DO YOU LOVE ME 08
WHO IS FATHER OF THE PREGNANT?
Nilirudia kama mara mbili kuisoma ile meseji ambayo ilinifanya kubaki nimeganda kama sanamu pale ndani lakini sauti ya Rely iliyokua inatokea nje ilinishtua na kunifanya niirudishe ile simu pale kisha nikamsikilize alichokua anakisema.
"Mume wangu, mda ndio huu sasa mbona unachelewaa kuondoka?? Inamaana mda wote huo ulikua unavaa..??
"Aaah.. yeaah, nilikua natafuta hii kadi ya benki.." Nilidanganya maana hakuna nilichokua natafuta zaidi ya kwamba nilikua nasoma ile meseji ambayo ilinifanya kuwa kama nimejitwishwa chungu cha moto kichwani.
"Aaah basi sawa amna shida, kazi njema.." Alinitakia kazi njema huku akiachia bonge la tabasam na kunikiss shavuni. Niliondoka Mim mtoto wa Mama Rahim na kuingia mtaani sasa kuendeleaa na kazi ambayo nilipanga kuifanya siku ile.
Baada ya mimi kuondoka Rely alimaliza kazi zake na kuingia chumban na kukutana na ile mesej kutoka kwa huyo ambae inaonekana ni mpenz wake.
"Oooh Calvin amenitafta..??" Aliongea huku akijarb kuipiga ile namba ambayo ilikua haijaseviwa kweny simu yake.
"Halloo.." Ni sauti ya upande wa pili iliitikia, sauti hii ilikua nzito kiasi na ilionesha ni sauti ya mwanaume haswa..!! Nikisema sauti ya mwanaume haswa sijui kama mtakuwa mnanielewa lakin tufanye mnanielewa.
"Yees, mambo.."
"Safi nimepiga sana simu haipokelewi, ulikuwa wapi??"
"Ooh sorry nilikua kazi nyingi leo si unajua nipo off kwahiyo nikaona nifanye kazi za hapa nyumban kwanza.."
"Sawa, sasa nahitaji kuongea na wewe leo mpenzi, kwanza nimekumiss si unajua lakin??"
"Naelewa, kwahiyo tutakutana mda gani sasa maana huyu mwanaume sitaki ajue kitu chochote kuhusu mim na wewe.."
"Usijal ni hata mda huu tu kama utakua free ni sawa, lakin mwisho wa siku lazima huyo mumeo akubaliane na ukweli.."
"Kwamba..."
"Njoo tuonane kwanza maana kesho nina safari ya kwenda Kenya hivyo sihitaji kuondoka bila kukuona."
"Sawa nakuja baby.."
Rely alijiandaa kwa ajili ya kwenda kuonana na huyo mpenzi wake ambae anafahamika kwa jina la Calvin. Ilikuaje mpka wakajuana??
Turudi nyuma kidogo..
Siku ambayo Rely ameenda kutafuta kazi alikutana na huyu Mwanaume maeneo ya maegesho ya magari nje ya hiyo restaurant ambayo ndio anapofanyia kazi sasa hivi na huyu mwanaume alijitambulisha kama Calvin..
"Hii dada samahan.." Calvin alimuita Rely huku akiwa anafung mlango wa gari lake, inamaana Calvin alimuona Rely wakati yupo kweny gari bado. Baada ya Rely kuitwa alisimama na kumsikilza Calvin..
"Aaah samahan, habari yako??"
"Salama.." alijibu kifupi huku akimuangalia yule mwanaume jinsi alivyokua ameyapangilia mavazi yake vizuri huku akinukiaa marashi ambayo hayakumfanya Rely kuchoka kuvuta hewa ya eneo lile.
"Naitwa Calvin, sijui unaitwa nan mwenzang??"
"Naitwa Rely.."
"Oooh karibu, umekuja kupata chakula eneo hili??"
"Hapana nimekuja kutafta kazi..!"
"Ooh imekua vizuri basi maana mim ndio mkurugenzi eneo hili, kwahiyo karibu ofsin kwangu" Alijibu na kuanza kutangulia huku akimuacha Rely nyuma akiwaza na kushukuru Mungu kwasababu ilikua kama bahati kwake kukutana na boss tena boss kamsimamisha mwenyewe.
Waliingia mpaki ofsin kisha Rely akaeleza shida yake na kwakuwa yule mwanaume alikua tayari ameshavutiwa na Rely basi hapakua na shida tena zaidi ya kumpa kazi Rely na hapo ndipo ukawa mwanzo wa mapenzi yao.
Rely alitoka nyumban na kuelekea huko anapofanyia kazi ili kuonana na Calvin. Alifika kule kisha waliongea mambo mengi ikiwemo namna ambayo Rely anajiandaa kuondoka kwangu, waliongea sana na mwisho wa maongezi yule mwanaume alimpatia Rely pesa ambazo zingetumika kuanzisha duka. Baada ya hapo waliagana huku wakipeana ahadi nyingi nyingi kama ilivyokuwa kawaida kwa wapenzi wengine.
Majira ya usiku tukiwa tunakula, kimya kilitawala eneo lile lakini nikaamua kuuvunja ule ukimya kwa kuanzisha story za biashara..
"Mke wangu umefikia wapi kwenye swala la kufungua duka maana nimeenda kwenye site ambayo nitafungua kibanda changu cha chips, nmeongea na mhusika na kila kitu nmeweka sawa na pesa imebaki kama milion 5."
"Aaah sas milion tano itatosha kweli?? Maana hatujalipia frame bado na vitu vingine pia.."
"Basi tusubir huu mwezi uishe alafu unaofatiaa tuongezee pesa" Niliongea vile maksudi kwasababu najua atanipinga sema niliongea tu ili nisikie atasemaje..?
"Aah mwezi ni mrefu sana, mi nitaongezea pesa.. nitamkopa rafiki yangu mmoja hivi tupo nae kazin maana yeye hela zake hazina mambo mengi sana!" Alinijibu hivyo lakin mim nilikua tayari nimeshajua hapa hakuna cha rafiki yake wala nin ila ni yule mwanaume wake ambae alimtumia mesej mda ule.
"Aaah sawa kama umeamua hivyo! Hivi ulishawahi kuongea na Rola hizi sku za hapa karibuni..?" Nilichomeka swali ambalo nilikua najua jibu lake ni hapana.
"Mmmmh hapana, sijaongea nae wala sijui anaishi vipi?? Yeye si akitufukuza sas naongea nae wa nin??"
"Lakin ni ndugu yako labda wewe ndo ungeanza kum..." Sikumalzia sentensi yangu, Rely alikimbia kweny sink na kuanza kutapika. Nilimfata pale ili kutaka kujua hali yake kama ipo sawa.
"Nin shida mke wangu??"
"Nahisi kichefu chefu sana alafu piaa kizungu zungu hakiishi.."
"Pole itabdi kesho twende hospital sasa tukajue shida ni nin??" Nilimwambia hivyo huku moyon nikiwa najua kabisa itakua ni ujauzito, sas swali ni je huo ujauzito ni wangu au wa huyo hawala yake..?? ITAENDELEA
.