WATOTO MAPACHA
Sehemu ,,,,, 3
Mama celena AKATOA MACHO,,
Akataka kumfuatilia lakin celina akawa amepotelea vichochoroni ,
"" Unamfahamu ,,""
Mama celena alimuuliza mwanae,
""Hapana ndo kwanza nimemuona leo ,,""
Celena alijibu .
""Yule atakuwa ni jini ,na ukiona kitu cha ajabu kama kile usipende kukifuata sawa mwanangu ""?
Mama celena alimwambia mwanae huku akimshika mkono na kuondoka eneo hilo .
Pamoja na kudanganywa na mama yake kuwa yule hakuwa mtu bali nijini amejigeuza na kufanana nayeye lakini celena hakuamini ,aliendelea kuwaza tu ,
Mama celena yeye aliamini yule mtoto aliefanana na mwanae ni jini ,
Celina alivyoachana na celena nae alipofika kule kwenye jumba bovu ambalo ndiko wanakaa yeye na mama yake ,alimkuta mama yake yuko hoi yaan anaumwa si kawaida ,
Celina alijitahid kumwinua na kumshika mkono na kumpeleka hospital ,alipofika hospitali kila mtu aliwakimbia walionekana kama vichaa yaan kichaa mdogo na kichaa mkubwa wamekuingia hospital,
""Samahani nesi mama yangu anaumwa sana tafadhali naomba dawa ""
Celina alimwambia kwa huruma nesi mmoja aliepita karibu yake ,
""Wee hebu niachie mi nnakaz za kufanya kwanza unanichafua ,""
Yule nes alimjibu kwa nyodo na kuondoka zake.
Akamkimbilia nes mwingine na kumwambia shida yake ,lakini pia yule nesi alimjibu kuwa hawezi kutibu vichaa,
Celina aliumia sana na kwa utoto wake aliokuwa nao akaanza kulia ,na hakuna hata mtu aliem bembeleza ,
Wakat analia akapata wazo la kwenda kwa docta mkuu ,akatoka mbio nakuwapita watu waliojipanga foleni kwa ajili ya kumuona docta na akaingia ndani kwa docta,
"" Shikamoo ,,docta mama yangu ni mgonjwa na akifa inabidi na mimi nife kwa sababu yeye ananipenda na mimi nampenda mama yangu,,,"""
Celina aliongea kwa uchungu na akaanza kulia ,
Gafra akaingia nesi
""Samahani docta tulimzuia asiingie ila amefosi tu kuingia toka nnje we mtoto ,,""
Yule nesi aliongea kwa hasira .
""Hebu twende unipeleke kwa Mama yake na huyu mtoto ,,""
Yule docta alimwambia yule nesi ,
""Docta huyo mtoto ni kichaa pamoja na mama yake ""
"""Nimesema twende unipeleke alipo.""
Docta alimgombeza yule nesi ,na yule nes hakuwa na namna tena ikabidi ampeleke akamuoneshe ,
""Huyu hapa si nilikwambia docta huyu mama ni kichaa ,,""
Nes alimuonesha docta,
""Eti mtoto mbona mama yako ni kichaa ,,""
Docta alimgeukia celina.
"Ndio ni kichaa lakini anaumwa ,angekuwa haumwi angeshaenda majalalani kunitafutia chakula ,""
Celina alijibu huku analia kilio cha kwikwi,
"Huyu ndio mama yako mzazi ,,""?
Docta alimuuliza tena celina ,
" "Ndio na Sina mwingine kwenye hii Dunia nnaempenda kama yeye,,,""
Celina alijibu mpaka docta chozi likamlenga lenga,
Celina alitia huruma sana ,na docta akaamuru yule Mama apimwe ili apewe dawa , kweli manes walimpima kama ushahidi tu na wakampa dawa , Celina akaondoka na mama yake ,
Lakini pamoja na hayo yote yule docta alipanga kumsaidia mtoto celina ,
Alimwita ofisini kwake na kumwambia atampeleka shule asome ili baadae aje amsaidie mama yake ,
Celina alikubali lakini akamwambia docta hata akirudi shule ataenda kulala na mama yake ,hawezi kumwacha mama yake peke yake ,
Docta alikubaliana na mtoto celina ,
Mama yake alipopona yule docta akamwandikisha celina shule na celina akaanza masomo,
Japo yule docta alimwandika celina jina la kwake yaani celina Mathias,lakini shule watoto wote walimjua kuwa ni mtoto wa kichaa ,
Celina alikuwa na akili sana na hapo shuleni walimu wengi walijua docta Mathias mwanae ni celina ,
Kutokana na akili zake celina akarushwa darasa ,
Akawa anasoma darasa la 3 ,
Ndani ya darasa la 3 kulikuwa na kijana mmoja wanamuita Stefano ,
Stefano alikuwa mtundu halafu mchokozi balaa ,
Lakini pamoja na utundu alionao stefano alikuwa akiambiwa na Celina
""Stefano tulia ,""!
Stefano anatulia kama sio yeye ,hata stefano mwenyewe alijishangaa, na watoto wenzake walimcheka maana Celina alikuwa haongei mala mbili , na hata muda wa kutoka Stefano alikuwa na kawaida ya kucheza njiani lakini akimuona Celina haraka na upesi anaongoza njia ya nyumban ,
Stefano ni mtoto wa yule mama aliezaa watoto Mapacha miaka7 iliyopita, na manesi wakamwambia mapacha wake wamefariki ,kumbe walimuuza pacha mmoja na pacha mwingine wakamtupa dampo wakizan atakufa, na kwa mipango ya Mungu akaokotwa na yule mama chizi,
mama yule anaitwa Rebecca ,
kaa mkao wa kusoma story tamu na yenye msisimko kumbuka story hii utaipata yote mwanzo mwisho kwa elf moja tu ,0655772653 njoo whtsap,
Itaendelea.