VYOTE NDANI GONGA94
MAHABA YA MZOA TAKA 18 ππ
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Kulingana na mazingira yalivyokuwa sikutaka kumwambia palepale kuwa Grace sio mtoto wake maana ni lazima angeanzisha vulugu.
"Siwezi kukupatia mtoto Alex kaa ukijua hilo" niliongea na baadae niligeuka kwa ajili ya kuondoka ili nikaendelee na kazi zangu.
"Wewe malaya emu usiniletee utani, mwanangu lazima utanipa sitaki aishi kwako maana utamfundisha tabia za kutembea na wazoa taka na huenda ukamfundisha kutembea na vichaa kabisa" Alex aliongea.
"Wewe ata uniite malaya sawa tu ila mtoto sikupi" niliongea na kuondoka huku nikimuacha Alex akisema lazima atamchukua mtoto wake kutoka kwenye mikono yangu.
Nilikuwa na uhakika wa karibu asilimia 100% kuwa hakuwa na lengo la kuishi na mtoto ila alitaka kunikomoa tu na ndiyo maana sikuwa tayari kumpatia mwanangu na ukizingatia sio baba halisi wa mtoto.
Niliporudi nyumbani nilimweleza Damian kile kilichotokea.
"Irene ilitakiwa umwambie ukweli kuwa Grace sio mtoto wake" Damian aliongea.
"Bora ibaki kuwa siri yetu tu akijua yanaweza kuwa mengine na ukizingatia ndiyo sababu iliyonifanya anioe kipindi cha nyuma" niliongea lakini Damian hakuacha kunisisitizia kuwa nimweleze ukweli Alex.
Pia aliniambia nisije kurudiana nae tena au kumfanya nae mapenzi.
Nilimtoa wasiwasi Damian na kumwambia haitawezekana tena mimi kuwa na Alex pamoja.
"Nyie mnasemaga tu alafu baadae mnakubali kwenda kunyanduliwa huko kisiri siri" Mzoa taka hakuacha kuongea wasiwasi aliokuwa nao mbele yangu.
Basi siku iliyofata kumbe Alex alikuwa amethamilia kumchukua mtoto wangu Grace alikuja akiwa na mwenyekiti wa mtaa asubuhi hiyo na mimi mda huo nilikuwa nikijandaa kwenda kazini.
"Mwenyekiti mwanamke mwenyewe ndiyo huyu hapa hataki ata kunipa nafasi ya kuonana na mwanangu, na hataki niishi na mwanangu" Alex aliongea na mimi nilishangaa kwa maneno aliyoyasema.
Sauti ya Alex, Damian aliyekuwa ndani aliweza kuisikia nakuamua kutoka nje, ile anafika nje Alex alimwangalia kwa hasira nahisi kilichokuwa kikimtia hasira zaidi ni baada ya kugundua kuwa nilikuwa nikitoka nae kimapenzi kipindi tupo kwenye ndoa.
Mwenyekiti alinitaka nieleze kwanini sitaki kumpa nafasi Alex ya kuonana na mtoto wangu au kwenda kuishi nae.
"Mwenyekiti mimi simwamini huyu mwanaume kabisa kwenye maisha yangu na anatabia chafu sana ndiyo maana sitaki akae karibu na mwanangu" niliongea.
Kama kungekuwa na mtu mwingine ambae hatufahamu asingeweza kuamini kama mimi na Alex ni watu tuliokuwa tukiishi pamoja tena tukiwa na elimuΒ zetu za juu.
Alex alikasirika baada ya kumwambia ana tabia chafu "Nani anatabia chafu!?, mimi natabia chafu!?" Alex aliongea huku akinisogelea lakini Damian aliamua kuingilia mazungumzo yetu.
"Wewe dingi usimsogelee mke wangu" Damian au mzoa taka aliongea huku akimzuia Alex asisogee karibu yangu.
"Nani dingi!!?" Alex alimuuliza na mda huo alizidi kukasirika zaidi.
Alex alifanya kitendo cha kushitukiza kwa kunyenyua mkono wake na kumpiga ngumu ya usoni Damian ambae nae hakutaka kukubali kupigwa na Alex. wote walianza kupigana mbele ya mwenyekiti na sisi tulikuwa na kazi ya kuwaachanisha.
Nyie acheni tu ndiyo maana sipendi kuachanisha watu wakiwa wanapigani kwani kipindi namzuia Damian asiendelee kupigana nilijikuta ngumi iliyopigwa na Alex ikinipata kwenye titi langu la kushoto na kunifanya nisogee pembeni.
kihelehele cha kuendelea kuwaachanisha kiliisha na kuamua kumwangalia mwenyekiti aliyekuwa akiwaachanisha huku nikipiga kelele za kuhitaji msaada.
Baada ya mda mwenyekiti alifanikiwa kuwaachanisha na kwakuwa Damian au mzoa taka alikuwa kwenye hasira kwa wakati huo aliamua kulopoka mbele ya Alex.
"Kwanza mtoto mwenyewe sio wako ni mtoto wangu mimi" Damian aliongea na mimi niliona sasa kili kitu kinaenda kuwa wazi.
"Unasemaje wewe mjinga yani mpaka mtoto wangu unasema ni mtoto wako!? mwenyekiti unamuona huyu, nitaua mtu mimi hapa" Alex aliongea kwa sauti ya juu.
"Nani umuue!? wewe ata kukagua mtoto kama ni mtoto wako hujui huoni nafanana nae macho yule mtoto!?" Damian alizidi kuongea huku mimi nikihisi kushikwa na haja kubwa mda huo.
Alex baada ya kuona mzoa taka amekomalia kuwa ni mtoto wake alinigeukia mimi na kuniuliza.
"Wewe malaya, ni kweli huyo mtoto ni wa huyu malaya mwenzako!?" Alex aliongea na Damian alichukia kumuona akiniita malaya.
"Kuwa na adabu huwezi kumuita mama wa mtoto wangu malaya lasivyo nitakupasua hapa sasa ivi" Damian aliongea na majibizano yaliendelea mpaka pale mwenyekiti alipoamua kuingilia kati.....ITAENDELEA
Unajua nini kilitokea baada ya mwenyekiti kuingilia kati πͺπͺπͺπͺ sehemu ijayo ina majibu zaidi.
Umesoma kwa utulivu Β· dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi mahaba-ya-mzoa-taka

