DO YOU LOVE ME 10 (S2)
UNTOLD STORY
Baada ya Rola kumuuliza Hussein lile swali, Hussein hakuwa tayari kujibu na badala yake alisimama na kuelekea chumbani. Rola alibaki akimuangalia asijue shida ni nini? Hakuona sababu ya kuendeleaa kubaki pale yeye mwenyewe hivyo na yeye akaamua kumfata huko huko.
"Hii tabia imeanza lini Hussein??"
"Kwani unataka kujua nini wewe??"
"Nataka kujua una mwanamke mwingine tofauti na mimi??"
"Ndiyo ninae!" Hussein alijibu lile swali na kumuangalia Rola ambaye alikua kama vile amepigwa na shoti ya umeme kwasababu alijikuta anakosa nguvu na kubaki ameganda kama sanamu la posta.
Hussein hakutaka kuongea tena baada ya kumuona Rola kama kashtuka, alichokifanya ni kupanda kitandan na kulala.
Rola alijikuta akitoa machozi na kubaki akijiambia kwamba huwenda zile zilikua ni hasira tu ndio maana amemjibu vile. Usingizi kwake siku hii haukuwa mzuri kama ilivyokua kawaida kwake, alikumbuka maisha yake na Hussein kipindi cha nyuma yalivyokua lakini hakuweza kuamini kama alichokisema Hussein alikua anamaanisha.
Ni siku nyingine tena katika jumba la Rola, Rola hakuwa sawa hata kidogo. Haya yote nilisimuliwa na mwenyewe. Ko anasems alikua ni mtu mwenye mawazo sana kutokana na kumfikiria Hussein kwa muda mrefu. Siku hii akiwa amekaa katika kiti chake, simu yake iliita lakini namba ilikua ni ngeni na alivyoiangalia ni kama alikua anaijua hivyo akapokea na kisha sauti ya kike ikasikika..
"Haloo.."
"We mwanamke umempa nini mume wangu??" Aliuliza swali mwanamke aliyekua anaongea na Rola swali ambalo lilimfanya Rola kukumbuka kuwa huyu mtu alikua ameshampigia tena na kudai kwamba Hussein ni mume wake.
"Dada samahan, sikujui hunijui naomba kaa na huyo mume wako muongee na akwambie kila kitu kwasababu hakuna ninachokijuaa kuhusu yeye."
"Unajifanya jeuri si ndio?? Sasa nakupa siku mbili tu uachane na Hussein vinginevyo nitakufanya kitu kibaya sana ambacho kitakua kinakupa kumbukumbu mbaya kila ukikikumbuka." Alizungumza mwanamke yule na kukata sim yake.
Rola alibaki njia panda, je amskilize huyo mwanamke au aendelee na mambo yake?? Lakini amepewa siku mbili tu za kuachana na Hussein na asipoachana nae kuna kitu kitamkuta na yeye hayupo tayari kwa chochote sio kumuacha Hussein wala kupatwa na kitu kibaya. Aliwaza sana lakini mawazo yake yaliishia kwenye sim yake ambayo ilikua inaita na mpigaji nilikuwa ni Mimi, Rahim. Hapa aliwaza mara mbili mbili apokee au asipokee, alijifikiria lakini mwisho aliona kupokea ndio jambo sahihi..
"Rola."
"Nakusikia"
"Habari yako?"
"Salama nikusaidie nini?"
"Aaah.. hapana nilitaka tu kukujulia hali, mnaendeleaje hapo nyumbani?"
"Hayakuhusu Rahim, fanya yako!!"
"Lakini ni.."
"Nimesema hayakuhusu Rahim fanya yako full stop!!" Alinijibu kwa hasira sana lakini sikuwa na namna ikabidi niwe mpole kwasababu kihere here changu cha kumtafuta mwanamke ninayempenda ndio kimeniponza.
Rola alikua ni mtu mwenye mawazo na hasira kwa wakati mmoja na kama ungethubutu kumsemesha kwa siku hii basi ungekutana na matusi yasiyoelezeka.
Rola alinisimulia kwamba; Majira ya jioni, Hussein alirudi nyumbani lakini alikuwa na haraka sana kana kwamba kuna sehemu alikua anataka kwenda. Alikua bize sana kitu ambacho kikampa Rola wasi wasi na kuamua kuuliza.
"Hussein nina mazungumzo na wewe, unataka kwenda wapi??"
"Kuna sehemu nawahi, hayo mazungumzo tutazungumza hata kesho kama ikiwezekana."
"Unaenda wapi?"
"Nimekwambia kuna sehemu nawahi."
"Wapi?"
"Sitaki maswali yako Rola, elewa kuna sehemu nawahi basi!"
"Hauendi popote mpaka nijue hatima yangu mimi na huyo mwanamke wako!"
"Unataka kujua nini sasa na tayari nilishakwambia kwamba nina mwanamke mwingine?"
"Ndio unapokwenda sasa hivi sio?"
"Nipishe nipite bwana nachelewa..!"
"Nimesema hakuna kwenda Hussein!"
Zilikuwa ni kelele ambazo hazikua na mantiki yoyote kwasababu Rola hakutaka Hussein atoke lakini Hussein alitaka kutoka. Kelele zile ziliendelea mpaka wakatoana nje ya chumba chao huku wakizidi kurumbana na Hussein alikua akimsukuma Rola amuachie huku Rola anamvuta Hussein abaki kwahiyo. Ikawa ni vuta nikuvute ambayo mwisho wa siku ilisababisha ajali kwani katika vutana vutana ile Hussein alimsukuma Rola na kwa bahati mbaya aliseleleka kutoka kule juu ghorofani hadi chini, Hussein aliona ndio njia sahihi ya yeye kutoka kwa wakati ule kwasababu kulikua na wafanyakazi hivyo aliamini watamsaidia Rola.
Rola alianguka vibaya na kujiumiza sehemu mbali mbali za mwili wake ikiwemo kichwani. Zile kelele zilimshtua sana mfanyakazi hivyo alitoka kuangaliaa sebleni na kukuta Rola akiwa ametuliaa tuli huku akivuja damu puani. Alipiga kelele akiomba msaada, akatoka hadi nje akaomba mlinzi amsaidie wampeleke hospital kwani hali yake ilikuwa mbaya sana. ITAENDELEA.