Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

PAKA WA MAMA KIZIBO SEHEMU YA PILI

24th Aug, 2025 Views 17



Saa Sita mchana Mwanamtama alikwenda ofisini kwa Bakari. Alipoingia alimkuta Bakari kama alivyomwacha; amekaa, kajiinamia na machozi yakiwa yanamlengalenga.

"Bakari, suala lako ni zito sana; na usipoangalia litaharibu hatma yako kabisa. Nilikuwa nikiwaza nikusaidie namna gani. Labda kama utaafiki wewe mwenyewe tujaribu kubahatisha. Hatuwezi kukaa tu kusubiri hawa wahindi wakurarue." Mwanamtama alimsemesha Bakari huku akikaa juu ya Meza baada ya kuhakikisha amefunga komeo la mlango wa ofisi ya Bwana Bakari.

Bakari aliposikia maneno hayo akafuta uso na kumwangalia Mwanamtama. Hakusema kitu ila kwa namna alivyomwangalia Mwanamtama ni kama mtu aliyekuwa akisubiri kwa hamu kusikia huo msaada ni wa aina gani.

"Kaa hadi saa kumi na mbili. Utoke ukapande mabasi ya kwenda Tandika kupitia Mwembe Yanga kisha ushuke kituo cha Gereji. Ukishavuka barabara uende mbele kidogo kisha upinde kulia. Fuata hiyo barabara hadi utakapoikuta nyumba yenye rangi ya kijani na bati la blue. Ukifika gonga mlango na ulizia Ustaadhi. Huyo babu anaweza kukusaidia kutatua hili tatizo lako. Ameshawasaidia watu wengi kuwaokoa katika majanga makubwa zaidi ya hili lako." Mwanamtama alikuwa akimweleza Bakari kwa kituo huku akihakikisha kila neno linaingia masikioni mwa Bakari.

"Nakushukuru sana Mwanamtama kwa msaada wako. Kwa msala huu ulionikuta hata ungesema niende wapi mimi ningekwenda." Bakari alikubali maelekezo hayo huku uso wake ukionyesha matumaini.

Kama alivyoelekezwa na Mwanamtama Bakari alikaa ofisini hadi saa kumi na mbili jioni akafunga ofisi na kwenda kupanda mabasi ya Tandika. Alishuka kituo cha Gereji na kufuata barabara kama alivyoelekezwa.

Giza lilikuwa limeanza kuingia. Alifuata barabara ya mkono wa kulia na kuanza kutembea. Alipita nyumba ya kwanza, ya pili, na nyumba ya tatu. Alipofika usawa nyumba ya nne akasikia sauti kutoka katika moja ya vyumba vya nyumba hiyo. Sauti hiyo ilikuwa kama ya mtu anayeugulia maumivu makali. Alitaka kuipuuza aendelee na safari yake; mara sauti hiyo ikasikika tena na safari hii sauti hiyo ilikuwa kali zaidi. Bakari akapata hisia kuwa huyo aliyetoa sauti kama ni mtu basi alikuwa anakabiliwa na hatari kubwa.

Taratibu Bakari akachepuka na kusogelea dirisha ambalo alihisi sauti inatokea hapo. Alinyatia huku akiwa kakingwa na kichaka cha michongoma hadi akafika dirishani. Alipofika dirishani akachungulia. Ndani ya chumba hakukuwa na mwanga mkubwa. Aliweza kumwona mtu mmoja amekalishwa juu ya kiti huku akiwa amesimamiwa na watu wawili.

Bakari alijitahidi kufinya macho ili awatambue au awakariri wale watu wawili waliosimama na yule aliyekuwa amefungwa kamba kwenye kiti.

Pamoja na mwanga kutokuwa rafiki Bakari alibahatika kuisoma sura ya mtu mmoja ambaye alikumbuka kuwahi kumwona sehemu fulani ambayo ameisahau.

"......sema lile moja umeliweka wapi. Haya yalikuwa matatu; hapa yamebaki mawili tu." jamaa aliyekumbukwa na Bakari alikuwa akimhoji yule mateka kwenye kiti huku akimchapa mijeredi.

Kauli ya yule jamaa ilimfanya Bakari aongeze umakini wa kuchungulia na kusikiliza. Alipata hamu ya kujua hayo anayodaiwa yule mateka ni vitu gani.

Bakari akiwa kazama kwenye utafiti na kusahau kabisa safari yake kwa ustaadhi, ghafla aliguswa na mkono begani mwake. Bila kutaka kujua nani kamgusa alirusha teke la punda akasikia kishindo cha mtu akianguka kwenye michongoma. Bakari bila kujua anaelekea wapi akakurupuka mbio akiwa anakata kona moja baada ya nyingine gizani.

Kwa mbali alisikia kikundi cha watu wakimkimbiza. Na yeye akaendelea na kukimbia hadi akakikuta kibanda cha mkaa kikiwa wazi akaingia na kujificha kwenye magunia ya mkaa.

Akiwa kajificha kwenye magunia ya mkaa nje ya kibanda akasikia kikundi cha watu wakiulizana wapi alipopotelea mtu waliyekuwa wakimkimbiza.

"Ebu mmoja aingie kwenye hiki kibanda inawezekana yule mtu akawa amehificha humu" mmoja ya wale watu aliwashauri wenzake.

Kusikia hivyo mapigo ya moyo ya Bakari yaliongeza kasi. Alijua wazi endapo watakikagua kibanda haitachukua dakika nyingi yeye kupatikana. Akajikuta akitaja majina ya mitume wote na mungu wake.

TUMEONA JINSI BAKARI ALIVYOJIINGIZA KWENYE JANGA JINGINE. JE ATASALIMIKA ?

UNGANA NAMI SEHEMU YA TATU UWEZE KUJUA NI NANI WALIOKUWA WAKIMKIMBIZA BAKARI NA BAADA YA MSAKO NINI KILIENDELEA.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

PAKA WA MAMA KIZIBO SEHEMU YA PILI  >>> https://gonga94.com/semajambo/paka-wa-mama-kizibo-sehemu-ya-pili

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
never give up harmonize
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
VERY HANDSOME ?Lover boy??
VERY HANDSOME ?Lover boy??

RATIBA YA SIMULI ZETU

Ratiba ya Simulizi

  • PAKA WA MAMA KIZIBO SEHEMU YA TATU. 25-08-2025 05:55

Ratiba ya Simulizi

  • PAKA WA MAMA KIZIBO SEHEMU YA SABA 25-08-2025 07:00

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest