Asubuhi hakuweza hata kwenda chuo nikaenda mimi na Aggy..
Nilivyomuona Gerson nilitabasamu nilienda hadi alipokaa nikamsalimia...
Vipi umeamkaje? Salama sijui wewe alinijibu
Niko poa kitabu nimesoma nimeelewa pia ni kizuri nimechukua bahadhi ya maswali nahisi nitaelewa..
Vizuri jitahidi hivyo hivyo halafu kingine usiwe unakaa back bhana njoo ukae huku mbele...
Kabla sijajibu alikuja mdada mwingine huyu anaitwae Nice ni aina ya wale watu wenye mashauzi na matawi ya juu halafu baba yake alikuwa ni mtu tajiri mwenye pesa zake na ni maarufu sana......
Gerson sorry nimeingilia mazungumzo yako kuna maswali yananichanganya nataka unielekeza sijui utapata muda saa ngapi ?
Hata sasa hivi ๐ค njoo nikuelekeze sipo bize.
Sawa ngoja nichukue begi nakuja......
Gerson baadae basi.... Nilimuaga
Sawa niliinuka nikaenda kukaa napokaaga nikawa namuangalia tu mara alikuja yule dada akasogeza kiti akakaa karibu na Gerson wakaanza kufundishana yule dada muda wote akawa anamuangalia tu Gerson badala ya kumsikiliza..
Roho ilikuwa inaniuma nusu nipasuke kwa hasira..
Basi baada ya muda kidogo aliingia lecture mzee wa discussion akatupa kazi kisha akaondoka...
Kila mtu alienda kwenye kundi lake ili tujadiliane.. kidogo nikapata ahueni Nice akaenda kwenye grupu lake....
Tukiwa kati kati ya majadiliano alikuja Nice na kiti chake akaja kukaa pembeni ya Gerson..
Jamani naombeni nikae hapa kule mimi sielewi labda hapa nitaelewa...
Gerson alimwambia sawa karibu tu ...kile kitendo sikukipenda niliinuka nikachukua begi langu nikatoka nje nikawa natembea taratibu naelekea nyumbani kwa mguu na hapo juu wingu โ๏ธ la mvua ๐ง๏ธ limetanda na sina hata mwamvuli wa kujikinga na mvua โ wivu huu๐.....
Angel....... Angel nilisikia sauti ya Gerson ikiniita kwa nyuma... Niligeuka
Unasemaje Gerson? Nilimuuliza
Mbona umeondoka kwenye discussions huku umechukia kuna kitu kimekuuzi mbona sijakuzoea...
Hamna kitu nataka tu niwahi nyumbani najihisi tumbo linauma..
Sawa kuna dalili ya mvua naomba basi nikusindikize nyumbani...
Mh unisindikize nyumbani sasa ๐ค na wewe si utaloa na vipi kuhusu kujadiliana yale maswali?
Hapana nina usafiri nimepaki hapo sheli nitakupeleka pia kuhusu maswali nimeshawaelekeza jinsi ya kufanya ... Gerson alinijibu.....
Mh una gari? Nilimuuliza
Ndio ninalo..... Nilishangaa sijawahi kumuona na gari hata mara moja basi tukapitia sheli kweli nikakuta kapaki gari yake tukaingia ile tumeingia tu na mvua kubwa ikaanza kunyesha...
Si unaona ungeloa na mvua leo haya nielekeze nyumbani kwenu nikupeleke..
Nilimuelekeza akanipeleka hadi nyumbani..
Asante kwa kunileta hadi nyumbani karibu hata ndani basi.... Niliongea
Asante ๐ hata siku nyingine nitaingia kingine subiri mvua ikate utaloa ukishuka sasa hivi kwenye gari.... Gerson aliongea
Sawa kwanini una gari na hautaki kuja nalo hadi chuo halafu wewe ni mwanafunzi uwezo wa kuwa na gari umetoa wapi? Nilimuuliza bila uoga maana sasa hivi nilikua nishaanza kumzoea.
๐ Kwamba kuwa na gari ni ajabu mbona ni kawaida chuo sio kama shule ya msingi mule darasani kuna watu wana maisha yao wengine hadi wameoa na wengine wameolewa hadi na watoto juu...
Je nini kitafuata??
Full 1000
Whatsapp 0742133100.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments