Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  artist

Unawezaje Kumiliki Soko Lolote? Kwa mujibu wa Mukesh Ambani, tajiri mkubwa zaidi barani Asia

1st Jun, 2025 Views 27

Unawezaje Kumiliki Soko Lolote?

Kwa mujibu wa Mukesh Ambani, tajiri mkubwa zaidi barani Asia, unatoa zawadi yenye thamani ya dola bilioni 25.

Washindani wake walimcheka... hadi alipoyafilisi makampuni 11, akaunda kampuni yenye thamani ya dola bilioni 100, na kuyumbisha uchumi wa India.

Hii ni moja ya stori za unyakuzi wa kikatili zaidi katika historia ya biashara:

Mwaka 2016, sekta ya mawasiliano nchini India ilikuwa inatawaliwa na Airtel, Vodafone, na Idea, kwa kushikilia asilimia 70 ya soko.

Bei ya data ilikuwa kati ya dola 3 hadi 5 kwa GB, moja ya gharama za juu zaidi duniani.

Mamilioni ya Waasia hawakuweza kumudu huduma ya intaneti. Lakini kila kitu kilikuwa karibu kubadilika...

Mukesh Ambani, aliyekuwa na utajiri wa dola bilioni 92 na mkuu wa Reliance Industries—kampuni inayodhibiti asilimia 10 ya Pato la Taifa la India—aliingia kwenye ulingo.

Alikuwa tayari ameshashinda katika sekta ya mafuta, biashara ya rejareja, na petrochemical.

Mawasiliano yangekuwa ushindi wake wa kipekee zaidi. Na mpango wake ulikuwa tayari unaendelea.

Ambani kwa kimya alijenga Jio, mtandao wa kwanza wa 4G pekee nchini India, akiwekeza dola bilioni 25.

Wakati washindani wake bado walihangaika na 3G, Jio tayari ilikuwa imefika katika miji 18,000 na vijiji 200,000.

Lakini kuwa na miundombinu bora hakutoshi—alihitaji watu wengi kuitumia.

Ndipo alipofanya hatua ya kushangaza...

Mkakati wake wa kipekee:

Huduma zote za Jio BURE kwa miezi 6:

• Kupiga Simu bure
• Ujumbe mfupi wa maandishi bure
• Data ya bure ya 4G isiyo na kikomo

"Anajitoa ufahamu kifedha," washindani walidharau. Hawakuwa na wazo la kile kilichokuwa kinakuja.

Matokeo yalikuwa ya kushangaza:

• Watumiaji milioni 16 mwezi wa kwanza
• Milioni 50 ndani ya miezi mitatu
• Zaidi ya milioni 100 ndani ya miezi sita

Hii haikuwa upatikanaji wa wateja— bali ulikuwa uvamizi wa soko. Na washindani walibaki wakitazama kwa hofu.

Ambani hakuwa tu anatoa huduma—alikuwa anabadilisha tabia.

Mamilioni ya watu ambao hawakuwa wamewahi kutumia data kabla walianza kutazama video na kupiga simu za video.

Baada ya kuonja faida, hawakuweza kurudi nyuma. Na hapo ndipo alikua akitegemea.

Makampuni ya mawasiliano yakaanza kupaniki, yakapunguza bei zao kwa asilimia 80.

Lakini tayari ilikuwa wamechelewa. Ambani alikuwa tayari ameyapunguzia makampuni hayo thamani ya dola bilioni 25.

Watoa huduma wadogo wakaanza kufa.

Mauaji yalikuwa yameanza...

Baada ya miezi sita, Jio ilianza kutoza—lakini kwa gharama ya $0.15 kwa GB, ndogo kwa asilimia 95 ya bei iliyokuwepo awali.

Hata kwa bei ya chini kabisa, Jio ilikuwa inatengeneza faida kutokana na miundombinu bora.

Washindani walinaswa kwenye mchezo ambao wasingeweza kushinda.

Matokeo ya kikatili:

• Vodafone na Idea walilazimika kuungana
• Airtel ilipata hasara yake ya kwanza katika miaka 15
• Watoa huduma 11 walipungua hadi kubakia 4
• Ajira 150,000 za sekta ya mawasiliano zilipotea

Si tu kuyumbisha sekta. Ni kuiangamiza kabisa. Lakini kwa watumiaji wa kawaida? Hadithi ilikuwa tofauti.

Kwa watu wa India, kulikuwa na mapinduzi:

• Matumizi ya data yaliruka na kuongezeka mara 50 hadi 10GB kwa mwezi
• Upatikanaji wa intaneti uliongezeka kutoka asilimia 27 hadi 47
• India ikawa na gharama ya data ya bei rahisi zaidi duniani

Lakini mpango mkuu wa Ambani ulikuwa bado haujakamilika...

Ujanja wa Ambani haukuwa tu kushika sehemu ya soko—bali kujenga mfumo mzima wa kidijitali.

Akiwa na zaidi ya watumiaji milioni 400, Jio ilitanuka hadi:

• Biashara ya mtandaoni (E-commerce)
• Intaneti ya nyumbani (Broadband)
• Huduma za kifedha (Fintech)
• Mikutano ya video (Video conferencing)

Zawadi ya "dola bilioni 25" ilikuwa tu mwanzo wa mchezo mkubwa zaidi.

Kamari ya dola bilioni 25 iliunda kampuni ya mawasiliano ya dola bilioni 70.

Mwaka 2020, makampuni ya teknolojia yaliwekeza:

• Google: dola bilioni 4.5
• Facebook: dola bilioni 5.7
• Intel na Qualcomm nao walifuata

Kilichowahi kuonekana kama wendawazimu kwa washindani, kiligeuka kuwa dili la karne.

Leo, Jio ina thamani ya zaidi ya dola bilioni 100 na inashikilia asilimia 40 ya soko.

Kile kilichoonekana kama "kujitakia maangamizi ya kifedha" kiligeuka kuwa mojawapo ya unyakuzi bora zaidi wa soko katika historia.

Uchumi wa kidijitali wa India ulilipuka hadi dola bilioni 200.

Mamilioni ya biashara ziliingia mtandaoni, na malipo ya kidijitali yakapaa hadi miamala bilioni 8.3 kwa mwezi.

Ambani aliona kile ambacho wengine walikikosa:

Katika zama hizi za kidijitali, mawasiliano si huduma tu—ni msingi wa kila kitu.

Kwa kuifanya huduma hii kuwa karibu bure, aliweka kampuni yake katikati ya mustakabali wa kidijitali wa India.

Asante kwa kusoma na kushea ????????????????????????.
   

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

side chick episode 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

SIDE CHICK EPisode 2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NIPE YOTE DADY???15

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 18

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 17

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 16

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 8

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

RATIFA Sehemu ya 32

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NAWASHWAA? Sehemu 13.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NIPE YOTE DADY ???11

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

BOYCHILD PART 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 4.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 29

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

LOVE Part 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 28

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NAWASHWAA Sehemu nne.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 26

mrindia rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 25

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest