DO YOU LOVE ME 18 (S2)
IF THAT, SHOW ME A RIGHT WAY
Haraka sana nilimuambia Dereva Taxi kughairisha safari, atupeleke nyumbani kwetu. Rola alinielewa na tulirudi hadi nyumbani, tulipoingia ndani tulikuta mwili wa Rely ukiwa unaning’inia katika kitanzi. Alikwisha jinyonga.
Ukiniuliza, upi ulikuwa wakati mgumu kwako katika maisha yako yote? Basi nitakutajia ni hii siku ambayo nilishuhudia mwili wa Rely ukining’inia. Ulikuwa ni wakati ambao siwezi kuusimulia mara mbili mbili lakini wajuzi wa mambo wanadai kuwa licha ya ‘depression’ yaani msongo wa mawazo ambao Rely alikuwa nao. Lakini pia nyuma yake kuna karma ambayo ilitengenezwa na wazazi wake. Lile la kuwaua wazazi wa Rola na kumtesa Rola, kwasasa linawarudia kwa sababu Karma inaangamiza kizazi na kizazi. Nisiende sana huko sababu wengine hawaamini haya mambo.
Nakumbuka tulipiga simu polisi, wakaja wakafanya uchunguzi na mtu wa kwanza kudhaniwa kuwa amehusika katika mauaji yale ni Mimi. Nikafungwa pingu na kusweka lumande nikisubiri uchunguzi uendelee. Lakini nilikuja kuwaambia ukweli, mimi sikuwa sehemu ya watu ambao wamemtaka Rely ajinyonge bali yalikuwa ni maamuzi yake.
Maelezo yangu niliambatanisha na meseji ya mwisho ambayo nilitumiwa. Waliniamini baada ya kupima maelezo na ushahidi ambao nimeutoa. Sikuwa na kesi isipokuwa katika simu ya Rely kulikuwa na meseji za vitisho kutoka kwa Calvin akimtishia maisha kama akiendelea kumfuatilia. Mzigo ukadondoka kwake, polisi hawakuwa na mchezo tena.
Walianza kumfuatilia na ndani ya wiki tu, Calvin alipatikana akafunguliwa kesi. Mashataka yakafika mahakamani. Kesi yake ikanguruma kwa zaidi ya wiki 15. Hakuweza kukwepa sakata lililokuwa mbele yake kwamba amesababisha hadi Rely kujiua. Hakim akampiga nyundo 20 jela kwa kosa hilo. Mke wake alimlaumu na kumtukana. Akidai kwamba bila tamaa zake za kuchepuka hata haya yasingetokea. Yule Mama alilia sana siku ile mahakamani, hakukuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana na hukumu ile.
Hapa ndipo maisha ya Mimi na Rola yakaanza rasmi, maisha ambayo yalikuwa na msongo wa mawazo ya kuondokewa na Rely wetu. Maisha ambayo yalikuwa na furaha katika eneo fulani. Tulifunga ndoa huku Mama na Thelesia wakisimamia
Haikuwa ndoa tamu lakini sisi wenyewe tulifurahia. Siku moja Rola aliniambia kwamba kama ikiwezekana basi tufanye kitu cha kumbukumbu kuhusu Rely. Kitu ambacho kitakumbukwa ulimwengu wote na hata kama tukifa basi watu watajivunia uwepo wetu.
“Labda tufungue shule?” nilimweleza
“Wazo nzuri lakini kwanini tusiwe na foundation na iitwe Rely Foundation?”
“Sio mbaya. Swali ni je, itahusu nini hiyo foundation?”
“Tutadili na watu wenye matatizo ya akili, usonji na msongo wa mawazo. Hapa tu’deal na watoto wadogo. Kama uliweza kunisaidia mimi na nikapona ingawa nilikuwa nimerogwa, sidhani kama utashindwa kusimama na kuwasaidia wengine huko nje?” Rola alinieleza na kunifafanulia namna gani wazo lake linaweza kufanya kazi.
Sikuwa katika upande wake kwa siku za mwanzoni lakini ilifikia kipindi ilinibidi nikubali. Tukafungua kituo chetu ambacho tulikiita ‘RELY FOUNDATION’ Nashkuru Mungu, tulianza vizuri. Mwezi mmoja mbele tukapokea barua kwamba kesi ya Hussein inaendelea na hukumu yake inatolewa siku za mbeleni. Tukafunga safari tukiwa na Thelesia hadi Zanzibar.
Siku ya pili tukaamkia Mahakamani ambapo kesi ilisomwa na Hussein alikuwa na hatia ya kuficha nyalaka ili apate mali. Kugushi nyalaka na kuibia watu wengine. Miaka 10 jela ikamuangukia.
“Ingekuwa hata miaka 100 mshenzi huyu” Rola aliniambia tukiwa tunatoka pale mahakamani.
“Hukumu hutolewa lengo sio kukomoa bali kuwafunza wengine. Hiyo aliyopewa inatosha kuwa fundisho huko nje” Nilimweleza.
Huu ndio ukawa mwanzo wa maisha ya furaha kati yetu. Maisha ya amani na mazuri ambayo hadi sasa tuna miaka sita katika ndoa ambayo tuliifunga na tumempata mtoto mmoja wa kike ambaye tumemuita Rely. Ana miaka minne.
Rely ni mtundu, mkorofi na muongeaji kama Rely mwenyewe. Namna ya utazamaji wake, uongeaji wake wa haraka haraka na kuuliza uliza hata kutembea alikuwa ni Rely. Amefanana na marehemu. Kuhusu kumpenda hilo usiulize sababu mimi ndio nilimpa jina. Mimi ndio namchukulia kama mtu muhimu zaidi na sio kwamba Rola hampendi lahasha bali wote tunampenda na tunaenzi yale mazuri ambayo marehemu Rely alituachia.
Siku moja tukiwa ufukweni tunapata upepo, mke wangu alihisi kizunguzungu. Akadondoka na kupoteza fahamu, nilihisi kuchanganikiwa kwanini imekuwa hivi? Haraka sana nilimpeleka hospital. Dakika 56 mbele Daktari aliniita na kuniuliza.
“Alishawahi kuwa na ujauzito hapo kabla?”
“Mke wangu ana ujauzito?”
“Swadakta, ana ujauzito?” hii ilikuwa ni taarifa nzuri sana kwetu maana Rola alikuwa na ujauzito mwingine. Nikaenda kumpongeza mke wangu kwa mabusu ya paji la uso. Wote kwa pamoja tukawa na hamu kubwa ya kujua ni jinsia gani ya huyo mtoto ajae. Mimi nilitamani awe wa kike, Rola akatamani awe wa kiume. Mungu ndio angetuamulia. Nilimgeukia Rola na kumwambia.
"WASIKUDANGANYE, HAKUNA ANAYEJUA UZURI WAKO ZAIDI YANGU. TAFADHARI, POKEA UPENDO HUU" niliona Rola akinitazama kwa hisia, akanijibu.
“NITAKUPENDA HADI MWISHO WA MAISHA YANGU” Maneno yake yakaukonga moyo wangu. Nilihisi fahari kuambiwa hivi.
Naomba niweke hapa tamati ya simulizi yangu. Mimi na Rola ni wanandoa na tuna watoto wawili, wa kike na wakiume. Rely na Rolen.......
MWISHO
Mapenzi ya dhati yapo, ukiyahitaji yanapatikana. Kuwa mkweli ili usijifunge kwa idadi ya makosa unayoyafanya. Jitoe kwa unayempenda ili aone thamani na umuhimu wako maishani.
SHUKRANI
AHSANTE KWA UPENDO wako na kuthamini andiko hili takatifu lililoandikwa nami naitwa Sam Darfur nikishirikiana na Mwandishi Mwenzangu, Ray Kido.
Nitakuwa mchoyo wa fadhira kama sitamshukuru MwenyeziMungu kwa kunibariki kipawa hichi cha uandishi kuanzia nilipoanza kuandika hadi hapa pamoja na baraka nyingi alizozijaza katika maisha yangu ikiwemo ya kufahamiana na wadau mbalimbali.
Lakini pia kwa kutambua watu walionizunguka, Ninamshkuru Mama yangu pamoja na Baba yangu. Hawa ni sehemu ya watu walionihamasisha kuweka andiko hili katika ubora kupitia kauli yao ya 'pambana mwanangu, mjini mtu anakula kwa jasho lake” Mungu awabariki wazazi wangu popote mlipo sababu maneno yetu yamezaa kazi hii.
Pia namshukuru sana Halid Salum kama sehemu ya watu ambao wameweka mawazo mbalimbali kwa kunikosoa na kunirekebisha pale alipohisi sio sahihi hadi SEASON ONE NA TWO kukamilika.
Lakini pia nitakuwa Mchoyo wa fadhira kama sitamshukuru Mwandishi RayKido kwa kuandika sehemu ya ishirini ya season one pamoja kipande cha 7 hadi 15 cha season two huku akiweka mawazo mengine ya kazi hii. Hakusita kuniambia naona hapo ungeweka hili, ungefanya hivi na vile.
Shukrani zingine ziende kwa Mwandishi Husqer Bultazar, alipokea simu yangu kila nilipohitaji ushauri kutoka kwake, akaweka mawazo yake katika kazi hii. Wote Mungu awabariki na tuzidi kushirikiana katika kuijenga jamii.
Shukrani ziende kwa kampuni mbili ambazo zimesimamia kazi hii hadi kuingia sokoni. Ahsante kwa kampuni ya SOMANOW ambayo ndio wamesimamia usambazaji wa kazi hii pamoja na kampuni ya NOW ambao ndio watengenezaji wa kifungashio (Kava) la kazi hii.
Shukrani za ziada zikufikie wewe mdau ambaye umenunua kazi hii, hakika wewe ni wa muhimu. Umeonesha jinsi gani unaweza kuchangia hata kazi zangu zijazo ikiwemo BEFORE WEDDING na nyingine nyingi.
Lakini pia nikushkuru wewe mdau ambaye umeipa utulivu kazi hii kwa kusoma hata kama hujanunua lakini ulichokifanya ni kikubwa sababu ungeweza kupuuza na kusoma kazi zingine lakini ukaamini katika kipaji changu. Ahsante sana
Binafsi, naomba DO YOU LOVE ME? iwe funzo kwetu na usisite kubaki na mimi katika riwaya zangu zingine zijazo. Kama ungependa nikuunge katika group langu la Telegram ili usome kazi zangu zingine basi nitext kwa namba 0717255498 ili nikuunge.
TAFADHARI
Mazingira, majina na matukio yote yaliyopatikana katika kazi hii ni ya kubuni na kufikirika. Hivyo, haihusiani na hali halisi, bali ni mali ya mwadishi na mtunzi ambaye amebuni na kuumba kila ulichokisoma..