Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  artist

NILIMDANGANYA MKE WANGU NIMEFUKUZWA KAZI KUMBE NNALIKIZO MIEZI 3 SEHEMU YA 11&12

1st Jun, 2025 Views 31

NILIMDANGANYA MKE WANGU NIMEFUKUZWA KAZI KUMBE NNALIKIZO MIEZI 3

SEHEMU YA 11&12

Nilinyanyua shoka nikataka kumpiga nalo yule jamaa , yule jamaa akalidaka lile shoka na kunipokonya halafu akanisukuma nikaanguka pembeni, mke wangu akawa anacheka tu na kusema mtu mwenyewe huna nguvu halafu unataka kupigana hahahaaa, nilikasirika nikanyanyua jiwe yule jamaa akaniwahi na kunizaba makofi akanipokonya jiwe na kulitupa ,niliumia sana kwani nilikuwa nanyanyasika mbele ya mke wangu halafu mke wangu anacheka tu,
Nikaingia ndani huku nimejiinamia tu maana ingekuwa mchana watu wangeniona sijui ingekuwaje , lakini sikufika ndani nikajiona mjinga kuingia na kumuacha mke wangu nje tena akiwa na mwanaume mwingine , nikatoka tena nje nakumwambia mke wangu plz nakuomba usinifanyie hivyo plz , mke wangu akajibu kwani mi nimekufanyaje ,? Mi nawewe tulishaachana na talaka umeandika sasa mbona tunafuatana ,? Kwanza wewe si unamalaya zako wenye magari si uwafuate ,mke wangu bado aliniuliza huku akinikejeli akamkumbatia yule jamaa yake na kupeana mabusu mbele yangu ,
Nilihisi moyo unapasuka ikabidi nijiegemeze kwenye ukuta , nilimuona mke wangu mkatili sana maana mbele yangu ananyonywa mate na mwanaume mwingine , nikaingia ndani tena chumbani kwangu nikajifunika shuka nikalia sana nilimlaumu mungu kwa kumwambia kwanini unaruhusu niumie ,nililia sana na Nakumbuka siku hiyo usiku sijui saa ngapi nilihisi miguno ya mapenzi chumbani anakolala mke wangu yaani kwamala nyingine mke wangu aliingiza yule mwanaume ndani na wanafanya mapenzi , nikasikiliza kwa makini nikamsikia mke wangu anamsifu yule jamaa kwa kumpa penzi tamu kuliko mimi , nilitoka chumbani nikaenda kugonga mlango kwa nguvu huku nikimwambia mke wangu, nilikudanganya tu kuwa nimefukuzwa kazi ili nione uvumilivu wako ,lakini umenilipa maumivu makali sana , basi nakuomba usiendelee kuniumiza , nilimwambia mke wangu huku nikigonga mlango , ni kama mke wangu alifanya kusudi ili niumie maana hakujali nnavyosema ndo kwanza alizidisha kelele za mapenzi huku akimsifu jamaa ,
Nilirudi chumbani kwangu na nikaweka manguo kichwani nisisikie kelele zao , nilijiuliza huyu mwanamke nimempendea nini au alikuwa hanipendi alikuwa anaishi namimi ilimradi tu,
Walimaliza kufanya yao nikashangaa mke wangu anakuja chumbani kwangu nakuanza kuniambia ,sitaki usumbufu ninapokuwa kwenye starehe zangu sawa ,? Naona unachanganyikiwa kila siku maneno ni hayo hayo tu eti umenidanganya eti hujafukuzwa kazi wakati mwezi wa pili huu unaenda watatu umekalisha makende yako tu ndani ,tena sipendi kabisa unifatefate subilia siku zako za kuishi hapa ziishe uondoke zako usinichoshe kabisa ,aliongea mke wangu na hakunipa hata nafasi ya kujibu akaondoka zake ,
Asubuhi niliamka nikamuona mke wangu anamuandaa mtoto kwa ajili ya shule huku akipika maziwa na chapat , nikajisemea ngoja leo Nile chakula cha mke wangu nikamimina maziwa kwenye kikombe na kuchukua chapati kama mbili, mke wangu alikuja mbio akanipokonya na kuniambia we huoni aibu yaani mwanaume mwenzako atoe pesa apikiwe we uje ule hebu achiaaa , aliongea mke wangu huku akinipokonya yale maziwa na chapati , nikamuuliza inamaana huyo mwanaume yupo ndani ,? Akanijibu ndio , tena alinijibu kwa dharau huku anaondoka , nilikaa nimejiinamia tu nisijue la kufanya , wakati wanaendelea kunywa maziwa yao na machapati nikasikia kelele huko nje nilipotoka nikashangaa kuona wafanyakazi wenzangu tena wakiwa na bosi wangu , wakishangilia huku wananiita jina langu , nilishangaa sana bosi wangu alishuka nakuniambia aisee tumekustukiza lakini ndio sapraiz yenyewe huu ufunguo wa gari yako hiyo hapo na utaitumia kuja nayo kazini tumekuletea mapema ili uizoee , daah aisee ilikuwa ni V8 New model ile ya wabunge , sikuamini nilifurahi sana sasa wakati naikagua ile gari mke wangu si akatoka nje wafanyakazi wote wakashangilia na kuimba sheeemu shemu ,,, shemuuuuu ,,! Shemu huyo shemuuu shemu huyo shemuuu shemu huyo shemuuu shemu wetu wee ,,!
Nikamuona mke wangu anashangaa tu huku akiwa haamini anachokiona , kumbuka mwanaume wake yupo ndani ,

Hayaaaa nomanomaa nomaaa ,,!!!????????

NILIMDANGANYA MKE WANGU NIMEFUKUZWA KAZI KUMBE NNALIKIZO MIEZI 3

SEHEMU YA 12

Nikamuona mke wangu anashangaa tu huku akiwa haamini anachokiona, kumbuka mwanaume wake yupo ndani,
Yule bosi wangu akamfuata nakumpa hongera eti kwa kunitunza na kuniamsha asubuhi niwahi kazini , haya mafanikio ni wewe ndo umesababisha hongera sana shemeji na ofisi imekuzawadia shilingi milion 1 lakini hii milioni moja hatukupi sisi ,bali atapewa mumeo nae atakupa yeye kwa mikono yake, muda wote huo mke wangu alikuwa ananiangalia tu huku akiwa kama mtu mwenye maswali mengi yasiyo na majibu , weee shemejiiiii ,, yule bosi akamstua mke wangu baada ya kumuona yupo kwenye dimbwi la mawazo , mke wangu akastuka na kusema Asante jamani nilikuwa kwenye mawazo sana unajua siamini kama mume wangu amepata gari kama hili , bosi akamwambia basi ndo uwamini sasa ,
Wafanyakazi walinipa hongera huku hawajui kinachoendelea mimi na mke wangu waliona tupo sawa tu yaani tunafuraha tele kumbe moyoni moto unawaka ,
Zawadi ya wafanyakazi ikaletwa ubavu wa mbuzi akakabidhiwa mke wangu huku wafanyakazi wakisema mtengenezee shemeji ale ashibe , tulifirahi sana na tukawashukuru , na wakaaga wakaondoka nikabaki na li V8 langu nikiwa siamini kabisa kama ni lakwangu, mke wangu alisimama tu pale mlangoni akiniangalia ,niliingia kwenye gari hilo na kuwasha mziki nikaanza kucheza mwenyewe, yaani ilikuwa ni furaha Sana ,
Niliingia ndani nikachukua mkaa na kuwasha jiko la nyama kisha nikatoa ule ubavu wa mbuzi nikauchoma huku mziki unapiga kwenye gari ,mke wangu alijikaza akaniuliza vp nije nikusaidie kuchoma nyama ,? Nikamjibu hapana nenda kamuhudumie mumeo huko chumbani , jibu hilo likamchoma mke wangu nikamuona amekaa kimya tu ananiangalia nnchokifanya ,
Nilichoma nyama nikawa nakata pande moja nakuja nalo mpaka pale kwenye V8 langu nikawa nalitafuna huku napiga yope maana nilifungulia mziki nyimbo ya diamond, yaani ungebahatika kuniona ungecheka maana nilikuwa kama chizi , niliingia ndani kuchukua sahani nilipotoka nikamuona mke wangu amechukua kisu eti anakata kipande cha nyama , nikajikuta namwambia ,eeeeh ebu toka hapo na uwache unachokifanya ,yaani nyama yangu unataka kumpelekea bwana ako ,,? Mke wangu alihuzunika sana maana aliona kama namkejeli, alikuwa amekata kakipande kadogo tu yaani kama ka kuonja nikampokonya nikakitumbukiza mdomoni nikakitafuna , nikamwambia atoke hapa karibu yangu bwana ake asije akaniona akanivunja sehemu, nilimuona nikama machozi yanamlenga lenga na mimi sikujali nikaendelea zangu kuchoma nyama huku nacheza zangu mziki , usoni nilimchukia Sana ila moyoni nikama upendo bado ulikuwepo maana kuna muda nilikuwa namuonea huruma,
Mke wangu aliingia mule chumbani alikokuwa yule bwana ake , nikasikia kama wanagombana maana walikuwa kama wanafokeana , sikuwajali mi nikaingia zangu ndani nikajiandaa nikaweka ile nyama nyuma ya buti ya gari maana nilikula nyama ikanishinda nikaona kuliko nimuachie mke wangu si bora nikawape wale mafundi wangu, nikawasha gari huyooo mpaka kule kwenye nyumba yangu nikawakuta mafundi wanapiga kazi si mchezo kweli ukiwa napesa kila kitu kinakwenda fasta tu,
Niliwapa ule upande wa mbuzi na mchana wakapiga bonge la ugali tukala pamoja ,
Nyumba ilikuwa wanaiezeka mabati ya msauz na ndani walikuwa wanaendelea na prasta pamoja na nyiru ,
Ilifika muda kama wa jion nikawaaga mafundi na kuwaachia posho kidogo, nikaenda kupanda kwenye V8 langu lakini wakati nafunga mlango nikashangaa mtu amefungua mlango wa kushoto akaingia ,alikuwa ni mke wangu, sikusubiri hata aongee nikamwambia SHUKA CHINI,,! akajifanya anajibalaguza na kuongea eti mi nnamaongez nawewe,,, nikamwambia SHUUUKA CHINIII ,,,!!



Kumekuchaaa.
   

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

side chick episode 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

SIDE CHICK EPisode 2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 18

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 17

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 16

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 8

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

RATIFA Sehemu ya 32

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

BOYCHILD PART 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 4.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 29

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

LOVE Part 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 28

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NAWASHWAA Sehemu nne.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 26

mrindia rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 25

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest