SIMULIZI : KISURA WA DAMPO
(nilizaliwa na kichaa, nikazaa na ceo)
SEHEMU 3
Sasa ile nimetoka tu nje ya ule mlango, na hapo ilikuwa ni tayar asubuh, nikakutana na Yule dada ambae alikuja na mama yake Yule kijana, ambae hata sikuw namjua jina lake kisha akaniambia “ najua una maisha magumu na umekuja hapa kuchukua pesa za mwanaume wangu, yaan wanawake wengine hata akili ya kujiongeza hawana, unavyoona kuwa huyu mwanaume anaweza kuwa na mwanamke mchafu na unaenuka dhiki kama wewe, mackmill ni wangu na daima atakuwa wangu kwenye maisha yangu yote, akasema kwa kijitapa…
Kiukweli sikutaka hata kubishana nae, nikaanza kuondoka zangu kimya kimya, ila alipoona nampuuza sijui ndio hasira zake zikampanda, akaanza kunitukana na kusema “ hizo pesa ambazo amekupa mac usifikirie kama zitakutoa kwenye umaskin wako…
Hata kama nilikuwa nina dhiki na shida kiasi gani, ila sikuwa nataka kabisa kudhalilishwa, aisee niliitu[pa ile kard ambayo yuule kijana ambae baadae nilikuja kujua anaitwa mackmill alinipa kisha nikaanza kuondoka huku machozi yakiwa yananitoka….
Nilienda mpaka nilipomuacha mama yangu, nikakuta watu wamemzunguka pale, nikasogea mpaka alipo, nikashangaa anatoa wadudu, aisee nilishangaa, hata kama nilikuwa sijasoma ila isingewezekana kwa masaa kadhaa tu ambayo nimeondoka ndio mama yangu aoze na atoe wadudu kama alivyokuwa wakati ule…
Kuna watu wakaanza kuhusisha tukio la mama yangu na imani za kishirikina, wengine wakawa wanasema ni kichaa huenda alikuwa na maradhi yake, yaan kila mtu akawa anasema jambo lake, kiukweli sikuwa na la klufanya zaidi ya kulia tu, yaan nimetoka kuliwa huko nikijua mama yangu nitamkuta salama, na badala yake nimemkuta kafa tena kaoza vibaya mno…
Nililia sana, mwisho watu wa manispaa wakaja na kumchukua kisha wakaenda kumzika kimanispaa maana hatukuwa na ndugu, jamaa wala rafiki kwa kipindi chote kile ambacho nilikuwa naishi na mama yangu pale jalalani…
Basi sikuona haja ya kuendelea kukaa pale pale mtaani, nikaona nihame kambi, nikaja kusikia kuna watoto wa mtaani ambao wanajifichaga kwenye lorry, nikataka na mimi wanifundishe, haikuwa kazi rahisi, ila niliingia kwenye moja ya mzigo , yaan niliingia kwe ye salfet kisha wakaja kunijazia majani kwa juu, na huyo ambae alikuwa anasafirisha alikuwa anasafirisha mchele, hivyo nikawa nimekaa na kama gunia la mchele kisha nikatoka mkoani mpanda mpaka jijini arusha…
Nilipohakikisha nimefika nikatafuta namna ya kutoka kisha nikaondoka zangu, na kwakuwa sikuwa na pa kuishi nikaishia kuwa naishi jalalani maana ndio maisha ambayo nilikuwa nimeyazoea, nilikuwa mrembo sana, na machokoraa wa eneo hilo wale wa kiume wengi ambao walikuwa wanalala pale samunge wakawa wananipenda maana ni kweli nilikuwa na sura nzuri na umbo flani hivi maridhawa, wakawa wanataka kunibaka mara kadhaa ila nikawa napambana nao…
Siku moja tumelala zetu kwenye yale maboksi pale pale samungee saa ngapi sungu sungu wasije kutudaka na kutupeleka ndani wakidai kuwa sisi ni wezi, yaan nilijisikia vibaya, maana kwenye maisha yangu yote nilikuwa nakula maembe yale yaliotupwa na makatiti, yaan sijawah kula chakula kinachoeleweka hata mara moja, na hapo sikuwah kuona siku zangu kwa miezi kama mitatu, na kwakuwa sikuwa na elimu sikujua kama nina mimba au ni hali ya kawaida tu …
NAKUJA….Je nini KITAENDELEAAA!! "
ofaaa simulizi hi ipo mpk mwisho ni .