PENZI LA MHALIFU 21
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA....
Cyborg alinivulisha nguo zangu nakunibeba kunipeleka bafuni kwa ajili ya kwenda kuniogesha.
Siku hiyo alitaka kunifanyia mambo ambayo hakuwahi kunifanyia tangu tumeoana.
TUENDELEA....
Cyborg aliniogesha na kunifanyia kila aina ya michezo ya kunitekenya kwa ajili ya kunipa furaha. Hiyo siku nilienjoy kuwa kwenye ndoa na Cyborg kwa kile alichokuwa akinifanyia.
Mimi na Cyborg tuliendelea kufurahi na kuogeshana pamoja lakini tukiwa tunaendelea kuogeshana nilisikia simu yangu ikiita.
Nilitaka kunyenyuka kwa ajili ya kwenda kupokea simu ila Cyborg alinizuia nakuniambia.
"Haina haja ya kwenda kuipokea hiyo simu Malaika, huu ni mda wa sisi kufurahi" Cyborg aliongea lakini moyo wangu ulikuwa ukinituma kwenda kupokea simu.
Niliamua kufata moyo wangu ulivyokuwa ukitaka, hivyo nilijitoa kwenye mikono yake nikiwa uchi na kwenda kupokea simu. Cyborg hakuacha kulalamika baada ya kumkatisha.
Mtu aliyekuwa akinipigia alikuwa ni asikari mwenzangu hivyo niliamua kuipokea.
Baada ya kupokea simu niliambiwa kuwa kuna tukio la kiharifu limetokea hivyo natakiwa niwahi haraka sehemu husika.
Sikutaka tena kuendelea kubebishana na Cyborg sababu ulikuwa ni mda wa kazi.
Nilimuaga Cyborg na kuondoka huku nikimuacha akiwa hamini kama starehe yetu ya kubebishana imekatishwa na mambo yangu ya kikazi.sikuwa na njia nyingine zaidi ya kuweka mapenzi kando kwanza kwa wakati huo.
Nilifika sehemu husika na kuwakuta asikari wenzangu wakinisubiri, haraka tulipanda kwenye gari nakuondoka kuelekea sehemu ya tukio na ilikuwa ni mida ya saa 1 jioni.
Tulifika kwenye eneo la tukio na kukuta uvamizi umeshafanyika masaa kadhaa yaliyopita huku watu wawili wakiwa wameshauliwa.
Tulichukua maelezo kwa baadhi ya raia walioshuhudia tukio hilo na walitueleza kila kitu walichokiona.
Mmoja wao alituambia kuwa watu waliovamia kwenye duka hilo walikuwa ni majambazi watatu waliokuwa na siraha.
Kazi ilibaki kwetu ya kuwatafuta wahusika na kazi hiyo nilipatiwa mimi pamoja na asikari wenzangu wawili na miongoni mwao alikuwa ni Afande Joel.
Afande Joel iliniomba tusogee pembeni kwa ajili ya kujadili pamoja jinsi tutakavyowakamata watuhumiwa. sikutaka kukataa nilikubali na tulianza kufanya maongezi.
Maongezi yetu yalichukua mda mrefu, ilifika saa 4 usiku na tulikuwa bado tupo kwenye majadiliano, baadae niliamua kumuaga Afande Joel ili nielekee nyumbani na kwakuwa alikuwa na usafiri wake aliamua kunipakiza kwa ajili ya kunipeleka kwangu.
Sikutaka kukataa na ukizingatia alikuwa ni Asikari mwenzangu, hivyo tuliongozana moja kwa moja mpaka sehemu niliyokuwa nikiishi.
Tulifika na Afande Joel alitaka kuondoka bira ya kuingia ndani ila nilimzuia kwani nilitaka kwenda kumtambulisha kwa mme wangu Cyborg.
Mimi na Afande Joel tuliingia huku tukiwa tumeongozana mpaka ndani na Cyborg alishangaa kuniona nikiwa nimeongozana na Asikari mwenzangu tena mwenye jinsia ya kiume.
Nilimtambulisha mme wangu kwa Afande Joel aliyefurahi kumuona ila ilikuwa tofauti kwa Cyborg kwani hakuwa na furaha baada ya kumuona Afande Joel nyumbani kwetu.
Baada ya utambulisho Afande Joel hakutaka kukaa sana kwani alituaga na kuondoka.
Ilibidi nimuulize Cyborg maana hakuwa na furaha baada ya mimi kusindikizwa na Afande Joel.
"Mme wangu kuna tatizo gani!?"
Baada ya mimi kumuuliza Cyborg hakutaka kuficha kile kilichokuwa kwenye moyo wake.
"Tatizo lipo yani ata mwaka haujamaliza kwenye kituo chako cha kazi ila tayari umeshapata rafiki wa kiume mpya Malaika? na wasi wasi kabisa huyo Afande anavyoonekana anapenda sana wanawake" Cyborg aliongea na mimi nilijua ni wivu wake wa mapenzi ndiyo uliokuwa ukimsumbua.
Niliamua kumwelewesha vizuri na kumsihi asihisi mambo mengine kwani mimi na Afande Joel tunaukaribu wa kikazi zaidi hivyo haina haja ya yeye kuwa na wasiwasi na mimi.
Cyborg alienda mbali na kiniuliza ni kazi gani hiyo iliyotufanya mpaka tukaongozana pamoja.
Sikutaka kumficha zaidi ya kumweleza kazi niliyopewa mimi pamoja na Asikari wenzangu.
kiukweli nilikuwa sina idea ya wapi pakuanzia ili niweze kuifanikisha kazi tuliyopewa na Cyborg baadae aliamua kuniambia kuwa atanisaidia kuifanya hiyo kazi.
"Unasema kweli Kelvin!? huoni kama utaingia matatizoni!?" ilibidi nimuulize baada ya kusema yupo tayari kuifanya kazi yangu.
"Kwani umesahau kuwa niliwahi kuwa mharifu na mtu hatari kabra sijakuoa wewe!?"
"Hapana sijasahau"
"Basi niachie mimi nitajua pakuanzia ninachotaka sitaki kuona asikari mwenzako hasa uliyekuja nae anajipendekeza kwako kwa ajili ya kukusaidia kazi sababu najua baadae lazima ataomba sex kutoka kwako"
Jamani kuna wanaume wenye wivu na mmoja wao ni Cyborg yani alikuwa hataki kabisa kuniona nikitengeneza urafiki na mwanaume yoyote yule, tatizo la Cyborg wangu lilikuwa hilo.
Baada ya Cyborg kuniambia ataifanya kazi kwa ajili ya kuzuia Asikari wa kiume wasitengeneze mazoea na mimi nilielewa ni wivu wa mapenzi aliokuwa nao kwangu na ndiyo uliomfanya Cyborg awe tayari kunisaidia kazi niliyokuwa nimepewa.Upande mwingine nilijua anatania.
Siku hiyo ilipita. ilivyofika asubuhi kama kawaida ya Cyborg hawezi kuacha kufanya sex asubuhi, nilimpa cha asubuhi na baadae aliniuliza sehemu lilipotokea tukio.
"Ina maana kumbe umedhamilia kupeleleza ni wapi walipo hao magaidi!?" nilimuuliza.
"Wewe niambie Malaika ili nikafanye yangu sitaki kuona kabisa ukiwa karibu na Afande Joel" Cyborg aliniambia kwa msisitizo na mimi nilijisemea kama kuolewa kweli nimeolewa, niliamua kumwambia na kumwelekeza sehemu lilipotokea tukio.
Cyborg aliondoka kwa ajili ya kwenda kufatilia.......ITAENDELEA..