nije nikupokee nikupeleke hotel uliyoandaliwa" Jah Sam alijieleza kwa unyenyekevu.

" Ili niwe na uhakika, siyo vibaya nikajua umeagizwa na nani." Bakari alijikuta anauliza kwa kuhofia asije akaangukia mikononi mwa tapering.

"Nimeagizwa na Arsenal Patel. Aliagizwa ukifika upelekwe New Lake View Hotel. Huduma zako zote zimeshalipwa hivyo unakaribishwa Mwanza." Jah Sam alijieleza kwa kujiamini.

Baada ya maelezo hayo ya Bwana Samwel Rweikiza au Jah Sam Bakari hakuwa na ubishi zaidi ya kumfuata mwenyeji wake hadi ambako alikuwa ameegesha gari.

Walifika hotelini baada ya saa moja za mwendo. Bakari akafikishwa kwenye chumba alichopangiwa ambacho kilikuwa na jina la Kasuku maana vyumba vyote vya hoteli vilikuwa na majina ya ndege kama tausi, chiriku, kanga na wengine wengi. Chumba cha Kasuku kilikuwa ghorofa ya tano ambapo madirisha yake yalikuwa yanatazamana na ziwa Victoria.

Jah Sam alipohakikisha mgeni wake amefika salama hotelini alitoa taarifa kwa bwana Arsenal Patel huku Bakari akisikia na alipomaliza akamuaga mgeni wake.

"Endapo utakuwa na lolote chukua hii kadi yangu ina namba zangu unipigie." Jah alisema huku akimpatia Bakari kadi yake ya mawasiliano.

Baada ya Jah Sam kwenda zake Bakari alijilaza kitandani akiwa anatafakari. Alikuwa akiwaza juu ya lengo la hiyo safari yake. Alikuwa kaletwa Mwanza na kupangiwa Hoteli ya nyota tano. Kwa kawaida yeye alikuwa kazoea kufikia maeneo ya Buzuruga, Nyamagana na pembezoni mwa mji kulingana na uwezo wake. Alishangaa safari hii kuletwa kwenye Hoteli ambayo atatumia mshahara wake wote endapo atakuwepo hapo kwa siku mbili tu.

Kitu kingine kilichomtia shaka ulikuwa ni utaratibu wa yeye kama mfanyakazi kusafirishwa kama kifurushi; amechukuliwa na gari nyumbani kwake, analipiwa nauli ya ndege, anatumiwa gari ya kumpokea, anapelekwa hotelini ambako nako amekwisha lipiwa. Hata ambaye hakwenda shule lazima angelitilia shaka huduma hizo zote

Akiwa bado anajiuliza maswali pale kitandani ukaingia ujumbe kwenye simu yake kutoka Benki kuwa kwenye akaunti yake kumewekwa shilingi milioni kumi na jina la muwekaji pesa likisomeka Deus Paka.

"Deus PAKA !" Bakari alijikuta anatamka kwa sauti kubwa iliyojaa mshangao.

TUMEONA NDUGU YETU BAKARI AMEMWISHA FIKA MWANZA. AMEPOKELEWA NA JAH SAM NA KUPELEKWA HOTELI YA KIFAHARI YA NEW LAKE VIEW HOTELI NA BAADAE KUINGIZIWA SHILINGI MILIONI KUMI KWENYE AKAUNTI YAKE ZILIYOINGIZWA NA DEUS PAKA.

TUUNGANE SEHEMU YA SABA TUONE NINI KILIENDELEA. HUKO TUTAJUA UKARIMU HUU ANAOFANYIWA BAKARI NI WA KAMPUNI, BOSI WAKE ARSENAL PATEL AU KUNA NAMNA INAMUWINDA..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

PAKA WA MAMA KIZIBO SEHEMU YA SITA.  >>> https://gonga94.com/semajambo/paka-wa-mama-kizibo-sehemu-ya-sita

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
never give up harmonize
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
VERY HANDSOME ?Lover boy??
VERY HANDSOME ?Lover boy??

RATIBA YA SIMULI ZETU

Ratiba ya Simulizi

  • PAKA WA MAMA KIZIBO SEHEMU YA TATU. 25-08-2025 05:55

Ratiba ya Simulizi

  • PAKA WA MAMA KIZIBO SEHEMU YA SABA 25-08-2025 07:00

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest