Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

PAKA WA MAMA KIZIBO SEHEMU YA SABA

24th Aug, 2025 Views


Baada ya bwana Bakari kuachwa hotelini hakutoka nje ya chumba chake. Muda mwingi aliumaliza akiwa amaangalia vipindi kwenye televisheni kubwa ya kisasa iliyokuwa imeunganishwa na ving'amuzi vinne tofauti.

Ilipofika saa mbili usiku aliitisha chakula na matunda vikaletwa na mhudumu katika chumba chake.

Alipomaliza kula akaenda kuoga tayari kwa kwenda kulala. Wakati anaweka nguo zake kwenye kabati simu yake ikaita.

"Mimi ni Jah Sam naongea. Naomba ujiandae, kesho alfajiri nitakupitia kuna sehemu nimeambiwa nikupeleke" Samwel Rweikiza aliongea taratibu kama anayekusudia kila neno liingie barabara kwenye masikio ya Bakari.

Kabla Bakari hajauliza wala kusema chochote simu ikakata. Mwanzoni Bakari alidhani ni tatizo la mawasiliano hivyo akajaribu kuipigia namba hiyo mara kadhaa ili apate maelezo ya kina; alichoambulia ni kuwa "namba unayoipigia haipatikani jaribu tena baadae".

Akiwa kakerwa na kitendo hicho Bakari alijitupa kitandani kujaribu kuutafuta usingizi; lakini hakuupata akaishia kugalagala hadi karibu kunakucha.

Wakati kausingizi kanamzengea akasikia mlango wa chumba chake ukigongwa. Akiwa kajawa na usingizi aliamka na kwenda kufungua mlango. Mlangoni akamkuta mhudumu wa kiume wa hoteli amesimama.

"Mheshimiwa. Jah Sam yuko mapokezi anakusubiri. Mtaondoka kuanza safari dakika kumi zijazo. Hivyo anaomba ujiandae". Mhudumu baada ya kufikisha ujumbe kwa Bakari akafyatuka mbio kwenda zake kama anakimbia moto.

Bakari bila kuchelewa akaingia bafuni kuoga, akavaa na kuelekea alipoliweka begi lake la nguo ili alibebe. Lakini kabla hajaligusa begi ujumbe ukaingia kwenye simu yake.

"Usibebe mzigo wowote. Tunakwenda tunarudi". Ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Jah Sam.

Bakari baada ya kuusoma ujumbe huo akabeba simu yake akafunga chumba na kushuka kwenda mapokezi.

Alipofika mapokezi akamkuta Jah Sam anamsubiri. Wakasalimiana na kuongozana kwenda kwenye Gari.

Gari lililokuja siku hiyo halikuwa Range Rover kama walilotumia kutoka uwanja wa ndege jana yake; hili lilikuwa ni Toyota Land Cruiser kama wayotumia watalii mbugani.

Hawakupoteza muda pale chini Bakari na Jah Sam wakaingia kwenye Gari na kuanza safari.

Wakiwa katika mwendo Bakari akavunja ukimya kwa kumwuliza mwenyeji wake "Kwani tunaelekea wapi ?"

Akiwa kama anashangaa Jah Sam akajibu " ....nilidhani unajua. Tunaelekea Lamadi. Ila sijui ni wapi hasa na nini tunakwenda kufanya".

Kuanzia hapo hayupo aliyeongea hadi walipofika karibu na mji wa Magu ambapo kulikuwa na kituo cha doria cha askari walipoamriwa waegeshe gari yao pembeni.

"Wote shukeni tunafanya ukaguzi wa gari" kiongozi wa kile kituo aliwaamuru akina Bakari. Bila ya kukaidi wote wakashuka.

Bakari na Jah Sam waliposhuka askari watatu wa Dorian wakaanza kulikagua gari. Haikuchukua hata dakika tano wakasikia askari mmoja akisema " na hawa wanayo. Haya hapa."

Askari watatu waliliacha gari wakawa wanakwenda kwenye hema lao ambalo walilitumia kama ofisi huku wakiwapa ishara Bakari na mwenzake wawafuate. Miongoni mwa wale askari watatu waliokagua gari mmoja wao alikuwa ameshika mfuko mbadala mweusi ambao ndani yake kulikuwa na kitu.

"Unaujua ule mfuko ?" Bakari alimuuliza Jah Sam ambaye saa hiyo macho yalikuwa yamemtoka kwa hofu.

"Hapana. Sijui chochote kuhusu ule mfuko na sikumbuki kuuona" Jah Sam alijibu akionyesha hata usoni kuwa ni kweli alikuwa hajui kitu.

Baada ya Jah Sam na Bakari kufika kwenye hema yule kamanda mkuu wa doria akaingiza mkono kwenye ule mfuko na kutoa vipande vitatu vya dhahabu.

"Hii ni mali ya nani na mnapeleka wapi. Naomba vibali vyake". Kamanda aliongea huku akiwaangalia akina Bakari usoni.

Kwa karibu dakika tano Bakari na mwenzake Jah Sam walikuwa hawana mawasiliano na vichwa vyao hadi kamanda alipowauliza kwa mara nyingine kutaka wampatie maelezo ya vile vipande vya dhahabu.

Bakari ndiye aliyekuwa wa kwanza kurudiwa na fahamu. Alijua wazi kuwa hapo walipokuwa hawakuwa salama tena na kama watalegea wataishia jela.

"Vibali vyake vipo. Ngoja nikaangalie kwenye gari." Ilibidi Bakari adanganye ili kuvuta muda wa kujua namna ya kutoka japo ukweli wa mambo hakujua habari zozote kuhusu madini yale wala mengine katika maisha yake.

" ......kama mnavyo vibali nenda kavilete" kamanda alimruhusu Bakari akalete vibali.

Bakari akatoka pale haraka kama kweli anakwenda kufuata Vitali kwenye gari lakini ukweli wa mambo alijua hakuna kibali chochote anachokijua. Bakari alikuwa anajua ana milioni kumi na zaidi kwenye akaunti yake. Laiti hizo zingekuwa ni pesa taslimu angeweza hata kuzitoa zote kama hongo ili ajinasue kwenye msala huu lakini fimbo ya mbali haiuwi nyoka.

Alipofika kwenye gari akajifanya kama kweli anatafuta kitu; hapo likamjia wazo la kumpigia simu Arsenal Patel ili kumweleza yaliyowasibu.

Kabla hajapiga simu akasikia akiitwa kwenye hema la doria.

Bila ya kujua kama anaitwa kwa heri au kwa shari akafunga mlango wa gari na kuelekea alikoitwa kwa mwendo wa kinyonga. Alikuwa anakwenda kwa wasiwasi isije ikawa Jah Sam kamfanyia fitina ili ajiokoe. Hata hivyo alipiga moyo konde akajivuta hemani na kwamwachia mungu muweza wa yote aamue.

HAYA SASA MAMBO YAMEANZA KUCHANGAMKA. BAKARI NA JAH SAM WAMEKAMATWA NA ASKARI WA DORIA WAKIWA WAMEBEBA VIPANDE VYA DHAHABU AMBAVYO HAWAKUWA NA HABARI NAVYO. JE WATASALIMIKA NA KUENDELEA NA SAFARI YA LAMADI.

TUKUTANE SEHEMU YA NANE YA SIMULIZI YETU ILI TUJUE NINI KILIENDELEA..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

PAKA WA MAMA KIZIBO SEHEMU YA SABA  >>> https://gonga94.com/semajambo/paka-wa-mama-kizibo-sehemu-ya-saba

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
never give up harmonize
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
VERY HANDSOME ?Lover boy??
VERY HANDSOME ?Lover boy??

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest