DO YOU LOVE ME 15 (S2)
WANTED AGAIN
Hussein alitoka mpaka kwa mwanasheria lakini hakumkuta. Mda huo pia Rola alitoka pale sebleni akaenda kwenye vitu vya Hussein na kuanza kutafta hiyo bahasha aliitafta sana lakin kwa bahati nzuri aliipata akaichukua na kwenda kuiweka chumbani kwa Thelesia.
"Naomba ukae na hii, najua atakua ameenda huko kwa Mr Michael lakin hatompata." Alisema Rola akimaanisha kwamba anajua Mr Michael hayupo kule na bila shaka yeye ndo anajua alipo.
"Usijali, hapo ulipoiweka hakuna mtu ataweza kujua isipokua Mimi na wewe tu, ila nakushauri ukamshtaki maana anaweza kukuua ata wewe."
"Hawezi, najua cha kumfanya hawezi kunihangaisha kiasi hiki. Mimi nilijua he is a good guy lakin alikua anapretend. Nashukuru sana kwasababu ulimuona wakati anasikiliza maongezi yangu na mwanasheria maana bila hivyo ingekua shida. Huyu ni mtu mbaya sana ila ntamkomesha."
Wakiwa pale wanapanga mikakati yao, aliingia Hussein akiwa ni mwenye hasira sana lakini hakuna aliejishughulisha nae kila mtu akawa bize na yake. Aliingia moja kwa moja adi chumban akaanza kuongea mwenyewe huku akizunguka zunguka pale ndani.
"Kuna mchezo unaendelea hapa haiwezekan. Inamaana mwanasheria kaenda wapi? Kwahiyo wanajuana na Rola kiasi kwamba wameamua kushirikiana?? Hapana na kama wanashirikiana mbona Rola hajasema kitu kuhusu hiyo bahasha niliyoichukua au hajui? Kama hajui anatakiwa kuendeleaa kutokujua hivyo hivyo mpaka siku atakayoshangaa tu anatolewa kwenye kampuni zake na kupolwa kila kitu na hapo ntakua nimeshinda na ntaanza maisha mapya na mke pamoja na mtoto wangu."
Hussein alikua akiwaza hayo wakati akiwa amesimama kwenye dirisha akiangalia nje.
Baada ya kuwaza sana aliamua kutoa vitu vyake akiimani kwamba mpango wake umeenda kama alivyotaka kumbe hakujua kuwa yeye ndo ameliwa changalamacho. Alitoa nguo zake pamoja na baadhi ya vitu mpaka sebleni.
"Na ukienda usirudi, mwanaume hujui kupenda wewe unajua kutenda tuu." Aliongea Rola kwa dharau akimpandisha Hussein juu mpaka chini.
"Naenda lakini utakuja kujutia uamuzi yako Rola. Na utakuja kwangu kwa magoti!" Alijitapa.
"Nendaa bwanaa, nije kwako kwa magoti kwakua miguu yangu haitembei au vipi? Ebu nenda toa giza hapa!"
Ni Rola huyu huyu ambae alikua hasikii chochote wala haoni chochote linapokuja swala la Hussein leo ndo anaongea maneno kama haya. Aisee mwanamke akishakuchoka ni balaa tupu.
"Tena kukuhakikishia kwamba sitokuja kwako kwa magoti wala kwa kilio ni kwamba ata nyumba ile niyoandika jina lako pamoja na gari nimekuachia, nenda kadunde navyo mjini si ndo kazi yako hiyo, haya nenda na uwasalimie."
Ama kweli siku hii Rola alichafukwa vilivyo.
Hussein aliondoka zake kwa amani kabisa bila shaka kwasababu alijua utajiri wa Rola anao yeye.
"Thelesia tunatakiwa kuhama hapa upesi sana. Turudi dar au unashaurije wewe?" Aliuliza Rola.
"Ni wazo zuri kwasababu Hussein lazima atakufatilia. Kwahiyo ni bora tuhame huku alafu ukafungue kesi polisi kuhusu yeye."
"Nawaza hivyo pia, sasa sikia naenda kuweka mambo sawa natafta na mteja apa, hii nyumba tuiuze tukatafte nyumba nyingine dar lakini nahisi tungeongea na Rahim kwasababu yeye kule ni mwenyeji atutaftie nyumba."
"Yeaah itabidi tumtafte."
"Sawa nakuja." Aliongea Rola kisha akatoka kuelekea nje na mwisho ulisikika tu muungurumo wa gari kumaanisha alikua anatoka.
Baada ya siku mbili kupita, siku hii Hussein alikua anatafuta ile bahasha aliyokua ameiweka kwenye begi lake la nguo kwa chini kabsa lakin hakuiona. Alitafta kila sehemu lakin hola. Alitafta na kutafta lakin wapi. Alichoka!
"Rolaaaa!!!" Alipaza sauti yake kwa hasira sana adi mke wake akamfata.
"Una nini Hussein? Mbona kelele?"
"Huyu mwanamke ntamuuaa!!" Alifoka.
"Kuna nini kwani?"
"Ile kitu niliyoichukua haipo, haipo ile bahasha, shit!!!" Alisema kwa hasira huku akivuruga vuruga vitu vyake akijaribu kuitafta tena.
"Tulia na uiangalie vizuri huenda ukaipata!"
"Haipooo!!!" Alifoka tena kwa hasira na safari hii alitoka na funguo yake ya gari na kuelekea kwa Rola.
Wakati yeye anapanga kwenda kwa Rola kumbe mda huo Rola alikua yupo hotelin yeye pamoja na Thelesia wakiendelea kupanga mikakati dhidi ya Hussein.
"Nimepata namba ya Rahim." Alisema Thelesia huku akimpatia Rola simu.
"Nipe niongee nae." Rola alichukua sim ya Thelesia na kumpigia Rahim.
"Haloo, Rahim mzima wewe?"
"Niko poa, naongea na Rola sio?" Niliuliza kwasababu niliifaham sauti ya Rola atakama angetumia sim ya mtu mwingine.
"Yeaa ni mimi, tuna shida na nyumba huko dar maeneo ya mbezi sijui unaweza ukatutaftia?"
"Mnataka kupangisha au kuna mtu unamtaftia?"
"Aaah ni sisi ndio tunatafta, na ingependeza kama tungepata leo au kesho kwasababu tuna haraka."
"Kuna usalama kweli?" Niliuliza kwa wasi wasi.
"Hapana, hakuna shida naomba utusaidie kwa hilo."
"Sawa nitakupa feedback badae."
Simu ilikatwa huku nikiendelea kuwaza nin kimetokea maana ata ongea ya Rola imebadilika anaongea kistaarabu jambo ambalo sio kawaida yake haswa akiwa anaongea na mimi, au kwakua ana shida? Sikutaka kuwaza sana kuhusu yeye na badala yake niliingia kwenye sim yangu na kuitafta namba ambayo niliisave dalali kisha nikampigia.
"Haloo Jose"
"Bwana Rahim kwema?"
"Kwema ndugu yangu sema nilikua na shida na nyumba maeneo ya mbezi huko sijui nitapata?"
"Nyumba zipo sijajua wewe unataka ya aina gani?"
Kwa jinsi nilivokua najua maisha ya Rola ni lazima angekua anahitaji nyumba yenye hadhi yake kwahiyo sikua na shida sana katika hilo. Nilimwambia yule dalali nyumba inayohitajika na kisha akanipa bei, suala likabaki kwangu kuongea na Rola kumpa mrejesho.
___________
Hussein alifika mpaka pale kwa Rola lakini cha ajabu alikuta kufuli getini na bango juu "NYUMBA INAUZWA" Alishtuka kwasababu hakutegemea kama Rola angeweza kukimbia na kuuza nyumba.
"Amehama mji au kauza nyumba tuu kaendelea kubaki hapa Zanzibar?" Alijiuliza Hussein kisha akatoa sim na kumpigia Rola lakin sim haikupokelewa na badae akawa anaambiwa inatumika kumaanisha kwamba alishalishwa block mpaka pale. Hussein alichoka sana hakujua anampatia wapi Rola. Akiwa pale anawaza kuondoka sim yake iliita lakin ilikua ni namba ngeni akaona apokee ajue nani kampigia.
"Haloo."
"Haloo, unaongea na Afisa polisi apa kituo cha kati, unahitajika kituoni sasa hivi." Sauti upande wa pili ilisikika iliyomfanya Hussein kubaki anashangaa, polisi tena? Imekuaje?
"Kuna nini kwani afande?" Aliuliza kwa wasi wasi.
"Ukija utajua, ila ni muhim sana kufika, asante." Simu ilikatwa na kumuacha Hussein akiwa kachanganyikiwa hakuelewa ni nin kinaendelea. Aliwaza lakini mwisho aliona wacha aende akajue nini kimetokea.
"Haloo. Eeh Rola nyumba nimepata sasa sijui mnakuja lini?" Nilimpigia Rola na kumuuliza baada ya kuwa nimepewa zile taarifa na dalali ambae alifahamika kama Joseph.
"Woow kweli? Sasa sikia, sisi tutafika apo asubuhi na boti nakuomba uje utupokee ili utupeleke huko."
"Aaah sawa haina shida."
"Asante sana Rahim." Alisema Rola kwa utaratibu kabisa na sauti yake laini.
"Usijali nipo kukusaidia endapo utapata shida."
"Sawa badae."
Nilikata simu lakini nilivyoangalia upande wa pili nilikuta Rely ananiangalia tena kwa jicho la hasira sana sikujua kuna shida gani mpaka aniangalie vile ikabidi nimuulize. ITAENDELEA
.