NILIMDANGANYA MKE WANGU NIMEFUKUZWA KAZI KUMBE NNALIKIZO MIEZI 3
SEHEMU YA 16
Aisee sikuweza kuimalizia hii sms nikakaa chini kama mzigo,,,,
Nilipata mstuko wa moyo nikatamani niende nikachomoe hata yale madrip aliyowekewa ili afie mbali lakini nilishindwa ,nikaona machozi yananitoka tu yenyewe, ndugu msomaji usiombe uwambiwe ukweli wako yaani kitu chochote chenye ukweli kinaumiza sana moyo,
Nilimuwaza sana mtoto wangu jinsi alivyompole wala sio muongeaji tena nampenda sana kama mwanangu eti leo naambiwa sio mwanangu , roho inaniuma sana mwenzenu,
Kuna nesi alikuja akanikuta nimekaa tu pale chini akaniuliza kulikoni wala hata sikumsikia ,nilikuwa mbali sana kimawazo ,niliona jinsi wanawake walivyowakatili ,eti yule mtoto sio wangu,?
Simu ikaita alikuwa ni afande nilishindwa kuipokea ,ikaita mpaka ikakata , ikaita tena ndipo nikaipokea , akaniuliza vip mgonjwa , nikamjibu bora afe tu nikuoe , ilikuwa ni kauli yenye utani lakin ndani yake nilimaanisha , afande akacheka akajua utani , akaniambia acha utani bana vip anaendeleaje, sikumjibu aisee nilijikuta kuna kitu kinanikaba kwenye Koo nikaanza kulia , afande akajua labda mke wangu amefariki akakata simu na akatoka kituon akaja mpaka pale hospital akaniuliza vipi mbona hivyo ,? Nikampa tu ile sms asome , aliisoma huku anasikitika , sasa mimi si unajua ile sms sijaisoma mpaka mwisho ,? Sasa yule afande akaisoma mpaka mwisho akaniambia kama amesema mtoto sio wako basi hata hiyo mimba sio yako , nikashangaa nikamuuliza mimba ipi ,? Akaniambia we si umesoma hii sms , nikamwambia ndio ila sio mpaka mwisho , akaniambia basi ameandika anamimba yako tena ya miez miwili, nikashangaa nikamuuliza yaani anamimba yangu ,,? Afande akasema ndio , nikamuuliza afande miezi mingapi kasema ,afande akajibu miwili , nikamwambia yaani hapo sijui kama ni yangu kweli au , afande akaniambia hebu acha upumbavu bana utamwamini vipi mtu alikuwa na wanaume tena anafanya mapenzi mbele yako hebu nyanyuka kwanza twende nyumbani , niliwaza nikawazua , afande alininyanyua tukaondoka pale hospital,
Tulienda nyumbani kwa afande ilikuwa ni nyumba ndogo tu inavyumba vitatu lakini kamjengo kakisasa , alinipa pole kwa kuniliwaza akaniambia yule mwanamke ni nyoka kaza moyo umfukuze pale kwako ,kwa sababu mwanzoni ulikuwa unamwachia nyumba kwa sababu ya mtoto sasa mtoto sio wako na anadai anamimba yako na je kama pia sio yako itakuwaje ,na imebaki wiki moja tu urudi kazini , nikamuuliza sasa ntamfukuzaje , akaniambia akipata nafuu mfukuze kabisa ,nikamjibu sawa ,
Tulikunywa tukala na sikurudi nyumbani nikalala kwa afande , yaani sio kulala tu tulilaliana , nyie afande nyie Acheni tu , unajua utofauti wa afande niyeye ndo anataka yaani hata kama umewahi kumaliza halalamiki atakufanya urudi mchezoni lakini mke wangu ukiwahi kumaliza tu analalamika huku analala zake badala ya kunifanya nirudi mchezoni tuendelee na mchezo , nikanogewa aisee na penzi la afande , nikasema ntamfukuza mke wangu niishi na afande,
Kesho yake nikatoka kwa afande ilikuwa ni mchana mchana nikarudi home , nikakuta mke wangu amerudi yaani ameruhusiwa kule hospital, nilipandwa na hasira nilipomuona , nikajikuta nimeingia ndani na kukusanya kila kilichochakwake na kuvitupa nje nikamwambia ondoka sitaki hata kukuona , mke wangu alianza kulia na akaniambia usinifukuze mume wangu nitaenda wapi na hii mimba yako , nikamjibu hiyo mimba sio yangu kama umeweza kunibambikia mtoto kwa miaka yote utashindwa mimba nimekwambia toka kwangu, wakati mke wangu analia akaja mtoto wangu naye akawa analia huku anasema baba mbona unatufukuza nilimwangalia kwa hasira yule mtoto baade huruma ikaniingia , nikajiuliza nifanyeje sasa , mke wangu alikuja mpaka miguuni kwangu akaniambia mume wangu nilikudanganya kuwa mtoto sio wako lakini hii mimba siwez kukudanganya ni yako ,nikamjibu funga bakuli lako nikamsukuma nakumwambia sitaki niwaone hapa kwangu wewe na hako katoto Kako ,, ilikuwa simanzi sana kwa kale katoto maana kalikuwa kanalia huku kamemkumbatia mama yake pale chini aisee nilijikuta machozi yananitoka ,, nisamehe mume wangu nimekosa miee mimba hii ni yako nitaenda wapi mie na hali hii na mtoto,, aliongea mke wangu huku akilia ,
Naombeni ushauri jamani sijui nimsamehe ,lakini nishampenda afande , na sijui kama hii mimba ni yangu ,
Nini kitaendelea usikose mkasa huu,????
ITAENDELEA.