PENZI LA MAFIA NA DOCTOR DYNESS
????????????????????????
BY DIANA STORIES
Wtsp 0768328909
SEHEMU YA KWANZA(01)
Katika hospital kubwa ya kifahali inayojulikana kwa jina la Aghakhan, kulionekana msafara wa magari ukiwasili eneo lile na kushuka vijana waliovalia suti nyeusi uku wengine wakiingia ndani ya hospital kwa ajili ya kwenda kuita madokta waje kusaidia kumchukua mgonjwa wao.
Baada ya dakika kadhaa madokta baadhi waliwasili eneo lile na kwenda kumchukua mgonjwa aliyeletwa na ule msafara na moja kwa moja kumpeleka kwenye chumba cha matibabu.
Baada ya mgonjwa kufikishwa eneo husika, wale vijana walio valia suti nyeusi walikutana kwa pamoja na kuanza kupewa maelekezo na kiongozi wao.
"Wanahitajika vijana watano wabaki hapa kwa ajili ya kumlinda mkuu wetu na hakikisheni hakuna anayejua kama Mr.G ameletwa hapa hata madokta wenyewe hawaruhusuwi kujua hii siri Sawa? ",
"Sawa kiongozi"
Aliongea msaidizi wa Mr. G uku akitoa maelezo baadhi kwa wafanyakazi wenzake.
"Kitu kingine hakuna anayeruhusiwa kumtoa hiyo mask, alafu sisi wengine twende tukamsake huyo aliyempiga risasi mkuu wetu kabla hajaamka yule mwalifu awe ameshapatikana". " Ndiyo kiongozi tutafanya hivo",
Baada ya makubaliano kadhaa, baadhi ya wafanyakazi wa Mr. G waliondoka na kuwaacha baadhi ili wamlinde Mr. G pale hospital.
"Jamani mgonjwa wenu ana hali mbaya sana, na inahitajika afanyiwe operation ya haraka."
Aliongea daktari mmoja wapo uku akiwaangalia wale vijana waliokuwa wamemzunguka Mr. G.na kuanza kukiendesha kitanda alichokuwa amelazwa Mr. G kwa ajili ya kumpeleka kwenye chumba cha operation.
" Samahani hamruhusiwi kuingia, itakuwa vizuri kama mngebaki hapa nje mara moja" ,.
Aliongea nesi aliyekuwa anasaidiana na dokta kusukuma kile kitanda baada ya kufika kwenye chumba cha Operation lakini Cha ajabu wale wasimamizi wakawa wanaingia kilazima bila kujibu chochote.
Manesi na baadhi ya madokta waliokuwa eneo lile walijikuta wanaangaliana wasielewe cha
kufanya wakaona bora wanyamaze tu
.
"Hey mnahitajika kuokoa maisha yake haraka iwezekanavyo na siyo kuangaliana apo".
Aliongea mmoja wa wasimamizi wa Mr G uku akiwa serous.
Ikabidi madokta waingie nao hivo hivo, mana hali ya mgonjwa haikuwa nzuri kwa mda ule bora wamuwaishe kwanza.
Baada ya dakika kadhaa akaingia dokta wa kike, aliyevalia mvazi ya operation.
" Khee tangu lini kwenye chumba cha operation tukaanza kusimamiwa hivi?
"
Aliongea yule dokta anayejulikana kwa jina la dyness uku akichukua baadhi ya vifaa vyake kwa ajili ya kazi.
"Na nyie mnawaangalia tu,waone kwanza na miwani yao, hawa kama siyo majambazi hawa sijui,naona wanamlinda kubwa la maadui ili asije akawatoroka".
"Dokta Dyness aliongea uku akitaka kumtoa barakoa yule mgonjwa lakini gafla alishangaa amekamatwa mkono ",
"Samahani, binti fanya kazi yako iliyokuleta, usijitafutie matatizo",
Aliongea msimamizi wa Mr G aliyekuwa amemkamata mkono dokta Dyness.
"Doctor hawa watu inaonyesha siyo wazuri tufanye kazi tu,tuachane na yasiyokuwa ya lazima".
Aliongea dokta mwingine taratibu kwa sauti ya chini na moja kwa moja wakaanza kutoa risasi zilikuwa ndani ya mwili wa yule mgonjwa.
"mmhg!huyu kijana inaonyesha ni bonge moja la jambazi, yaani risasi karibia tatu zote zipo ndani ya mwili wake, na kwa nini analindwa kiasi hiki, lazima nitajua tu we subiri nitoke apa",
Doctor Dyness aliwaza kimoyomoyo uku akiendelea na operation yake.
Baada ya siku kadhaa hali ya Mr G ilianza kutengemaa ila alitakiwa aendelee kukaa hospital kwa ajili ya kutibia vidonda vyake.
Huku upande wa pili taarifa zilisambaa kwenye vyombo vya habari kuwa kijana anayejulikana kwa jina la Mr G ambaye ni kiongozi wa kundi la mafia ameuwa kwa kupigwa risasi tatu mfululizo na snepa mahiri aliyeagizwa na serikali kwa ajili ya kufatilia kijana huyo.
Na mda huo huo walionyesha na picha za kijana huyo akiwa amefariki kwa lengo la kuwaaminisha wananchi. "Maskini huyu kijana kumbe bado mdogo kiasi hiki?"
Aliongea mmama mmoja aliyekuwa amesimama barabarani uku akiangalia zile taarifa kwenye tv kubwa za barabarani.
"Huyu kijana wanamuandama kwa sababu anaharibu mipango ya viongozi wakubwa ila siyo kama alikuwa anafanya mauwaji ya watu wasiokuwa na hatia, najua kabisa hawezi kufa kirahisi kiasi hicho itakuwa kuna sehemu amejificha kwa mda",
Aliongea mmiliki wa hospitali ya Aghakhan mwenye asili ya kihindi anayejulikana kama doctor Kristen.
"Mkuu kuna taarifa zimesambaa mitandaoni kuwa umefariki".
Aliongea msimamizi wa Mr G uku akiwa ameshika laptop.
"Wao ooh!Ebu nipe kwanza nione comment za viongozi kuhusu kifo changu".
Aliongea Mr G uku akichukua laptop yake na kuanza kuangalia vinavyoendelea mitandaoni.
"Waooo!Sasa huu ndo mda mzuri wa kutimiza malengo yangu, tena na hivi hawanijui sura yangu na wanaamini kuwa nimeshakufa lazima nitapata ninachokitaka".
Mr G aliongea peke yake uku akiachia tabasamu kwa mbali,.
"Sasa kuanzia leo tufanye hivi, ebu sogeeni karibu kwanza Sitaki kutumia nguvu kwenye kuongea",
Aliongea Mr. G uku akiwaamuru vijana wake wamsogelee lakini kabla hajaongea chochote mda huo huo kuna doctor aliingia akiwa na vipimo mbalimbali.
"Hey!aliyekuruhusu kuingia umu ni nani? "
Mr G aliuliza kwa hasira na kufanya baadhi wa wasimamizi wakamzuie yule dokta asiendelee kuingia kwenye kile chumba.
"Samahani nimekuja kukufanyia vipimo nijue hali yako".
"Toka sihitaji mtu kwa Sasa, nyie mtoeni huyo haraka".
Mr G aliongea kwa hasira na kufanya vijana wake wamtoe nje yule dokta.
Ebu nipeni simu yangu kwanza,nisipokuwa makini hawa madokta wanaweza wakaharibu kila kitu.
Mr G aliongea uku akichukua simu yake na kupiga sehemu.
Uku upande wa pili doctor Kristen akiwa busy na kazi zake alishangaa simu yake inaita, ila kuna namna ilionyesha hiyo simu ni ya muhimu kidogo. Mana alianza kuangalia uku na uko ili kuhakikisha hakuna mtu atajayeweza kumsikia alafu akapokea.
"*Hallo Mr
" *Kumbe Upo kwenye hospital yangu!
"*Sawa kuhusu hilo nipe dakika kadhaa watakuwa wamefika apo alafu utaangalia atakayekufaa.
" *Usijali kuhusu hilo nitahakikisha usalama wako hadi pale utakapoondoka eneo hili.
Baada ya dokta Kristen kuongea na ile simu, alionyesha kupagawa na kuanza kupiga simu sehemu tofauti tofauti uku akitoa maelekezo kadhaa.
Baada ya mda kuna madokta watatu waliingia kwenye chumba cha Mr G,akiwemo dokta Dyness pamoja na madokta wawili wa kiume.
"Hey ina maana huoni kama tushafika au? "
Aliuza dokta Dyness uku akimwangalia Mr G aliyekuwa busy na laptop yake mda wote.
Mr G baada ya kusikia anaulizwa hivo ikabidi aache alichokuwa anakifanya na kumtazama doctor Dyness.
"We mwanamke jifunze kuwa na adabu siku nyingine, huoni wenzako wamenyamaza we ndo kama nani unanyanyua mdomo wako? "
Stanley aliongea kwa hasira uku akiendelea na kazi yake.
"Samahani, Kiukweli siwezi kupoteza mda wangu apa nikusubiri wewe et umalize kazi zako, nina wagonjwa wengi wananisubiri uko".
Baada ya dokta Dyness kuongea hivo, apoapo kuna msimamizi mmoja alimsogelea Mr G na kumnong'oneza kitu.
"Oooh Waooo!good job,sasa nyie wawili nendeni nataka nibaki na huyu mwanamke asiye na adabu ndo atakuwa dokta wangu kuanzia leo."
"Khee!ina maana hujaona wote umeniona mimi, unajielewa kweli wewe? "
"Doctor Dyness unaongeaje na mgonjwa hivo? "
Doctor Dyness alivosikia hivo ikabidi ageuke ili amuone anayemuuliza, alijikuta anashtuka baada ya kumuona doctor Kristen mmiliki wa ile hospital, kwa mara ya kwanza anamuona mkuu wake kaja kwenye chumba cha mgonjwa.
"Samahani mkuu!huyu kaka inaonyesha ana matatizo ya akili kidogo ndo mana nikawa najaribu ku..ku.."
"Et nini!, ebu rudia tena ? "
Mr G aliuliza kwa hasira na kumfanya doctor Kristen aingilie kati.
Je nini kitaendelea! Doctor Dyness atakubali kuwa dokta special wa mr
G
Karibu full ni 1000 leo ni ofa ya ckukuu whtsp 0768328909.