DO YOU LOVE ME 11 (S2)
SHE LIED ME
Thelesia ambaye ni mfanyakazi wa Rola pamoja na mlinzi walishirikiana kumpeleka Rola hospital, na walipofika Rola alichukuliwa na kuanza kupewa matibabu.
Tuachane na Rola, turudi keangu sasa. Ilikuwa hivi kuhusu Rely; Maeneo ya hotel moja yenye hadhi yake ya nyota tano, anaonekana Rely akiwa na mpenzi wake Calvin tena wakiwa kwenye furaha sana kwani walikua wanapiga story huku wakicheka na kuenjoy.
"Mpenzi, nilikua nasubiri utoke Kenya nije nikupe zawadi yako"
"Zawadi?? Ni nini jamani nipe basi sasa hivi hiyo zawadi."
"Unadhani nakupa mkononi?" Aliuliza Rely huku akicheka.
"Sasa unanipa wapi?"
"Ni kitu kikubwa lakini sijui utakipokeaje?"
"Zawadi ni zawadi tu mama, lazima nipokee vizuri"
"Okay, mimi ni mjamzito!"
"Una ujauzito? Ngoja kwanza una ujauzito au sijasikia vizuri??"
"Ndio nina ujauzito tena wa miezi mitatu"
"Kwahiyo una ujauzito?? Naomba usiseme ni wa yule mwanaume wako please!"
"Ni wako mpenzi wangu sio wake."
"Kweli???"
"Ndiyo."
Calvin alifurahi sana kwasababu hakua na mke hivyo alitegemea kuwa Rely ndio angekua mke wake kwasababu alitokea kumpenda sana bila kujali ni mke wa mtu. Ilikua ni furaha kwa upande wao lakini huzuni upande wangu kwasababu sikua najua Rely yupo wapi na kibaya zaidi nilishapiga simu yake sana lakini haipatikani.
Akili nyingine iliniambia kwamba Rely atakuwa kwa mpenzi wake Calvin kitu ambacho kilizidi kuniumiza kwasababu ata kama simpendi sio anifanyie vile tena kwenye nyumba yangu ni kama alikua ananionesha dharau. Niliacha kumfikiria Rely na kurudisha mawazo yangu kwa Rola nikakumbuka alivyonijibu pale tu nilipompigia simu na kutaka kujua hali yake.
Kwa upande wa Rola, nilisimuliwa na Thelesia kwamba; Baada ya masaa mawili daktari aliyekua akimtibu Rola alimfata Thelesia ambaye kwa wakati huu alikua amekaa peke yake baada ya mlinzi kurudi nyumbani.
"Dokta, vipi hali ya mgongwa??" Aliuliza Thelesia huku akiwa na wasi wasi mkubwa.
"Mgonjwa ameumia sana kichwani lakini atakua sawa kwasababu tumejitahidi kumpatia huduma inayotakiwa, kwahiyo atarudi katika hali yake ya kawaida. Labda niulize kitu tu, ilikuwaje mpaka akaanguka na kuumia vile?"
"Aliteleza tu bahati mbaya." Alidanganya kwasababu hakua anajua kitu chochote kilichotokea mpaka Rola kuwa vile.
"Aaah sawa, na vipi kuhusu uhusiano wenu, namaanisha wewe ni nani yake?"
"Mimi ni mdogo wake"
"Mnaishi peke yenu?"
"Hapana, huyu dada yangu anae mume wake ndio tunaishi nae pale nyumban"
"Aaah sawa, nimeuliza hivyo kwasababu Kwenye mwili wake kuna alama za vidole na kwa namna moja au nyingine inaonekana ni vidole vya mwanaume, sasa sijui walikua wanarumbana na mume wake kitu kilichopelekea akasukumwa labda au lah!"
"Sifahamu dokta lakini nimejaribu kumpigia mume wake simu haipatikani"
"Sawa amna shida, ngoja akiamka nitazungumza nae."
"Sawa dokta" Dokta aliondoka na kumuacha Thelesia akiwa ana mawazo, apo sasa ndio aliweza kupata picha kwamba Hussein ndio aliemsukuma Rola.
"Kwanini Rola anamganda sana huyu mwanaume?? Mwanaume mwenyewe hampendi lakin ndio amekomaa nae tu, ona sasa kamsukuma, vipi kama angekufa??" Thelesia aliwaza sanaa bila kupata jibu.
Huo ni upande wa Rola, huku kwangu mambo yalikuwa hivi; Nikiwa nimekaa kitandani nilisikia mlango ukigongwa, hivyo nilisimama na kwenda kufungua na kukutana na Rely.
"Unatoka wapi usiku huu Rely?? Huoni hali yako ilivyo na unatembea usiku kama hivi??" Niliuliza nikiwa najua fika ametoka kwa Calvin sema niliona niulize tu kwasababu ni kama vile ananionesha dharau, hawezi kuingia kwangu usiku wa saa sita kama vile yeye ndio baba wa familia wakati ata mimi mwenyewe baba wa familia saa mbili tu nilishafika nyumbani.
"Utanipisha nipite au utaendelea kuniuliza maswali yako??"
"Nataka jibu, unatoka wapi sasa hivi??"
"Nilikua nafatilia baadhi ya mizigo ambayo itaingia dukani kesho" Alidanganya.
"Ndio mpaka sasa hivi saa sita??"
"Bwana nipishe mimi, kama huamini basi ila ndio hivyo nilivyokwambia" Alinipush na kuingia ndani akiniacha pale mlangoni nikiwa na hasira sana kwani nilitamani nimshike nimchape hata kibao kimoja kirudishe akili yake lakini niliwaza nikaona sio sawa kwasababu naweza kumsababishia shida kutokana na ile hali yake ya ujauzito. Nilienda mpaka chumbani na kumkuta akiongea na sim tena akiwa mwenye furaha sana na inaonekana alikua anaongea na mwanaume, nilisubiria hadi alipomaliza kuongea na ile simu kisha nikamuuliza.
"Ulikua unaongea na nani?"
"Heee jamani! Tumeanza lini kuulizana maswali kama hayo?"
"Sijataka maelezo Rely nimekuuliza nataka unijibu, ulikua unaongea na nani???"
"Bwana eenh, niache nilale usinipigie kelele!" Alinijibu kwa dharau mpaka nilitetemeka kwa hasira na kujikuta nampiga kibao cha shavu kilichomfanya apige kelele. ITAENDELEA
.