Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  artist

DO YOU LOVE ME 14 (S2)

15th Jun, 2025 Views 38

DO YOU LOVE ME 14 (S2)

LAWYER'S GAME
Baada ya Hussein kutoka alielekea kwenye gari yake akaingia na kuchukua sim yake kisha akachezea kidogo na kuweka sikioni baada ya sekunde chache ilipokelewa na mazungumzo yakaendelea.

"Upo wapi?"

"Nipo ofisini kwangu, kuna shida?" Sauti upande wa pili ilisikika.

"Nakuja sasa hivi." Aliongea Hussein na kukata sim kisha aliwasha gari na kuondoka.

Huku ndani walibaki Rola na Thelesia ambao ni kwamba kila mmoja alikua na mambo yake. Rola alikua bize na simu yake huku Thelesia akiwa bize kuandaa chakula. Dakika moja ilimtosha Thelesia kutoka kule jikoni na kumfata Rola pale seblen.

"Mmh dada upo sawa?" Aliuliza Thelesia.

"Ndio, kwanin?"

"Nilisikia kelele huko chumban kwenu nikahisi labda kuna shida."

"Aaah ni huyo mpuuzi Hussein, yan ananikera kila siku sijui ananitaka nini?" Aliongea Rola huku akionesha hasira zake wazi wazi.

"Samahani dada kama ntakua naingilia mipango yako, lakin huyu Hussein sio mtu mzuri. Nahisi yupo kwako kwa maslahi binafsi."

"Thelesia tumeanza kuingiliana au?"

"Hapana dada nimeongea tu kwa nia nzuri na sio kwa ubaya."

"Sawa nimekusikia unaweza kwenda kuendeleaa na kazi zako."

Rola hakutaka mjadala na Thelesia maana aliona kama anamuingilia kwenye mambo yake. Lakin akiwa pale aliwaza na kuona mawazo ya Thelesia kwa namna moja au nyingine yanaweza kuwa sahihi kwasababu Hussein amebadilika kabisa na kubwa zaidi ana mwanamke mwingine ambae ata Rola mwenyewe anajua hilo.

"Huyu Hussein sijui nimfanye nini? Kumpenda nampenda lakini naona atanipanda kichwani! Nifanye nini sasa ikiwa ata baadhi ya mali zangu nimeandika jina lake, si anaweza kunigeuka??"
Hili ni wazo ambalo lilipita kichwani kwa Rola na alijaribu kufikiria kwa kina akaona kuna jambo linaweza kutokea. Alichokifanya ni kwenda chumbani kwake na moja kwa moja alielekea kwenye ile droo ambayo mara ya kwanza Hussein aliifungua na kutoa bahasha ambayo aliificha kwenye nguo zake.

_____

"Rely hii tabia utaacha lini lakini? Mbona umebadilika sana, yan sasa hivi huoni ajabu kunivunjia heshima." Ilikua ni sauti yangu ambayo siku hii nilikaa na Rely kuzungumza nae baadhi ya mambo ikibidi tuwekane sawa tuishi kwa amani lakini mwenzangu hakua tayari kwa hilo.

"Unataka kusema nini Rahim?" Aliniuliza.

"Namaanisha haya maisha siyafurahii ata kidogo, umekua mtu wa dharau sana au kwasababu huo ujauzito ni wa kwanza?"

"Sijui unazungumzia nini, kwani we shida yako ni nini haswa?"

"Nataka tuishi kwa amani kama zamani."

"Uishi na mimi kwa amani kivipi wakati fika najua hunipendi unampenda Rola?"

"Sijaongelea habari za Rola hapa, nahitaji amani tuliyokua nayo iweze kurejea tena."

"Bwana wee, nasikia kiu niletee Pepsi ya baridi kwanza alafu ndo tuendelee na hizo habari zako."

Haya ndio maisha tuliyokua tunaishi na Rely kwa kipindi hiki. Alibadilika sana kiasi kwamba heshima yake na upendo wake wa zamani ulipotea. Niliwaza sanaa nikaona kama yule mwanaume wake ndio anampa kiburi si amchukue akaishi nae? Hivi ni nwanaume gani anaeweza kukaa na wewe na hali ya kuwa anajua una mwanaume mwingine lakin hakwambii kitu na badala yake anaendelea kukutunza na kulea ujauzito wako ambao pia hana uhakika kama analea kiumbe chake au kiumbe cha mwanaume mwenzie? Hayupo mwanaume wa hivyo si ndio?

______
Hussein alitoka akaelekea sehemu ambayo alikuwepo mwanasheria wake ambae alikua amemzoea sana katika kuweka mambo yake sawa.

"Bwana Michael nimekuja hapa kuna kitu nataka unisaidie!"

"Kitu gani Hussein, we sema tu mi nipo hapa kwa ajili ya watu kama nyie."

"Kuna nyalaka nataka ubadilishe jina na uweke jina langu maana pale kuna jina la mke wangu Rola."

"Sasa hili swala kwanini hamkuja wote apa kulitatua kwasababu itahitajika sahihi yake pia."

"Aaah hakuna haja ya sahihi yake maana yeye mwenyewe ndio kanipa hili agizo so fanya kama navokwambia kiongozi."

"Lakini ni..." Hakuweza kuongeza neno kwani wakati ule ule bahasha yenye pesa ilitua mezani kwake na kumfanya abaki anashangaa.

"Tufanye kazi, pesa ipo na kama haitoshi nitakuongezea. Hili jambo ni la muhim sana naomba nisaidie tafadhali."

"Sawa hakuna shida, hizo nyalaka zipo wapi?"

"Nilitaka kuzungumza na wewe kwanza na kwakua umekubali basi kesho ntakuja nazo ili tumalize kazi."

"Sawa sawa hakuna shida."

"Basi sawa mi acha niende, kwaheri na Asante sana."

Hussein aliaga na kuondoka huku akimuacha Mwanasheria wake Mr Michael akiwaza na kuwazua.

"Huyu Hussein anataka kuleta balaa kwasababu kuna mali tayari ambazo ameandikwa jina lake sasa inakuaje anataka na mali zingine za Rola? Ebu kwanza nione hizi pesa ni kiasi gani."
Alitoa pesa na kuzihesabu na kukuta kiasi cha million mbili.

"Hizi pesa ndo zinifunge? Hapana, natakiwa kufanya kitu, mimi mwenyewe mji naujua vile vile na hii kazi sijaanza leo. Hapa lazima nimsaidie mtoto wa kike. Huyu Hussein ataongeza pesa lakin bado nitamla, tulia nimuoneshe."
Alisema mwanasheria yule na kuchukua sim yake akachezea kidogo na kuweka sikioni.

Rola aliitafta ile bahasha kila sehemu lakin hakuipata. Kumbe wakati anafungua droo alikua anahitaji kuchukua ile bahasha ambayo inaonekana kuwa na nyalaka muhim sana za mali zake.

"Mungu wangu!! Imeenda wapi hiyo bahasha?" Alisema Rola huku akiwa amechanganyikiwa kitu kilichofanya kuanza kutupa vitu hovyo huku na huko akiitafta bahasha lakin hakuiona.

"Huyu atakua Hussein huyu, sijui anataka nini kwangu jaman!"
Rola alichukua sim yake haraka na kutaka kumpigia Hussein lakin mda huo huo sim iliita na namba aliisave Mwanasheria, akapokea.

"Mr michael." Aliita Rola.

"Yees, habari yako Madam?"

"Salama, nambie."

"Aaah samahani, mumeo yupo hapo?"

"Hayupo na ndio namtafta hapa!"

"Aaah sawa, sasa nakuomba ofisini kama utakua na mda sasa hivi kwasababu kuna kitu nataka tuweke sawa."

"Kitu gani? Mi nadhani ungeniambia saa hizi maana nina kazi nafanya."

"Sawa ni kuhusu Hussein alikuja hapa na akasema kwamba anataka kubadilisha jina Kwenye nyalaka ambazo zina jina lako lakin nikamwambia inahitajika sahihi yako na hakutaka kuelewa hilo swala. Sasa amesema kesho anakuja nazo ndo maana nimetaka kukushirikisha na wewe."

"Yaani anataka kunigeuka au?" Aliuliza Rola kwa hasira.

"Nadhani hivyo, so kuwa makini nae sana."

"Ntakupigia badae Mr Michael ngoja nideal nae kwanza."

"Naomba usimwambie kitu chochote kwanza kuhusu mimi."

"Usijali."
Rola alikata sim na kuitupa kitandani akiwa na hasira sana akaanza kuzunguka huku na huku kama mtu anaewaza kitu flani lakin hakimjii akilini.
Akiwa pale mlango ulifunguliwa akaingia Hussein.

"Ulikua unaongea na nani? Nimesikia mazungumzo yenu."

"Sihitaji kelele Hussein."
Alisema Rola na kutoka mpaka sebleni. Hakutaka kumwambiaa kitu Hussein kwa wakati ule akihisi kwamba Hussein atagundua kitu walichoongea na mwanasheria Michael bila kujua kwamba Hussein alisikia mazungumzo yao wakati akiwa pale mlangoni bila ata Rola kujua.

"Huyu Michael hanijui kumbe, anataka kunigeuka anahisi ataweza? Hahaa ntamuonesha, ngoja nimfate muda huu."
Hussein alisema kisha alitoka akiwa na bastora aliyokua ameiweka kiunoni na kuondoka zake. Alivofika sebleni Rola akamsemesha.

"Ni bora kama ungeondoka jumla nimechoka kukuona kwenye nyumba yangu!"
Rola aliongea kwa kufoka kidogo lakin Hussein hakujibu kitu zaidi ya kufungua mlango na kuondoka kuelekea kwa mwanasheria na bila shaka anaenda kufanya mauaji. ITAENDELEA

.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

DO YOU LOVE ME 14 (S2) https://gonga94.com/semajambo/do-you-love-me-14-s2 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MARIA Sehemu 16

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MARIA Sehemu ya 10

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MARIA Sehemu ya 7

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

RATIFA sehemu ya 37

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

RATIFA sehemu ya 36

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

Obi's Pain Chapter 4.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

TAMU YA SAKINA 02.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DEAR DOCTOR 01

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MPANGAJI ... 01

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 15

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 14

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

TAMU YA SAKINA 01

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

Obi's Pain Chapter 1

mjukuu rewards 100 Comments 1
 

MSHANGAZI EPISODE 2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 14

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MSHANGAZI EPISODE 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 13

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 10

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

YAMENIKUTA

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 9

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINSI YA KUTUNZA UKE

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

PART 5 MY HEART

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest