DO YOU LOVE ME 13
ZHIGZAG
Tulikaa pale kwa mda kidogo, kuna wakati nilitoka nje nkampisha Thelesia ampe chakula Rola na badae nilirudi wodini kutaka kujua hali ya Rola.
"Unajiskiaje?" Nilimuuliza.
"Kichwa kinaniuma sana, nahisi kuchoka kwa kweli."
"Pole utakua sawa."
"Rely umemuacha vipi? Na amejua kwamba umekuja huku? kwasababu sidhani kama akijua kama umekuja huku atafurahi."
"Usijali Rola kila kitu kipo sawa. Hata hivyo nilikua tu na wasi wasi, nilitaka kujua hali yako na kwakuwa umeshakua sawa sina budi kuwaacha." Nilijibu huku nikisimama kwenye kiti nilichokua nimekaaa.
"Mbona mapema sana Rahim?" Aliuliza Thelesia.
"Nashkuru sana kwa moyo wako na Mungu akubariki Rahim." Alisema Rola huku akijaribu kuachia tabasam uson kwake.
"Aaah usijali Rola, sisi ni binadam lazima upendo uendelee kuwepo"
"Asantee"
"Basi sawa, mi wacheni nitoke, kwaherini na mbaki salama."
Niliaga na wote wakashukuru kwa uwepo kwangu kisha sikua na namna tena kuendeleaa kubaki pale nikaondoka kutafuta njia ya kurudi dar.
Kufika nyumban kwangu sikumkuta Rely nikajua kaenda kazin kwake. Nilienda mpaka chumbani hata vitu vyake vilikuwepo.
"Ana mbwembwe sana huyu mwanamke, inamaana jana alivyokua anataka kuondoka alikua anabip fire au?" Nilijisemesha mwenyewe huku nikiwa najitupa kitandani.
Kwa wakati huu tayari ilikua imeshatim saa kumi na mbili jion, sikuona sababu ya kutoka na kwenda kwenye kibanda changu cha chips na badala yake nikaamua kuingia jikoni na kuandaa chakula cha usiku.
Siku zilipita, hatimaye miezi miwili ilikatika bila mawasiliano na Rola, sikuwa najua wanaendelea vipi yeye na familia yake kwasababu kila nilipokua nikipiga sim yake haikupokelewa na mda mwingine haikupatikana kabisa. Niliamua kupotezea lakini sio kupotezea upendo wangu kwake. Nilimpenda Rola kupita maelezo na wala sikuchoka kumpenda hata siku moja. Kipindi hiki ata ujauzito wa Rely ulikua umekua tayari lakin visa na mikasa havikuisha ndani ya nyumba yetu. Kila siku ilikua kelele na maneno yasiyokuwa na mpangilio, kwa kifupi tulikua kama paka na panya.
Siku moja niliamua kutoka na kwenda kwa mama na kwa bahati nzuri nilimkuta japo alikua anajiandaa kutoka lakin nashkuru nilim'wahi.
"Mama una safari?" Niliuliza.
"Makubwa! Ndio nini kunijia bila taarifa mapema yote hii, kwema huko?" Aliuliza mama akiwa anashangaa ujio wangu wa bila taarifa pale nyumban.
"Sasa Mama hapa si nyumbani? Kwani kuja mpaka nitoe taarifa?"
"Mtoto shika adabu yako tafadhali. Kwako hapa? Kwako si huko kwa huyo kichaa mwenzio?"
"Lakin mama sijajia hayo, shikamoo kwanza."
"Marahaba, na useme haraka bwana nina safari zangu saa hizi"
"Sawa, mama hapa nimejia swala moja tu mama yangu. Naomba uongee na Rely mama maana pale nyumban sahivi hapakaliki. Ukipita huku ni kelele ukirudi huku kelele yaani ile mimba inampelekesha sjui?"
"Kwahiyo unataka mimi niongee nae nin kama mwenyewe ushasema mimba inampelekesha?"
"Aaah mama yule ni mwanamke mwenzio!"
"Kwahiyo?"
"Ongea nae labda atakuelewa!"
"Bwana kama hakuna habari zingine fanya safari, nimekwambia nina safari zangu. Huyo mkeo hawezi kubadilika hata nikiongea nae nini. Kama unabisha subiri akijifungua halafu akibadilika urudi hapa unidai hii nyumba yote nikupe." Alisema mama kana kwamba anajua kila kitu kuhusu Rely.
"Mama!!" Nilimuita mama kwa mshangao sana maana kauli yake ilinipa utata.
"Hiyo ndio habari iliyopo. Haya fanya kuondoka nifunge mlango wangu mie."
Sikuwa na namna zaidi ya kuondoka na kurudi kuendeleaa na majukumu yangu huku nikiwa ni mwenye mawazo sana. Ukweli ni kwamba ata ule mwili niliokua nao mwanzo kipindi hiki ulipungua kabisa kwa mawazo. Nilikua najua Rely ananicheat lakin sikutaka kumwambiaa, na yeye alijua mimi sijui kwasababu sikuwahi kumwambiaa. Nilifanya hivi nikisubiri tu mtoto azaliwe tupime DNA halafu mtoto akiwa sio wangu basi baba yake atamchukua yeye pamoja na mama yake. Yaan kwa kipind hiki tulikua tunaishi kusukuma siku maana nilichokua nafanya ni kulea tu ule ujauzito ambao sikuwa na uhakika nao ata kidogo.
Upande wa Rola nilisimuliwa hivi; Nyumban kwa Rola siku hii alikua anaongea na Hussein lakin maongezi yao hayakua ya kawaidaa kwasababu walikua wanazozana sana.
"Nimeshakwambia sikutaki naomba uende kwa mkeo, sihitaji matatizo na mtu! Nilikuamini sana kiasi kwamba sikutaka kumsikiliza mtu yeyote lakin kumbe lengo lako ni mimi kufa si ndio??" Ilikua sauti ya Rola aliekua anamfokea Hussein.
"Lakin nakupenda wewe Rola!"
"Muongo mkubwa, unanipenda au unataka pesa zangu, najuta sana kukuamini. Najutaaa!!!"
"Haya maongezi tulitakiwa kuongea taratibu tuweze kuelewana kwanini unakuwa mkali?"
"Achana na mimi Hussein, we ni mwanaume gani? Mwanaume usiekua na utu ata kidogo. Siku ile apa ulitaka kuniua, yan asingekua Thelesia si ningekua marehem mimi au? Yan ukaona haitoshi kunisukuma, badala yake ukaniacha kabsa alafu unasema unanipendaa, unanipenda au unacheza na akili angu?"
"Tatizo unasikilza maneno ya watu mke wangu naomba basi nisikilize."
"Maneno ya watu, maneno gani? Niskilze Hussein naomba uondoke kwangu haraka sana!"
Rola aliongea na kuondoka chumbani akamuacha Hussein peke ake.
Baada ya Rola kutoka, Hussein kuna kitu kama aliwaza na baadae akatingisha kichwa kutoka juu kwenda chini na kutoka chini kwenda juu ishara ya kwamba alichokiwaza alikubaliana nacho. Mda huo huo alifungua droo iliyokua kwenye kabati ya Rola na kutoa bahasha moja kisha akaifungua na kutoa karatasi moja akaisoma kisha akaachia tabasam. Baada ya kuwa amesoma ile karatasi, aliirudisha kwenye bahasha kisha akafunga droo na kutoka na ile bahasha na kwenda kuificha kwenye nguo zake kisha alitoka na kuondoka zake akamuacha Rola aliyekua hafahamu kitu chochote kilichotokea huko chumban kwake baada ya yeye kutoka. ITAENDELEA
.