NILIMDANGANYA MKE WANGU NIMEFUKUZWA KAZI,
KUMBE NNALIKIZO MIEZI 3,
sehemu ya , , 1____2
Dunia imebeba mengi sana achana na majumba na magari pamoja na miti na watu wake , kuna vingi vimebebwa ndani ya mioyo ya watu , kuna Siri nzito zimejificha ndani ya moyo wa mwanadamu ,
Nasema hivyo kwa kuwa yamenikuta mwenzenu , nilipojaribu kuupima uvumilivu wa mke wangu kipindi cha shida , sikujua kuwa binaafamu anapande mbili , na kila upande haufanani hata kidogo,
Nilioa miaka mi4 iliyopita tulibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume , mimi namke wangu tuliishi kwa kupendana sana na nikampa mtaji wa kufungua duka la vipodozi maeneo ya Kinondon Manyanya , namimi nafanya kazi ya Reli TAZARA ,
Nilikuwa mchapakazi mzuri tu kiasi kwamba mpaka mabosi walinipenda na kuniongezea mshahara ,maisha yakawa mazuri tu mimi na mkewangu tukafanikiwa kujenga nyumba yetu kupitia ule mshahara wangu na pesa alizopata mke wangu kwenye duka lake la vipodozi ,
Tukahamia kwenye nyumba yetu mimi na mke wangu pamoja na mtoto wetu , maisha yakawa nafuu na ya furaha Sana ,
Siku moja niliitwa ofisini na kuambiwa na wakuu wangu wa kazi kuwa ofisi imenizawadia kiwanja na imenipa likizo ya miezi mi 3 kama zawadi ya mfanyakazi bora , nikashangaa sana na nikazani labda wamenifukuza kazi maana likizo ya miezi mi3 ni mingi sana , wakanitoa hof wakaniambia ukirudi utakuwa chini ya Station meneja , yaani akitoka meneja wa stesheni naingia mimi , nikafurahi sana , nilikwenda kukiona kiwanja na wakanikabidhi na pesa kidogo za likizo yangu ,
Nikarudi nyumbani nikiwa na raha tele , nilikuta mke wangu bado hajarudi ila mtoto wangu yupo amesharudi shule , nilikaa chumbani kwangu nikiwa siamini nikaangalia benk kujua nnashingapi nikagundua zinatosha kabisa kujenga nyumba ya kisasa ya vyumba 3 na vyoo humo humo ,nikajisemea hapa simwambii mke wangu kama nimepewa likizo , ila ntamwambia NIMEFUKUZWA kazi halafu nijenge nyumba haraka ndani ya miezi mitatu iwe tayari yaani hata kama itakuwa bado basi naamini ni mambo madogo madogo tu , kisha nitampa nyumba hiyo kama zawadi ya uvumilivu wake kwangu ,
Basi nikajifanya mnyonge kupita kiasi hata mke wangu aliporudi alinishangaa na kuniuliza kulikoni ,
Nikamwambia mke wangu NIMEFUKUZWA KAZI,
Mke wangu akashangaa na kuniuliza kosa la kufukuzwa kazi , nikamjibu kuna mizigo ya watu imeibiwa sasa wananihisi ni mimi , mke wangu akawa na simanzi sana na akawa kama ananionea huruma nami nikajiambia "hapa kweli nimepata mke ,"
Basi tuliongea mengi siku hiyo nikamwambia itabidi nikatafute Kaz sehemu nyingine nayeye akanipa moyo kuwa nisijali ntapata kazi nyingine ,
Bas siku ya kwanza ilipita nikaenda benk na kutoa pesa zote na kurudi nazo nyumbani Nakumbuka zilikuwa kama milion 30 hiv nikazihifadhi kwenye droo ya kabati moja na funguo nikawa nazo mimi , mke wangu aliporudi nikajifanya nalia huku nasikitika sana aliponiuliza tatizo nikamwambia ofisi wameamua kuchukua pesa zangu zote benk ili kufidia mizigo yao iliyopotea ,niliongea huku najifuta machozi, mke wangu alistuka sana na kuanza kulia nayeye , tukabembelezana na kupeana moyo kuwa ndo maisha ,
Basi kesho yake mke wangu akaenda dukani kwake na mimi nikajifanya natoka ili nikatafute kazi ,
Nilienda kule kwenye kiwanja changu na kutafuta mafundi na ujenzi ulianza mala moja ,
Nilikuwa nawahi kurudi na kupika chakula cha usiku na mke wangu akija tunakula na akiniuliza vp umepata kazi namwambia bado kazi ni ngumu ,
Basi maisha yakaendelea huku mke wangu ndo akawa anatoa pesa ya matumizi pale nyumbani ,
Zilipita wiki mbili tu mke wangu akaanza kuchelewa kurudi nyumbani , na kila nikimuuliza anadai wateja ni wengi , sio kawaida yake na akirudi anadai amechoka ,nikavumilia tu ,
Wiki ya tatu ilipoanza nikasema leo sipiki nataka mke wangu akirudi ndo apike maana nimemis kula chakula chake , nikanunua mboga na kuziweka , aliporudi akaniuliza vip umeshapika ,nikamwambia bado nataka leo upike wewe maana nimemis chakula chako ,
Cha kushangaza mke wangu alibadilika sura na kuniuliza kwani mume wangu we unakazi gani hapa nyumbani , yaani unanisubili mimi nitoke kazini nije nipike, ?
Nikamjibu kwa upole tu nikamwambia lakini mke wangu nimemis chakula chako ,
Mke wangu akaniambia sasa mi nimechoka na siwezi kuingia jikoni mda huu kama ni mtoto nenda kamnunulie chips ale tulale ,aliongea hivyo na kweli akaingia chumbani ,
Nikabaki nimejiinamia tu nakujiuliza hii ni wiki ya tatu tu je hiyo miezi mi 3 itakuwaje
ITAENDELEA
NILIMDANGANYA MKE WANGU NIMEFUKUZWA KAZI KUMBE NNALIKIZO MIEZI 3,
sehemu ya 2
Nilijiinamia na kujiuliza hii ni wiki ya 3 tu mambo yako hivi ,, je hiyo miezi mitatu je ,
Niliwaza Sana ,
Niliamua niingie chumbani kwetu nikamkuta mke wangu amejilaza kitandani , nikakaa pembeni yake na kumwambia mke wangu nisamehe kama nitakuwa nimekosea ,
Mke wangu aliniangalia tu na hakujibu kitu akavua nguo zake za kzini akaenda zake kuoga ,
Sasa ikabidi tu niingie jikoni nikaanza kupika huku nikijitahidi mtoto wangu asijue kinachoendelea , nikapika chakula na kukitenga mezani nikamtuma mtoto akamwite mama yake chumban amwambie chakula tayali aje tule , lakini akamjibu ameshiba , naomba tu niseme ukweli nilijisikia vibaya mno , nikaamka na kumfuata chumbani , nikamwambia mke wangu samahani kama nilikosea naomba tukale maana chakula nimepika kingi kwa ajili yetu , akanijibu kwa shot kat nakuja , na alipokuja tulikula lakini ni kimya kimya , mpaka tukamaliza na yeye akawahi kuamka na kuingia zake chumbani ,
Moyo uliniuma sana kama mwanaume ,
Niliingia na mimi chumbani nakumuuliza kwani shida nini mkewangu ? Mke wangu akanijibu amechoka tu ,nikaona ngoja nisimsumbue nimwache alale ,
Kesho yake aliamka na hakuandaa chai ,maana ilikuwa akiamka anafanya zake usafi wa ndani anaandaa chai ndio anaenda kazini , sasa aliamka na kujiandaa akaondoka zake na hata kuniaga ameniaga wakati yupo mlangoni ,
Nilivumilia tu na mimi nikaamka nikamwandaa mtoto ili aende shule , kisha na mimi nikajiandaa nikaenda kule kwenye ujenzi wa nyumba yangu ,
Ujenzi ulikuwa unaenda vzr tu maana tulishamwaga zege chini sasa tulikuwa tunakata vyumba, nikasimamia mafundi na kwa vile walikuwa wengi walipiga koz sita wakaniambia hapa tuache kwanza mpaka siku 3 ili siment ishike vzr kwa sababu tumejenga nyumba haraka ,
Nilikubali bas nikaondoka zangu kurudi nyumbani nikanunua mboga nikapika chakula cha usiku , tukakaa mimi na mwanangu tukiangalia tv huku namfundisha baadhi ya maswali ya shuleni ,
Kawaida mke wangu anarudi nyumbani saa 2 au amechelewa sana saa 3, lakini siku hiyo mpaka saa 4 hajarudi , ikabid nimpigie simu nimuulize kulikoni ,
Lakini simu iliita mpaka ikakata , halafu akatuma mesegi kuwa yupo njiani anakuja ,
Nikajiuliza sasa ameshindwaje kuipokea simu kama yupo njiani mpaka anatuma sms ,?
Nikaona ngoja tu niwe mpole , nikamwambia mwanangu aje tule kwani mama atachelewa kuja , tulikula na mwanangu lakini mimi chakula hakikupita kabisa nilijitahid lakini nikashindwa nikamtandikia mtoto akalala na mimi nikabaki sebuleni nikimsubilia mke wangu , aliingia nyumbani saa Tano kasoro , na akanisalimia na kupitiliza chumbani , nikamfuata na nikamuuliza mbona leo umechekewa kulikoni ,?
Akaniambia leo kulikuwa na wateja wengi na alichelewa kufunga , nikamwambia si ungenipigia simu ukaniambia ,,? Akanijibu kwani we shida yako nini mi si nimesharudi ,?
Nikamwambia shida sio kurudi ,shida niwewe kunipa taarifa mapema mi nisingejua kama unawateja wengi , akanijibu basi ndo ushajua kwani kuna tatizo lingine ,? Nikamjibu hakuna , ila twende tukale maana nilikuwa nakusubili wew , akanijibu mi nimeshakula maana nilijua ntachelewa kuja na ntakuta chakula kimepoa , alinijibu kawaida sana huku akijifunga taulo ili akaoge wakati mimi nilihisi kama kuna donge moja limenikaba kwenye Koo ,nilitamani kumpiga lakini nikajiuliza unampigia nini ,? Ikabidi na mimi nijilaze tu kitandani ,
Wakati anaoga simu yake ilikuwa kwenye mkoba wake nikasikia imeingia mesegi nikapatwa na shauku ya kuisoma nikaichukua ile simu nikatoa password ila haikukubali inamaana alikuwa kaibadilisha , wakati natafakari kwanini amebadirisha paswed ikaingia meseg nyingine , na kama unavyojua ujinga wa Smart fon mesegi inaonekana kwanza hapo juu haijaenda kwenye uwanja wa mesegi,
nikaisoma haraka haraka , hapo ndipo nilipochanga nyikiwa nikajikuta natetemeka mikono ,
Haya jamaa amekuta ujumbe gani tuonane kesho ????
.