DO YOU LOVE ME 12 (S2)
TAKE ME BACK
Baada ya kumpiga Rely kila kibao ni kama vile nilikua nimeyaamsha mashetani yake kwani baada ya zile kelele aliamka pale kitandani na bila kuongea kitu alianza kupark vitu vyake.
"Unafanya nini sasa?" Nilimuuliza.
"Niache Rahim, niache na usiniambie chochote." Alinijibu huku akiendelea kupanga vitu vyake huku akiwa analia.
"Sasa unapanga hivyo vitu vyako unataka kwenda wapi usiku huu? Ebu acha mara moja hicho unachokifanya!" Nilimwambia vile nikiiamani ataacha lakini ni kama nilikua nampigia mbuzi gitaa. Aliendelea kutoa nguo zake kwenye kabati na kutia kwenye begi.
Nilichokifanya ni kutoka chumban mpaka seblen, nikafika nikafunga mlango na ufunguo kisha ufunguo nikaweka kwenye mfuko wangu wa suruali. Nikaelekea chumbani pia nikachukua sim yake iliyokua kitandani na kuiweka mfukoni pia.
"Nimesema Rely acha unachokifanya nikwa.."
Sikuweza kumaliza kuongea nilichotaka kusema, simu yangu ikaita na mpigaji alikua ni Thelesia nikapokea.
"Thelesia." Niliita upande wa pili kitu kilichofanya ata Rely kuacha anachokifanya na kugeuka kuniangalia.
"Rahim, Dada Rola yupo kwenye matatizo." Aliongea sauti yenye kitetemeshi ndani yake iliyonifanya kurudisha swali kwake.
"Rola? Kawaje, yaani nini kimetokea?" Niliuliza huku nikiwa na wasi wasi ukizingatia ni mtu ninaempenda sana.
"Hussein alimsukuma kwenye ngazi kitu kilichopelekea akaanguka na kuumia sana, sasa hivi tupo hapa hospital."
"Yaani, yaani unasema kwamba ameumia? Sawa umetoa taarifa polisi kuhusu huyo Hussein?? Nin kinaendelea mpaka sasa? Fanya hivi nakuja kesho mapema sana asubuhi ntakua apo, kuweni makini." Niliongea nikiwa nimechanganyikiwa kabisa, nilisahau kabisa kuhusu swala la Rely kutaka kuondoka. Nikiwa nawaza nini cha kufanya, Rely alinisemesha.
"Kuna nini?" Aliuliza akisogea sehem nilipokua.
"Rola anaumwa, amelazwa na inasemekana mume wake Hussein ndio kamsukuma kwenye ngazi ikapelekea yeye kuumia vibaya"
"Kwahiyo inakuaje?"
"Kuhusu nini?"
"Utaenda au?"
"We utaenda au?"
"Sasa mi si ndo nimekuuliza si unijibu!"
"Unataka kujua nin? We si ulikua na safari imeishia wapi?"
"Yule ni ndugu yangu natakiwa kujua kuhusu yeye."
"Hauna namba zake? Sikia Rely usinichoshe." Nilimjibu kisha nikapanda kitandan na kuutafta usingizi ambao haikua rahisi kuupata kwasababu mawazo niliyokua nayo ni mengi sana kichwani kwangu.
Nikiwa kitandani nilimskia Rely akitokea seblen akiitilia jina langu kwa sauti na hasira kama vile amechanganyikiwa.
"Rahim naomba ufunguo. Naomba ufunguo nimesema. Halafu na simu yangu ilikua hapa kitandani haipo na wewe ndo umeichukua naomba Simu yangu naomba na ufunguo niondoke zangu. "
"Rely sitaki kelele, hivi we una akili timamu? Yaani unataka uende wapi usiku huu na hiyo hali yako? Kikikukuta cha kukukuta huko nani atalaumiwa kama sio mim? Sikia nikwambie, huendi popote sasa hivi labda kama hiyo mimba sio yangu. Au kama una uwezo hilo tumbo acha hapo na uondoke peke ako." Niliongea nikiwa namaanisha kabisa ninachokisema kwani baada ya kumaliza niligeukia upande mwingine wa kitanda na kuendeleaa kuutafta usingizi.
Rely alibaki pale asijue cha kufanya maana kusema tu ukweli uwezo wa kunipiga hakua nao, asingeweza kufungua mlango aondoke kwasababu ufunguo ninao mimi. Kwahiyo hakua na cha kufanya kwa wakati ule zaidi ya kupanda kitandan kulala.
Kesho yake mapema sana niliamka na kwenda Zanzibar, nilipanda boti asubuhi na kuelekea nyumban kwa Rola. Nilifika na kumkuta Thelesia akiandaa chakula na kwa wakati huo alikua anamalizia malzia kwahiyo tulitoka wote na kwenda mpaka hospital alipolazwa Rola.
Tukiwa tunaingia tulikutana na Hussein aliyekua amekuja pia kumuona Rola. Hakuna aliemsemesha mwenzie japo mimi na yeye tuliangaliana macho ya kuonya yaliyodhihirisha hasira zilizokuwemo ndani yetu haswa kwa upande wangu. Nilikua na hasira zisizoelezeka. Tukiwa pale alikuja daktari alieturuhusu kuingia kumuona Rola aliekua amepata nafuu kwa wakati huo.
Baada ya kuingia tu Rola alianza kulia. Bila kupoteza muda nilisogea pale alipo na kumfuta machozi yaliyokua yanatoka kwenye macho yake.
"Pole Rola utakua sawa." Nilimwambia taratibu huku nikiwa nafuta machozi yake."
"Unafanya nini hapo na mke wangu?" Sauti ya Hussein ilifika kwenye masikio yangu na bila hata kumsikiliza niliendelea na zoezi langu la kumbembeleza Rola.
"Nakuuliza unafanya nin hapo na mke wangu?" Safari hii alinisogelea na kunivuta shati na kunirudisha nyuma.
"Hussein stop it!" Aliongea Rola kwa sauti iliyokua na kilio ndani yake.
"Naomba uondoke, toka kabisa nisikuone kwenye macho yangu. Ondoka!" Alifoka Rola.
"Lakini nipo hapa kukuangalia mke wangu"
"Sihitaji uangalizi wako, naomba uondoke!"
Hussein alichukia baada ya Rola kumwambia vile kwahiyo hasira zake akazirudisha kwangu.
"Tutakutana!"
Alinambia hivyo tu kisha akafungua mlango kwa hasira na kuondoka. Tulibaki pale mimi, Thelesia na Rola tukiwa tunaangaliana kwa zamu huku mda wote macho ya Rola yakiwa yanatiririka machozi. ITAENDELEA
.