PENZI LA KULAZIMISHA (Mafia Na Wakili)*
*1---2*
*__________________________________________*
*SEHEMU YA KWANZA*
Carina ni binti wa miaka 25 , ni binti aliebarikiwa kuwa na akili sana anatoka katika familia ya watoto 5 yeye akiwa mtoto wa pili. Bwana na bibi Abdu ndio wazazi wake wa kumzaa.
Familia yao ilikuwa ni familia ya kawaida sana lakini wazazi wao walijitahidi sana kuwapambania kwenye swala la elimu . Licha ya wazazi kupambana lakini watoto wawili ndio walifanikiwa kushikamana na elimu.
Dada yao mkubwa Safina aliishia kidato cha pili akaishia kubeba mimba na sasa yupo kwa mume, carina amefanikiwa kuhitimu chuo cha sheria, Ibrahim yeye alikuwa mtoro shuleni kutokana na jitihada za wazazi alijitahidi sana akaishia darasa la saba na sasa hayupo nyumbani inasemekana alizamia huko africa kusini, zamda ni mama nitilie na Halfan yupo kidato cha tano.
Kutokana na maisha yao kuwa chini baba yao alifanya kazi yoyote kuhakikisha kuwa Halfani anasoma na kuhitimu masomo yake ,watu walimzarau sana baba yao kutokana na kuwa na kipato kidogo na maisha yao kuwa ya kubangaiza
" Siku moja carina alikuwa anatoka kwenye mihangaiko yake akapita sehemu akamuona baba yake akiwa anafanyishwa kazi ya kubeba mizigo kwenye nyumba ya muhindi mmoja na kutumwa kama mtoto mdogo tena huku akifokewa. Carina aliumizwa sana na ile hali ya baba yake kutumikishwa alitaka kuondoka ili baba yake asimuone maana alihisi huenda akimuona atajisikia vibaya. Lakini kwa bahati mbaya akiwa anaondoka baba yake aliangalia sehemu alipo na kufanya waangaliane, baba yake alionyesha kushituka lakini carina aligeuza macho yake haraka akaondoka akarudi nyumbani huku moyo wake ukiwa unasononeka kwa kile alichokiona hakujua kama baba yake anatumikiahwa vile kila siku aliaga anaenda kazini akajua anafanya kazi ya maana kumbe ilikuwa ni tofauti na ahavyofikiria.
" Weeee Mungu wangu nitoe nguvu kwenye hili mbona maumivu yake kama nashindwa kuvumilia. MUNGU wangu mfanyie wepesi baba yangu mpe rizki maana anayopitia kwa ule umri hastahili . MUNGU nisaidie nipate kazi niikomboe familia yangu.
Carina aliomba MUNGU amfanyie wepesi kwenye kutafuta kazi ili asaidie familia yake. Siku hiyo alishinda akiwa hana furaha .
Jioni akiwa amekaa nje anapanga na kupangua , akiwaza na kuwazua mara baba yake alirudi kutoka kibaruani kwake.
" Shikamoo baba.
" Marahaba.
" Baba tunaweza kuongea? Carina alimuomba baba yake,
Baba yake alisogea alipokuwa amekaa na kukaa pembeni yake.
" Baba ile ndio kazi unayofanya?
Carina aliuliza na baba yake akatulia kwa sekunde kadhaa kisha akajibu.
" Carina binti yangu sina kazi ya maana ninayofanya ,ninafanya kazi kama zile kwaajili yenu wangu.....
" Lakini ile ni kazi ya kudhalilisha haifai ufanye ile kazi baba.
" Nikiacha mtaishi je ? Unajua hakuna mwenye kipato kikubwa kati yenu, Halfani bado yupo shule ananitegemea, wewe bado haujabahatika kupata kazi unanitegemea mimi unafikiri nilikaa hapa ndani maisha yataendaje?
Carina alionekana kuhuzunika sana .
" Mwanangu usihuzunike pia naomba usiwaambie wenzio kuwa umenikuta nafanya kazi kama ile, sitaki mtu yoyote ajue.
Machozi yalimtoka alijifuta kisha akasema.
" Usijali baba yangu ipo siku nitakuheshimisha.
Baba yake carina alitoa tabasamu na kusema
" Asante mwanangu. Kwa wakati huu mimi kunyanyuka na kusema niwe na kipato kikubwa ni ngumu sana ila naamini utaniheshimisha binti yangu.
Kesho yake carina aliamka mapema sana akiwa na bahasha ya vyeti vyake alizunguka kwenye kampuni nyingi za wanasheria kwaajili ya kuomba kazi lakini kwa siku hiyo ilikuwa ngumu sana kupata ila kwenye kampuni moja aliambiwa aache namba za simu na kuambiwa azatafutwa.
Carina alirudi nyumbani akiwa kachoka sana lakini bado hakukata tamaa kwani alipokuwa anakumbuka jinsi baba yake alivyokuwa akidhalilika alipata machungu hakupata nguvu ya kuendelea kutafuta kazi.
Baada ya wiki moja kupita carina alipigiwa simu na mtu ambae hakufahamu.
" Hallow , habari yako carina.
" Salama.
" Unaongea na mwanasheria mwafongo sijui unanikumbuka?
" Ndio nakukumbuka.
" Leo unaweza kufika ofisini kwangu?
" Bila shaka nitafika. Muda na saa utakayotaka.
" Basi njoo sasa kuna jambo muhimu sana tunatakiwa kuongea bila kuchelewa wala kupoteza muda.
" Sawa.
Baada ya kukata simu carina akijiandaa haraka na kuelekea ofisini kwa mwanasheria mwafongo.
" Afadhali umefika mapema, karibu ukae.
Carina valivutavkiti akakaa na kusikiliza wito.
" Carina nikiangalia cv zako ziko vizuri sana sasa nimeongea na rafiki yangu Patrick ni mwanasheria mkubwa sana pia ana kampuni kubwa anakuhitaji kwenye kampuni yake.
Hatuna alivyosikia hivyo alifurahi sana .
" Ina maana nimepata kazi?
" Ndio na kama upo tayari basi kesho unatakiwa kuondoka uelekee Arusha.
" Sawa nipo tayari , mimi nitaenda popote ilimradi nipate kazi tu.
" Basi ngoja tuwasiliane .
Mwalongo alipiga simu na muda uleule Patrick alipokea simu wakaongea na carina makubaliano ilikuwa kesho yake carina apande gari kuelekea Arusha .
Carina aliondoka ofisini kwa Mwafongo na kwenda kufanya maandalizi ya safari maana pale alipo hakuwa hata na nauli ya kumfikisha Arusha . Alienda kwa watu wake wa karibu na kukopa huku akiahidi kulipa baada ya kupokea mshahara wake wa kwanza.
Carina alifika Arusha na kuanza kazi mara moja na mshahara wake wa kwanza hakuweza kufanyia kitu alilipa madeni na kiasi kidogo alituma nyumbani kwao.
Baada ya mwezi mmoja kupita carina alikabidhiwa kusimamia kesi ya mteja . Kwa mara ya kwanza Carina alisimama mahakamani kumtetea mteja na mambo yanaenda vizuri wakashindwa kesi. Pongezi zilikuwa nyingi kutoka kwa boss na wafanyakazi wengine.
Kutoka na kujiamini kwake Carina alifanya kazi nzuri sana na kuzidi kuipa jina kampuni yao na kufanya watu wengi kwenda kutafuta wanasheria kwaajili ya kusimamia kesi zao.
Siku moja wafanya kazi wote wakiwa kwenye majukumu Patrick alitoka ofisini kwake akiwa kaongozana na wanaume wawili.
" Jamani naomba tusikilizane kuna kesi ipo hapa mezani. Ni kesi ya mauwaji mshitakiwa ni Jofrey mosses almaarufu Tigger.
Wafanyakazi wote waligeuka kuangaliana maana huyo mtu aliyetajwa ni mtuhumiwa sugu mafia hatari. Hakuna aliejibu kama anaweza kusimamia hiyo kesi.
" Advocate Patrick hili swala unatakiwa kusimamia wewe hapa sijaona wa kusimamia kesi ya Tigger. Alisema mwanaume mmoja .
" Nina kesi nyingi hii itakuwa nzito kwangu ila kuna vijana wangu hawaamini sana.
" Mbona wapo kimya hakuna anaejibu?
Mara wakasikia
" Mimi nitasimamia hiyo kesi. Ilikuwa ni sauti kutoka kwa carina.
*SEHEMU YA PILI*
Kila mtu aligeuka kumuangalia Carina kwa mshangao lakini advocate Patrick aliachia tabasamu sababu alitaka carina asimamie hiyo kesi kutokana na kujituma kwake na kujituma kwenye kazi yake.
" Advocate huyu binti ataweza kweli? Aliuliza Erick mtu wa karibu sana na Tigger.
" Msijali huyu binti mbali na elimu yake ya sheria pia ana kipaji kizuri sana kwenye kusimamia kesi acha tumpe nafasi asimamie hili.
Erick alimuangalia sana carina ambae alionyesha kujiamini mno kisha akamgeukia mwenzie ambae alionyesha kuwa na wasiwasi.
Patrick aliona wasiwasi wao alimshika bega Erick alafu akasema
" Erick niamini mimi hilo swala litaenda vizuri anaposema Carina ni sawa nimesimama mimi .
" Sawa lakini asije akatuangusha si unajua Tigger?
" Nimesema ondoeni hofu nitashirikiana na carina na kila kitu kinaenda sawa.
" Kama Tigger atafanikiwa kutoka basi atapata milioni mbili kama shukurani.
Patrick alitabasamu kisha akasema
" Andaeni hiyo hela.
Wale watu walilidhika wakaondoka.
Huko nyuma gumzo liliibuka ofisini.
" Carina hivi unamfahamu huyo kutuhumiwa mwenyewe?
" Simfahamu
" Mmmh
" Ndio maana umekubali kirahisi kama ungekuwa unamfahamu usingekubali.
" Kwanini. Kwani ana shida gani?
" Huyo mtu ukimuona yupo tofauti na matendo yake. Kwanza fikiria hilo jina lake Tigger.
" Mbona hamalizi kunielezea mnaishia katikati nipeni maelezo ya kutosha.
" Hapana tusikukatushe tamaa nenda kakutane na mteja wako mr tigger muyajenge .
Carina aliona kama wanamtisha akuwapuuzia akaendelea na mambo yake.
Kesho yake majira ya saa tano asubuhi carina alienda magereza kuonana na Tigger.
Carina alikutana na wahusika na kujitambulisha kama wakili mpya wa Tigger baada ya hapo alipelekwa kwenye chumba maalumu kwaajili ya kukutana na Tigger.
Baada ya dakika chache Tigger alifika na kukaa kwenye kiti huku akimuangalia carina kwa makini. Wakati huo carina nae alikuwa akimuangalia kwani hakuamini kama huyo Tigger anaeongelewa kwa matukio makubwa ndio yule aliyekaa mbele yake.
Tigger alikuwa ni kijana mwenye umri kati ya miaka 35 na usoni alionekana ni mtu mstaarabu sana na sura yake ilikuwa ya kuvutia , alikuwa mkimnya sio mtu wa maneno mengi.
Baada ya kuangaliana kwa muda Carina aliamua kumsalimia na kujitambulisha.
" Habari , naitwa carina Abdu ni mwanasheria wako mpya. Aliongea Carina huku akimpa mkono Tigger lakini Tigger hakuangaika kutoa mkono wake alimuangalia tu.
Carina alirudisha mkono wake na kuendelea kuongea.
" Naomba unipe ushirikiano.
" Unataka ushirikiano gani?
" Unaweza kuniambia siku ya tukio ilikuwaje mpaka kukamatwa kwako?
Tigger bado alimuangalia tu bila kujibu swali aliloulizwa.
" Ongea ukweli wote maana ukweli wako ndio utakuwa mwanzo mzuri wa mimi kujua wapi nianzie.
Safari hii Tigger alitoa kicheko kidogo huku akipapasa kichwa chake alafu akasema.
" Kweli hawa watu wamenichoka yani safari hii wameamua kunileta mchumba . Wewe unaweza kweli kusimamia kesi yangu?
Carina hakupenda kauli ya Tigger .
" Kumbuka mimi ni mwanasheria nipo hapa kwaajili ya kukusaidia kuhusu hiyo kesi yako.
" Mmmmh wameshindwa mawakili wakubwa wanaume wenye ndevu zao wewe mchumba utaweza nini au unataka niozee gerezani kwa kosa ambalo bila kijinga?
Carina alishikwa na hasira kutokana na zarau anazoonyeshwa na Tigger .
" Huyu mpuuzi ananichukulia poa hajui kuwa naweza kuisimamia kesi yake na akawa huru sasa ngoja nimuonyeshe kuwa mimi naweza .
" Unafikiria nini ? Tigger waliuliza baada ya kuona carina yupo mbali kimawazo.
" Nahitaji kusikia neno kutoka kwako.
" Sina cha kusema ni bora uende ukampikie bwana ako na sio kupoteza muda hapa.
Alisema Tigger kisha akasimama na kuondoka huku Carina akiwa anamsindikiza kwa macho.
" Hivi kitu lenye dharau hivi tutaweza na kweli? Acha niondoke kwanza ila nitarudi tena.
Carina alikusanya vitu vyake akaondoka na kurudi ofisini. Alienda moja kwa moja ofisini kwa advocate Patrick.
" Vipi Carina umefanikiwa kuongea nae?
" Nimeona nae lakini sijafanikiwa kuongea nae kitu cha maana.
" Kwanini?
" Yule mtu ni jeuri sana ana dharau sana anahisi siwezi kusimamia kesi yake kutokana na jinsia yangu pamoja na muonekano wangu. Nadhani hii kesi ungesimamia wewe.
" Mmmh Tigger hana ujanja hakuna wa kusimamia kesi yake wewe ndio utakuwa wakili wake.
" Lakini hanipi ushirikiano wowote.
" Usijali kuhusu hilo kila kitu kitakuwa sawa na utafanya kazi yako.
Full 1000
Whatsp 0784468229.