SIMULIZI : KISURA WA DAMPO??
(nilizaliwa na kichaa, nikazaa na ceo)
Sehemuya 6 na 7
Sasa nikaona nikimbie, miguu nisaidie, maana sikutaka kutoa pesa ambazo nilikuwa naziweka kwaajili ya mwanangu, sasa katika kukimbia na ukilinganisha nilikuwa na mimba, nikaishiwa na nguvu nikiwa kwenye ile barabara ya france corner arusha na kuanguka, sasa kuna gari lilikuja na kuchuna break mbele yangu kisha likasimama, na dereva akashuka akawa ananitukana kwa kutokuwa mwangalifu, ila nilikuwa namsikia ila sikuwa na nguvu, ukilinganisha sikuwa nakula vizuri na nilikuwa na mimba, ndio Yule boss wake ambae alikuwa anamuendesha akashuka, wakati huo hata nguvu za kumuangalia sikuwa nazo, nikasikia akisema “ ni mke wangu mpeleken hospital…
Basi wakanibeba mpaka hospital ya AICC ambapo niliwekewa kwanza drip ya kuengeza nguvu kisha wakanipima na ultrasound ambapo niligundulika nina mimba ya mtoto wa kiume, bado sikuwa na nguvu za hata kuangalia ila nilimsikia namna ambavyo Yule mwanaume alikuwa anashangilia pale…
Basi nikapatiwa matibabu na nikajikuta nimepitiwa na usingizi maana nilishachoshwa na mihangaiko hivyo nikalala zangu tu…
Nimekuja kuamka ni asubuh, na mkono wangu, nilipofungua macho nikashangaa nakutana na sura ya mackmill akiwa ameshika mkono wangu huku akiwa amepitiwa na usingizi, na hapo tulikuwa wodini, ila kulikuwa na vitanda vitano ila hakukuwa na mjamzito hata mmoja wala mtu ambae alikuwa anajifungua hivyo tulikuwa pekee yetu tu…
Basi nikaamka kisha nikakaa nikashangaa anaamka na yeye kisha akasema “ umeamka mrembo…
Nikabaki nimetoa macho maana sijawah kuitwa mrembo, na kama alijua hivyo akatabasamu na kusema “ baada ya kunionjesha utamu ukanitoroka unajua nimekutafuta kwa kiasi gani?...
“ embu nambie ilikuwaje mpaka ukanikimbia au ulijua kuwa sitataka kuzaa na wewe na wakati nilishaapa kuwa nitakuoa, akasema mackmill na wakati wote mimi nilikuwa kimya tu nisijue natakiwa kumjibu nini kwa wakati ule….
Basi bana nikahudumiwa pale, na kuanzia nimezaliwa sikuwah kwenda hospital na wala kuchomwa sindano hivyo ilikuwa patyashika wakati wananitoa drip, maana nilishtuka nina drip na haiumi, ila wakati natolewa ndio nakuja kugundua kuna sindano nimewekewa , nikaanza kuleta usumbufu, wakanituliza pale, nikaanza kulia kisha nikasema “ mimi ni chokoraa tu, mmekuja kunichoma masindano yenu yenye sumu ili mniue kama mama yangu, kwani nani anapenda kuzaliwa na mama kichaa ili adharaulike, kwanini mnanifanyia hivi lakin, nikawa nalalamika pale na Yule mwanaume alikuwa kimya anawaacha manurse wafanye kazi yao…
Sikuwa na tatizo lolote lile kiafya zaidi ya kuwa na upungufu wa nguvu, sikuwa na UTI wala malaria, yaan ingawa nilikuwa nakula machakula ya hovyo ila damu yangu ilikuwa ni nyingi tena ni safi sana, mpaka manurse wakashangaa maana kila ambae alikuwa anakuja na nimjamzito ni lazima atakuwa na upungufu wa damu au UTI, nadhan mama wajawazito wanalijua hilo, ila kwa upande wangu ilikuwa tofauti kabisa, sikuwa naugonjwa wowote ule, basi siku hio nililala hospital na asubuh yake akaja mama mtu mzima kuniletea chakula, na nilipomuangalia vizuri nikagundua ndio Yule mama yake na mackmill ambae nilimuona siku ile nilipolala na mack….
Aliponiona alifurahi sana kisha kwa sauti ya bashasha kubwa akasema “ kwanini ulikuwa unakimbia na mtoto wetu, unajua ni kiasi gani mwanangu alikuwa anahangaika kukutafyuta, unajua ni kiasi gani tulikuwa tunataka mtoto, akawa anasema Yule mama…
“ mama muache husqer Apumzike bana, akasema mack na mama yake akamtoa mwanae nje kisha akamuuliza, “ alikuwa nje nini kimasomo, ila mbona kavaa nguo chakavu hivi kama omba omba, kiukweli niliposikia vile nilijisikia vibaya mno, maana nilidhan labda na mama yake ananipenda, ila kumbe anajua mimi natoka kwenye familia kama zao….
NAKUJA……………..
MREMBO WA DAMPO 7
(nilizaliwa na kichaa, nikazaa na ceo)
Mwandishi HURU MEDIA
Sio siri nilijisikia vibaya sana, kumbe huu upendo ambao mama yake na mack ananionesha ni upendo wa kinafki sana, kumbe anataman mwanae aoe mwanamke ambae ana hadhi kama ya kwao, ila sikutaka kuuliza, maana anagalau hata nimelala kwenye godoro kwa mara moja, manaa nilikuwa kila siku nalala kwenye maboksi kwenye maisha yangu yote…
Basi niliruhusiwa siku hio maana sikuwa na shida yoyote ile ya kiafya,na mackmill akawa anataka niende kutibiwa kwao, sikuweza kukataa, kwa maana kwanza sikuwa na sehemu ya kwenda, basi akanichukua mpaka kwenye nyumba moja hivi, sikuwa najua kama ni kwao au laa, sijawah kukaa kwenye nyumba hata mara moja kwenye maisha yangu alafu kwa mara ya kwanza nakuja kukaa kwenye hekalu…
“ hapa ni kwako? Nikamuuliza mack ila alitabasamu na kusema, “ hapa sio nyumban kwetu ila hii ni hotek ya baba yangu, ni kwamba hakuona kama kuna mapokezi kule chini? Akauliza, sikuwa na cha kumjibu maana hata hayo mapokezi nimeyaona ila nikajua ndio namna ambavyo matajiri huwa wanaishi, hivyo nikajua ni wafanyakazi wao tu…
“ ohhh nimeona watu wanainama inama, ila watu wamapokezi inaonekana wanakuogopa na mack akaanza kucheka kisha akasema “ sio kwamba wananiogopa ila huwa wanafanya hivyo kwa kila mteja, maana ukarimu mara nyingi huwa ndio unaamua kama mteja anatakiwa kurudi au asirudi tena, akasema mack na mimi nikatabasamu tu, maana sikuwa na kitu ambacho nilikuwa naelewa kabisa..
Basi akanionesha likitu kama sanduku ukutani kisha akasema “ utabonyeza hapa kama utakuwa unasikia baridi na utapata joto, maana si unajua huu mkoa na baridi tena, nikaitikia tu ndio maana hakuna kitu hata kimoja ambacho nilikuwa nakielewa pale….
Basi akanambia kuwa anaenda kunifuatia chakula, akaniuliza napenda kula nini ila hata sikuwa na cha kumjibu maana hata vyakula vizuri sikuwa navijua, maana niliishia kula mabaki ya chakula tu, tena unakuta yametupwa, ndipo tunaenda na wenzangu tunakigombania na kukila, kwa hio ile ladha halisi ya chakula hata sijawah kuipata hata mara moja kwenye maisha yangu……….
Basi akanileta supu kisha akasema “ nimekuletea kitu cha bei nafuu, kama hautaweza kula utanambia..
Nilimshangaa yaan mm nishindwe kula chakula si nitakuwa nimechanganyikiwa, chakula chenyewe kitamu kama nini, weee kuweza , nikaanza kunywa ile supu kama sina akili nzuri, na mackmill akaniongezea bakuli jingine nikagonga, yaan nilikunywa supu bakuli kama sita hivi, yaan nilikula mpaka basi…..
Nimemaliza kula akawa ananiangalia kisha akasema “ umeshiba au nikuongezee?....
Nataka maji ya kunywa, nikasema nikashangaa naletewa chupa ya maji, alafu angalia hizo safar za chooni, yaan supu ujumlishe na maji ya kunywa yaan ni tafran tu….
Nimemaliza nikalala zangu, ila kila dakika nilikuwa naamka naenda chooni, wakati wote huo mack alikuwa amekaa zake sehemu yuko busy na simu yake, hakuwa hata ananifatiliza, yaan tumbo ni kama lilijaa maji, basi tukashinda hapo mpaka usiku, akaniuliza nataka kula nini, nikamjibu tu nataka chakula kizuri, maana sikuwa najua nhata chakula kizuri ni kipi, ambacho labda watu ndio wanakipenda, basi akaniletea chips kuku na mishkaki, nyie nilikula sahani mbili, mpaka akanambia huyu mtoto sijui kama atatoka maana badala umnenepeshe akija duniani unaanza kumnenepesha akiwa tumboni….
Sijui ni kwanini yale maneno yake yalinikera sana, nikaanza kulia, yaan nililia kama nimefiwa vile, akaanza kunifata kisha akaniuliza unalilia nini?...….
.Je nini KITAENDELEAAA!! ".