NILIMDANGANYA MKE WANGU NIMEFUKUZWA KAZI KUMBE NNALIKIZO MIEZI 3
SEHEMU YA 17
Naombeni ushauri jamani sijui nimsamehe lakini nishampenda afande na sijui kama hii mimba ni yangu,
Niliingia ndani nikawaza huku nimejiinamia kichwa kilikuwa kimejam kabisa , ikabidi nipige mahesabu ya miezi miwili iliyopita Nakumbuka nilifanya nae mapenzi mala moja tu tena Nakumbuka ni mimi ndio nilimlazimisha na ni miezi miwili iliyopita , sasa je hii mimba ni yangu kweli au ni fix tu ,? Nakwann hakuniambia mapema ? Niliwaza sijapata jibu nikampigia afande ili aje maana nilikuwa sijielewi ,
Afande akaja na akamkuta bado mke wangu yupo nje na mabegi yake tena bado analia , afande akamuuliza mke wangu mumeo yupo , mke wangu hakujibu ila alimwangalia kwa hasira , afande akaingia ndani huku akimcheka ,
Vip mume mbona umeniita gafra hivyo naona na mkeo kafungasha hahahaaa ,, aliongea afande kwa kejeli , nikamjibu nimemfukuza na mtoto wake lakini hataki kuondoka anasema ataenda wapi na mimba yangu ,afande akaniuliza kwahiyo nawewe umekubali kuwa hiyo mimba ni yako ,? Mi nikamjibu sijui kama ni yangu kwasababu kila nikipiga hesabu ya siku niliyofanya mapenzi sielewi kabisa , akaniambia basi fanya kitu kimoja , nikamjibu kitu gani ,? Akaniambia mpangishie chumba halafu hapa weka wapangaji nawewe kakae kwenye ile nyumba mpya halafu subiri miezi aliyosema mpaka ujifungue mtoto kama ni wako bas utamuhudumia akiwa huko huko kwenye chumba cha kupanga ,
Nilimuelewa afande akanibusu tukatoka zetu nje tukamuacha mke wangu bado amekaa zake chini na mtoto wake , roho iliniuma sana ukizingatia ni mtu niliempenda sana , afande akamwambia kwa ulichokifanya ulitakiwa usiombe msamaha yaani uondoke kimya kimya mwanamke khasidi wewe ,unasubutu kabisa kuingiza mwanaume ndani kwako huna haya wewe na wala hujui vibaya , yaani unabahati umempata mwanaume huyu ingekuwa ni mwingine ungevunjwa shingo mpuuzi wewe ,tena mume wangu funga milango yote aondoke zake ,aliongea afande mi nikaona kama masihara nikasita sita kufunga mlango ,nikamuona yeye afande akafunga milango yote tukaondoka tukimwacha nje na mabegi yake ,mke wangu alianza kulia huku akisema ataenda wapi na mtoto, afande akamwambia tafuta pakwenda , aisee unajua asingekuwa afande ningeweza kumsamehe mke wangu maana mi nnahuruma sana lakini afande alikuwa anampa vidonge vyake mpaka mke wangu anajiinamia , nilimuuliza afande mbona ulisema tumtafutie chumba halafu unafunga mlango ,afande akajibu inatakiwa nayeye apate uchungu kama ulioupata wewe kama ukirudi ukimkuta bado yuko nje basi utamruhusu aingie ndani ,
Sasa wakati bado tuko kwenye gari tunamjadili mke wangu ,gafra get dogo likafunguliwa akaingia yule jamaa aliyempokonya duka mke wangu , akamkuta mke wangu amejiinamia pale nje nasisi tupo kwenye gari, akamuuliza kwanini unataka kuitoa hiyo mimba ,? Mke wangu akamjibu hii mimba nishakwambia sio yako ni yamume wangu ,yule jamaa akamwambia unajua weweusiniletee kichaa ntakuzibua sasa hivi umeniskia , mi na afande tukatega sikio vzr huku tukiangalia muvi ile , mke wangu akanyanyuka na kumwambia et nipige kama mwanaume kweli , yule jamaa akamwambia nishakwambia ukiwa na shida uje kule dukani uchukue pesa ili uitunze hiyo mimba yangu mbona unasema leo sio yangu , ? Mi na afande tukaangaliana , afande akaniambia umeona sasa na ulitaka kukubali mimba ni yako ,,nikapandwa na hasira nikatamani nitoke nikamzibue hata makofi ,afande akanizuia akaniambia tusubilie kwanza tuone mwisho , mke wangu akaanza kumwambia yule jamaa , nishakwambia mi nawewe mahusiano yameisha na hii mimba sio yako ni yamume wangu , jamaa alipandwa na hasira akamkata makofi mawili mke wangu tena mbele ya mwanae aisee pamoja na kuwa nilikuwa na hasira lakini ziliisha nikajikuta namuonea huruma huku nikitamani nikampige yule jamaa ,afande akanizuia tena , yule jamaa akamuuliza tena sasa niambie mimba ni ya nani ,,? La sivyo nikutandike makofi mengine , yule mtoto akawa analia huku anasema muache mama yanguuu babaa njoo umuone huyu anampiga mamaa ,,
Yule jamaa hakujali akamkunja tena mke wangu nakumwambia kwanini uliniambia una mimba yangu na sasa unasema sio yangu,,? Kabla mke wangu hajajibu jamaa akampiga tena Kofi la uso,,,, aisee ,,
Mwenzenu kalikoroga huku kaingia kusikoingilika ,?
Toa maoni yako basii tuyasome , mi naona amsamehe tu maana dah ,,
ITAENDELEA.