DO YOU LOVE ME 09 (S2)
ALWAYS MEN ARE CHEATER
Tulielekeaa chumban kwa ajili ya kupumzika lakin ukweli sikuwa sawa hata kidogo. Kitu ambacho nilikua nawaza akilini ni kumtafuta Rola tu niongee nae tu maana yeye ndio alikua mwanamke pekee ninaempenda kwa dhati japo kuna mda alikengeuka lakin nilijiambia kwamba huwenda zile zilikua ni hasira tu. Niliwaza piaa siku ambayo Rely ataondoka mazima kwenye maisha yangu itakuaje?? Maana pamoja na kwamba nampendaa sana ndugu yake lakin ahta yeye pia nilikuwa nimemzoea, nilijikuta naumia sana na kubaki njia panda huku swala la ujauzito wa Rely pia likizidi kunipa 'headache' kwasababu sikua na uhakika kama ujauzito ni wangu au lah..! Niliwaza sana na kuwazua mda huu Rely alikua tayari ameshazama kwenye usingizi mzito huku mimi nikiendelea kujigeuza kama chapati tu pale kitandan.
Kulikucha asubuhi na wa kwanza kuamka nilikua Mimi maana nilikua naisubiri sana hii siku ifike, niliandaa chai mim mwenyewe kisha tukanywa na baada ya hapo tulijiandaa kwenda hospital kupima afya ya Rely..
Tulifika daktari akachukua vipimo na majibu yalitoka kwamba Rely ana ujauzito wa miezi mitatu. Nilifurahi kwa kiasi chake japo sikua najua kama furaha yangu ingedumu kwasababu sijui mtoto ni wa nani?? Pamoja na kwamba nilikua najua Rely ananicheat ila sikuwahi hata siku moja kumwambia na yeye alijua sijui kwamba ana mwanaume kumbe naujua mkanda mzima sema nilichokua nakifanya ni kujiandaa tu kisaikolojiaa.
Tulirudi nyumban tukiwa na furaha sana, nilimuandalia chakula kisha nikamuaga kwamba naelekea kwa mama kumuona maana alinipigia simu. Nilielekea kwa Mama na nilimkuta akiwa jikoni kuandaa chakula..
"Mmh nimefikia pazuri maana naskia tu harufu nzuri nzuri huko jikon.."
"Upewe hayo kula tu, za huko utokako kwanza??" Aliniuliza mama yangu huku akikaa kwenye sofa.
"Za huko salama tuu za hapa..?"
" Za hapa kama unavyoziona ni nzuri nakula tu kiyoyozi.." Alinijibu hvyo mama yangu huku akiwa anapitisha macho kweny sebule yake ambayo naweza sema ni nguvu za wazazi wa Rely.
"Naona maisha ni safi"
"Eeeh, huyo mkeo hajambo?"
"Hajambo lakin hivi karibuni naenda kuitwa baba.."
"Kheee jaman.!!! Bora maana naona siku zinaenda tuu na sion dalili za kuitwa bibi, bora azae maana nilitaka kujua labda Mgumba maana sio kwa kukawia huko..!!"
"Mama maneno gani hayo?? Hujui kama kuzaa ni mpango wa Mungu..??" Nilimuulza kwa hasira maana niliona anataka kwenda mbali zaidi.
" Eeeh nisiseme sas..??"
"Hata hivo sikuja kwa ajili ya hilo apa..!!"
"Umejia nin sasa?"
"Nimekuja tu kukupa taarifa kwamba lolote linaweza kutokea kati yangu mim na Rely..!"
"Unamaanisha nin?? Mnataka kufa au?"
"Sio kufa mama, we elewa hivyo tu"
"Mtajua wenyewe bana, sasa mambo yenu mie yananihusu nin..?? Mtajuana huko, Em wacha kwanza nikuletee chakula ule ushibe uende kwa mkeo.." alijibu Mama huku akisimama kuelekea jikon.
Siku moja Rola alikua kazini kwake akiendelea kufanya kazi ndipo sim yake ikaita lakin namba haikua na jina hivyo akapokea na ilisikika sauti ya kike..
"Haloo.."
"Haloo, habari yako??"
"Salama"
"Unaongea na Rola, nan mwenzangu??"
"Sikia wewe mwanamke, najua unaitwa Rola ila nina jambo langu moja tu ambalo ndio limenifanya nikupigie sim sahivi" Aliongea yule mwanamke ambaye ongea yake tu ilionesha dhahiri kwamba alikua amevurugwa.
"Taratibu basi, sas unavyoongea hivyo kwa shari mi nikuelewe vip??"
"Utajua wew sas kama naongea kwa shari au kwa kheri lakin swala lililopo ni wewe kuachana na mume wangu la sivyo nitakutenganisha na huu ulimwengu!!"
"Kheee wew em samahan kwanza, we unamuongelea mumeo nani maana mi sina mahusiano na mume wa mtu.."
"We ndio unavojua hivyo, lakin achana na Hussein lasivyo tutaonana wabaya...!!" Alimaliza kuongea na kukata sim kabisa.
Rola alihisi kuchanganyikiwa maana hakua anajua kama Hussein ana mwanamke mwingine tofaut na yeye na hizi habari ndo kwanza anazisikia.
Alijikuta anachoka hata nguvu ya kufanya kazi tena ikaisha na kuamua tu kufunga safari ya kurudi nyumban kupumzika.
Majira ya usku wakiwa wanakula Rola pamoja na Hussein, Rola aliona amuulize Hussein juu ya kile alichoambiwa wakati yupo kazin.
"Hussein una mwanamke mwingine tofaut na mim??" Aliuliza swali ambalo lilimfanya Hussein kupaliwa na chakula.
"Uko sawa??" Aliuliza tena Rola baada ya kuona kwamba swali lake limemshtua Hussein na kumfanya apaliwe.
"Nipo sawa.."
"Okay, nijbu swali nililokuuliza, una mwanamke mwingine tofauti na mimi???" Aliuliza Rola na safari hii aliweka mkazo kabsa ila kumaanisha kwamba alikua serious na kile kitu na alidhamiria kujua ukweli kutoka kwa Hussein. ITAENDELEAA
.