NILIMDANGANYA MKE WANGU NIMEFUKUZWA KAZI KUMBE NNALIKIZO MIEZI 3
Sehemu ya 04&05
Nilikaa kule chooni nilijihisi kuharisha ila sikuwa na haja kubwa,
Nilikaa kwenye sinki la choo nikijiinamia huku nikijilaumu ,maana kama mke nikweli nampenda tena sio kidogo yaani nampenda sana tu , moyo uliniuma sana huku nikijiambia nimefanya kosa kubwa sana kumdanganya mke wangu , nikawaza labda nimwambie ukweli anaweza akatulia na mapenzi yakarudi kama zamani ,lakini upande mwingine nikawaza kuwa hata nikimwambia hawezi kubadilisha msimamo wake , nilikaa kule chooni nikaona mke wangu kanyamaza lakini kama anapilika pilika nyingine , nikaona ngoja nitoke nimuone anafanya nini , nikashangaa anahamisha nguo zake anapeleka chumba cha mtoto, nikakaa zangu kwenye kochi nikimwangalia ,alikuwa anakusanya nguo pamoja na vitu vyake vingine huku anasema ,, yaani mi natoa pesa mtu anakula anajaza choo halafu et ananipiga ,? Yaani mi niwakupigwa kweli ,? Yaani pesa nitafute mimi bili za maji nilipe mimi umeme nilipe mimi na kuna lijitu limekalisha makende yake tu linakula linavaa lisijue hata pesa ya dawa yamswaki , halafu ananipiga mimi , mke wangu aliongea hivyo mpaka anamaliza kukusanya vitu vyake akavipeleka chumba cha watoto na kuubana mlango , ukweli niliumia San na nilipata shida Sana nilihisi moyo unakufa ganzi yaani sijui nikwambieje kwa jinsi niliyokuwa najiskia , msomaji nakwambia kweli achana na vitu vyote ila mapenzi yanasiri kubwa sana we fikilia mi nilikuwa naumia lakini sikujua naumia wapi yaani nahisi maumivu tu ,
Niliingia chumbani kwangu nikaona chumba cheupe ,nikachoka nikakaa kwenye kitanda nikijiinamia , nimeyataka mwenyewe haya ,nilijisemea ,nilijilaza nikapitiwa na usingizi ,
Asubuhi nikaamka na nikamuona mke wangu anajiandaa kuondoka kwenda dukani kwake , nikamsalimia hakuitika ikabidi nimwambie mke wangu nakusalimia , akanijibu kwani salamu lazima ? Halafu usiniite mkeo ,kuanzia sasa tumeshaachana na tumeshagawana vyumba na sitaki maelezo mengine , kama ukiona nakukera unaweza kuhama nyumba au mi nihame nikuachie nyumba , aliongea hivyo akaondoka zake na hakuacha pesa ya chakula , maana kila akiondoka lazima aache mezani elfu Tano lakini siku hiyo hajaacha , hiyo haikuniuma sana kwa vile pesa ninazo japo yeye alijua ananikomoa ,
Nilimwandaa mwanangu na nikampeleka shule ,nikapitia kule kwenye nyumba yangu nikakutana na wale mafundi wakaniambia inabidi kesho tuendelee na kazi kwani tofari zimeshakauka , nikawajibu sawa ,tukapanga mipango mingine ikiwemo lenta na plasta ,pamoja na sinki la choo ,niliamua kuifanya nyumba hiyo kuwa yakisasa ,yaani nyumba nindogo inavyumba vitatu na sebule na jiko ,Yani ilikuwa na muonekano mzuri kweli ,
Nilipotoka kule site nikaamua nipitie kule kazini kwetu TAZARA, wafanyakazi wenzangu walifurahi sana kuniona na tukapiga story Sana , nikatoka nikarudi zangu nyumbani ,nikamkuta mwanangu karudi shule ,sikupika nikamnunulia chips na soda akala nikamfundisha baadhi ya maswali yake na siku ikaishia hivyo ,
Usiku mke wangu hakurudi nilimsubilia mpaka saa sita usiku nikaamua kupiga simu yake , simu iliita na haikupokelewa nikaingiwa na wasiwasi labda anatatizo nikapiga kama mala tatu ikapokelewa lakini hakuongea ila nilisikia miguno yaani kama watu wanafanya mapenzi ,
Nikahisi labda nasikia vibaya ,nikaita haloow ,sim ikakatwa , mwenzenu nilichanganyikiwa , nikapiga tena simu ikakatwa nikapiga tena ikawa haipatikani kabisa , nikaendelea kupiga tena natena lakini haikupatikana , nikajiuliza si alipokea nikasikia kama sauti ya mke wangu tena nikama anafanya mapenzi ,maana alikuwa anaguna kabisa tena kama analalamika kabisa ,au sio yeye ,?
Sikutaka kuamini ,unajua kama unampenda mtu Sana hata kama anafanya baya basi wewe utalitafutia sababu liwe zuri, sasa ndivyo ilivyokuwa kwangu sikutaka kuamini kama mke wangu anafanya mapenzi ,
Nilikaa macho mpaka asubuhi yaani Acheni tu mapenzi yaitwa mapenzi ,
Nilimwandaa mtoto wangu huku mtoto nae akiniongezea machungu kwa kuniuliza mama yupo wapi ,nikamjibu tu yupo kazini ila atarudi ,
Nilimpeleka mtoto shule kisha nikapitia kule site na kuwaachia mafundi pesa za matirio na kwenda mpaka dukani kwa mke wangu , nilifika lakini cha ajabu duka limefungwa , ikabidi niwaulize wadada wapale duka la pembeni wakaniambia amefunga tokea jana saa kumi alikuja kuchukuliwa na mumewe , nikastuka nikawauliza mumewe yupi ,?
Wakaniambia mumewe ye ndo alivyotutambulisha na mbona anakujaga hapa kila siku anagari dogo jeusi , yule dada aliniambia bila hata wasi wasi ,wakati mimi nilihisi kama mkojo unataka kutoka , nikamwambia sawa asanteni, nikaondoka ,bila hata kuaga ,
Sikwenda kule site nilirudi nyumbani na kwa vile Niko peke yangu nyumba nzima nilijifungia ndani nikalia , tena nililia kwa sauti kama mtu anamsiba , Acheni kabisa mapenzi yanaumiza ,
Usiku mida ya saa 4 mke wangu alirudi aisee huwezi amini nilipiga goti na kumuomba msamaha ,nikamwambia mke wangu naomba unisamehe nateseka , tuishi Kama zamani ,usiniache , niliongea huku machozi yananitoka , lakini mke wangu hakunijali aliingia chumbani kwa mtoto na kufunga mlango ,nikabaki pale mlangoni nimepiga magoti, mule ndani alikaa kama dakika 10 akatoka alikuwa kabadilisha nguo na viatu , akawa anatoka alifungua mlango nikamuwahi nikamshika mkono na kumwambia mke wangu usiende plz bado nakupenda tena sana tu, nikasikia honi kumbe mke wangu aliletwa na gari tena Rav4 New model, nyeusi nikajisemea huyu ndo yule jamaa walikuwa wanamzungumzia wale wasichana ,
Kwani we unashida gani we si tulishaachana ,? Mke wangu alisema hivyo huku akipanda kwenye gari , nikamfuata dereva wa hilo gar alikuwa ni kijana wa makamo yangu sema yeye alikuwa bishoo maana alivaa nguo za ujana ujana na macheni cheni shingoni ,
Nikamwambia yule jamaa plz huyu ni mke wangu na nampenda sana naomba uniachie mke wangu bado nampenda sana ,niliongea huku nalia , yule jamaa alicheka na kuondoa gari,
Sijui yule mwanamke alinipa nini maana kama kumpenda tu nilimpenda sana tu , nilijikuta nakaa chini huku nalia ,
Nini kitaendelea usikose MUENDELEZO
NILIMDANGANYA MKE WANGU NIMEFUKUZWA KAZI KUMBE NNALIKIZO MIEZI 3
SEHEMU YA 05
Sijui yule mwanamke alinipa nini maana kama kumpenda tu nilimpenda sana tu,
Nilikaa pale chini huku nalia,
Huwezi amini lakini nakwambia kweli mapenzi yanauma tena usimlamu mtu akinywa sumu au akijinyonga kwa ajili ya mapenzi ,
Nilikaa pale chini kama lisaa lizima huku nikijipa moyo kuwa mke wangu atakuja tu tena muda sio mrefu , nilipoona mmbu wananing'ata na Sion mke wangu akirudi nikaingia ndani nikapitia mpaka chumba cha mwanangu, nilikaa pale kitandani kwa mtoto wangu huku nalia ,nilimwangalia mwanangu nikamkumbatia japo alikuwa kalala na mimi nikapitiwa na usingizi ,
Mke wangu alirudi ilikuwa ni kama saa kumi namoja kasoro, ya usiku , akaniamsha kwa kunistua , tena akaniambia we mpuuzi kwanini hukufunga milango ,? Nikakumbuka nikweli nilisahau kufunga milango yaani jana nilipoingia ndani nilisahau kufunga mlango hata mmoja mpaka nikapitiwa na usingizi,
Vitu vyote vimeibiwa we umekalisha tu ,hebu amka huko uwende sebuleni , mke wangu aliniambia kwa ukali , na nilijikuta naamka tu na kwenda sebuleni, heeh nikashangaa sebule ilikuwa nyeupe ,yaani wameiba TV ,Redio , meza sofa seti yaani nikama mtu amehama , nikakumbuka chumbani kuna pesa kwenye kabati nikakimbilia chumbani kwangu , kwa bahati nikazikuta , nikashusha punzi ndefu nikapumua nikawaza hivi nikweli nilikuwa sijafunga milango ? Sasa hawa waizi wamekuja na pikap au ? Na kwanini wameiba vitu vya sebule tu ? Maana hata chumbani kwangu kulikuwa wazi na hakujaguswa hata kitu, nikarudi chumbani kwa mke wangu nikamkuta kalala tena hana hata presha , nikarudi sebuleni huku natafakari jinsi kulivyoibiwa pale ndani ,
Nikaamua nifunge milango tu nikaenda kulala , asubuhi niliamka nikaenda chumbani kwa mwanangu ili nimwandae kwa ajili ya shule ,nikamkuta mke wangu bado kalala , nikamwamsha mtoto na kumuandaa kisha nikampakiza kwenye gari lashule , nikarudi nyumbani nikaandaa chai maana niliona mke wangu hana dalili ya kwenda kazini ,mke wangu akaamka kwenye muda wa saa tatu na akaenda bafuni kaoga kisha akachukua nguo zake akaanza kufua , nikamfuata na kumwambia mke wangu chai tayari ,akanijibu we pesa umetoa wapi ? Kabla sijamjibu akaanza kufoka niliweka pesa kwenye mkoba wangu sizioni kwanini unakuwa mwizi wewe ,? Kama huna pesa si uwende ukabebe zege kule na wanaume ,? Nikamjibu mke wangu mimi sikuchukua pesa zako , akaniambia sasa hizo pesa umezitoa wapi za kupika chai na machapati yako ,au umeshakuwa shoga ,? Wanakugeuza eee ?? Nilikasirika nikataka kumpa bonge lakof lakini nikasita , hebu nipige uone kama hujaenda kunyea debe , aliniambia mke wangu ,nilirudi chumbani kwangu na hata chai haikunyweka tena ,
Nilikaa kule chumbani mpaka mke wangu alipomaliza kufua na akajiandaa akaondoka bila ya kuniaga , nikajua lazima atakuwa kaenda kazini ,
Namimi nikajiandaa ili niende kule kwenye nyumba yangu ninayojenga , niwe mkweli tu hii nyumba nilikuwa naijenga tu lakini sina furaha ,kumbuka hii nyumba nilikuwa naijenga ili nije nimpe mke wangu kama angeweza kunivumilia , lakini yametokea yakutokea ,mafundi walikuwa wanafunga lenta na wakaniambia niweke oda kabisa ya madirisha na milango maana baada ya wiki mbili watapauwa , mpaka hapo imekatika miezi miwili ,
Nikasema sawa nikaenda kutoa oda na mafund wakafika kwa ajili ya kupima madirisha na milango ,
Muda kama saa kumi nikasema ngoja nipitie dukani kwa mke wangu kisha nirudi nyumbani ,
Nilifika na nikakuta kweli kafungua na duka limejaa si mchezo yaani vipodozi vya ainazote na kaweka mpaka mawigi ,wiving na Rasta za kila aina , na anawafanyakazi wawili pale dukani ,
Nilifika lakini kabla hata sijasalimia mke wangu akatoka na kunivuta pembeni, akaniambia naomba uondoke eneo hili usinitie aibu sahii , hee nikashangaa na kumuuliza aibu ya nini tena ,? Akaniambia inamaana we hujioni ? Hebu jiangalie wewe na mimi halafu utaanza kuwaambia watu mimi nimkeo huoni utanitia aibu , ? Nikamwambia lakini mke wangu ,,,, ,,,
Weeeee koma ishia hapo hapo mi sio mkeo na ndo kitu nnachokikataa hapa naomba uondoke ,
Dada vipi tena kulikoni , alikuja kijana mmoja na kuuliza , mke wangu akajibu si huyu tapeli hapa anataka kunitapel , hee nikashangaa na kumuuliza mke wangu yaani mimi tapeli ??
Nikaona watu wameanza kusogea , yule kijana akanikunja , na kunisukumia ukutani , mi mwenyewe hata kupigana sijui masikini nilijikuta naanguka mzima mzima ,
Potea hapa watu wasije wakakuchoma moto tapel wewe ,mke wangu alisema na mimi kweli nikajikusanya pale chini na kuondoka mdogo mdogo,
Nilitembea huku kichwa kimeelemewa na mawazo , yaani mke wangu ananiita mimi tapeli duh , sikumbuki hata ilikuwaje ila nilikunywa pombe sana siku hiyo nilirudi nyumbani huku mvua inanyesha na sikujali mvua , yaani nililowana na sikuona kama kuna mvua , nilifika nyumbani nayumba yumba , lakini kabla hata sijafungua mlango nikamuona mwanangu kajikunyata pembeni ya ukuta ,mvua inamnyeshea kajiinamia na begi lake lashule kalikumbatia huku analia , aisee pombe ilikata ,
Nini kitaendelea tuonane mtaji wetu ni koment tu mpaka mwisho ,
ITAENDELEA.