Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  artist

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 7-- 8

1st Jun, 2025 Views 29

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 7

Nilimkuta yule Dada kashika cm yangu yuko na karatasi na pen anaandika namba ya Mahamood,, nikamuuliza vp mbona unachukua namba kwenye cm yangu? Akabaki kimya! Nikamwambia Dada nakuheshimu sana harafu ww ni mkubwa kwangu si vzr nikakuvunjia heshima,, akaniambia nilikuwa nataka kujua huyo Bwana wako anaekuhudumia yupo nchi gn? Ndio maana nikawa nachukua namba ili nijue ni za nchi ipi, nikamwambia aliyekwambia mm nahudumiwa na Bwana nani? Nikamwambia Sasa huyo ni Babu yangu yupo Nje,, akabaki katoa macho nikachukua ile karatasi,, nikamwambia naomba aende nataka kulala mapema kesho naenda kkoo kufata mzigo wa wateja,, bc alinyanyuka akaniambia sawa ucku mwema ila hajafurahia kabisa,,, akiwa anatoka hata mlangoni hajafika Mahamood akapiga cm nikapokea, bc Yule Dada akarudi akakaa kitandani akawa anasikiliza Mahamood akaniuliza vp umelala? Nikamwambia hapana ndio najiandaa, akaniambia ulifanikiwa kupata nyumba kubwa? Nikamwambia sio sana, akaniambia washa data nikupigie WhatsApp,, mhhhh nikaogopa asije akaona chumba kimoja,, nikamwambia sina MB na maduka yamefungwa,, akaniambia sawa ila sitaki uishi kwa mtu, wala sitaki makundi makundi, nimeamua kukuhudumia kwa kila kitu na nitabadilisha maisha yako, utaenda Nchi yeyote utakayo taka ila tu utulie,, nikamwambia sawa akakata cm,, yule Dada akawa ananiangalia kama mtu anayetamani,, nikamwambia naomba nilale bc tutaonana kesho,, akaniambia Jee unalinga sana eeh? Unajiona Queen?? Iv unauzuri gn wa kupata Bwana wa namna hio?? Nikabaki namtizama tu,, akaniambia bc nitakuonyesha akatoka akapigiza mlango

Sikumfatilia sana nikafunga mlango wangu nikalala,, asbh nikaamkia kkoo nilikuwa na oda za watu bc nikawa bize cku hio,, ilifika jion sijarudi kwangu nikapitia salon moja iv ya mteja wangu huwa nampelekea biashara zangu, yule Dada wa salon akawa ananishawishi nitengeneze nywele bc nikakubari nikaanza kufumua nilizosuka ili nioshe, Mara yule Dada wa nyumbani akanipigia cm,, Jee uko wapi? Nikamwambia nipo mahari nimekaa, akaniambia Jee ww huliziki? Yaan una Bwana anakuhudumia kwa kila kitu arafu bado unamsaliti?? Nikamwambia we Dada embu nikome sitaki mazoea ya kijinga na msaliti nani? Unajua nipo wp? Nikakata cm!! Yule Dada wa salon akaniuliza vp unagombana na nani tena? Nikamwambia jirani yangu huyu anapenda kunifatilia sana,, akaniambia ana wivu huyo achana nae,,, bc niliosha nywele nikamaliza nikarudi kwangu, nafika tu nikamkuta yupo mlangoni kwake sijamsalimia wala nn, nikaingia ndani nikavua nguo nikaenda kuoga nikafunga mlango wangu na funguo nikaingia nazo chooni,, natoka bafuni nikamkuta yupo mlangoni kwangu eti Jee mbona umefunga mlango?? Nikamwambia nimechoka sana sijisikii kuongea nataka kulala,, akaniambia unalinga eeh! ,, Kuna mpangaji mwengine pale yeye ni mke wa mtu, akamwambia yule Dada mbona unamuonea Jee?? C amekwambia amechoka ataki kuongea na mtu? Embu muache mwenzio akapumzike, alikuwa ameshika kitasa changu akakiachia nikaingia ndani nikafunga mlango wangu,,, nilikuwa nimebeba chips zangu nikawa nakula huku nachezea cm,, akanitumia msg unajifanya Queen kumbe sura mbaya!! Sijamjibu wala nn,, ila nikawa namtafakari huyu Dada nimemkosea nn? Au anamtaka Mahamood?? Angejua mwenzie maisha yangu ninayopitia bora angeniacha nipumzike tu,, mm Mahamood wala simtaki nimepokea pesa zake sababu ya umasikini wangu tu namchukia Mahamood na mjomba sana kwa kuniharibia usichana wangu ningekuwa na uwezo ningewashitaki wote,, bc nililia hadi usingizi ulinipitia nikalala

Asbh palivyokucha nikaamka nikamshukuru Mungu nikaenda zangu mjini, nilienda kufata mashuka kwenye mnada Tandika ya mitumba, nikachagua mashuka mazuri nikayakunja vzr nikaenda kuyazungusha kwa wateja wangu,, yaan Mungu ni mwema yakaisha yote na nikapata oda nyingine,, nilivyoona biashara ya mashuka inaenda vzr na vipodozi navyo vinaenda vzr nikapata wazo la kwenda kufata mashuka Kampala

Nikasema nisikurupuke kwanza ngoja nifanye utafiti

Bc maisha yangu yakaendelea hapo vita vinazidi mm na yule Dada aitwaye Edina

Itaendelea

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 8

Niliendelea kuwa bize na biashara zangu nikitoka nyumbani asbh bc kurudi ucku hata muda wa kupika sikuwa nao,, nilikuwa nasema ngoja nijichoshe kutafuta hela kwa bidii ili nisinyanyasike tena,, ilipita kama wiki iv niko bize balaa hata Edina nilikuwa sionani nae nikirudi ucku nazama chumbani kwangu,, kuna cku moja nimerudi ucku kama saa tatu iv nikaingia ndani kwangu nikajifungia, mara mlango ukagongwa nikafungua alikuwa Edina, nikamuuliza vp mbona ucku? Mm nimechoka nataka kulala, akaniambia nimekuja nataka uniazime hela nina shida Mama yangu amelazwa kisha nadaiwa kodi,, nikamwambia mm sina hela, hela zangu zote zipo kwa watu, akaniambia bc mpigie Bwana ako mwambie akutumie, nikamwambia sina Bwana na kama unaona rahisi ivo bc na ww mpigie Bwana ako akupe,, hee c akanisukuma nikadondoka chini akaniambia una linga sana? Unazarau sana? Unanijua mm ww? Nikamwambia naomba utoke ndani kwangu Edina,, akaniambia ctoki, akachukua cm yangu akawa anataka kuifungua ila akakuta nimeweka password, akaniambia toa password nichukue namba ya huyo Bwana ako, arafu tuone kama atakutaka tena mshamba ww,, nikamwambia Edina toka ndani kwangu please!! Aisee nikasema kuonewa sasa kumezidi huyu Dada ananitafutia kesi,, hasira zilinijaa za kikurya nilimshika Edina nikamkaba kwa nguvu hadi aliishiwa nguvu,, mara mlango wangu ukafunguliwa alikuwa yule Dada mwingine mpangaji mwenzetu yupo na mume wake wakanishika wakanitoa,, Yule Dada akaanza kukwambia Edina ww mkorofi umemfata mwenzio ndani kwake kwa nn? Nimekusikia muda mrefu unamuanza Jee?? Acha wivu Edina,, kwan mtoto wa watu kakukosea nn?? Edina kimyaa,, nikaanza kulia kwa nguvu na hasira kali nikakumbuka mapito yangu yote, nikajiona na mikosi tuu,, Mara cm yangu ikaita hapo watu wote wapo ndani kwangu ila yule mume wa yule Dada alitoka, nikapokea CM huku nalia alikuwa Mahamood,, vp mbona unalia una shida gani? Nikamwambia kuna jirani yangu hapa ananichukia bila sababu eti anataka namba yako ya cm ili akujue ww nani unaye nisaidia mm? Amenisukuma hadi chini , Mahamood akaniambia huyo mtu yupo hapo? Nikamwambia ndio, akasema embu weka sauti kubwa kwanza, nikaweka hapo Edina anaona aibu yule Dada mwingine anamuangalia,, Mahamood akasema anataka namba yangu ya nn? Kwanza ww Jee c nimekwambia sitaki uishi uswahilini?? Ctaki uzoeane na watu wa ajabu ajabu?? Kwan ile hela haijatosha kuishi masaki?? Nikamwambia naishi bunju napo ni pazuri,, akasema pangekuwa pazuri huyo kahaba asinge weza kuishi nakwambia iv Tafuta dalali akutafutie nyumba Masaki natuma kesho pesa,, harafu wee kahaba acha kumsumbua mke wangu Mm sichukui mwanamke ilimradi nina vigezo vyangu,, ukijiona mzuri bc jipike ujitafune sawa daah Muarabu ana maneno hadi nilishangaa,, bc akaniambia akikusumbua zaidi mripoti polisi, akakata cm

Edina lilimshuka htr, yule Dada akamwambia Edina unatia aibu doh? Unalazimisha bahati ya mwenzio?? Hadi unafikia hatua kutaka kumpiga kisa wivu?? Edina akanyanyuka akaenda zake,, Yule Dada akaniambia lala kesho tutaongea,, bc nikafunga mlango wangu hata kuoga sikuoga nikalala

Asbh palivyokucha Mahamood alinipigia kujua kiliendelea nn nikamwambia safi tu, akaniambia nikatafute dalali nikamwambia leo sipo sawa nitaenda kesho kutwa akasema sawa,, nikaamka zangu nikaoga nikasepa zangu,, nilikuwa naenda posta kwenye maofisi nilikuwa na wateja zangu nawapelekea mashuka,, bc nina mteja wangu mmoja yeye yupo serikalini ni mfanyakazi, alinizoea sana nikamwambia wazo langu la kufanya biashara ya mashuka na mapazia kutoa Kampala kuleta Dar,, akaniuliza ni biashara nzuri yeye ana mtu anaifahamu biashara hio vzr kwahyo ataniunganisha nae,, bc tulikubaliana vzr ,, nikarudi home kwangu nyumba ipo kimya nikazama ndani kwangu huku nimebeba chips zangu,, nimekaa zangu nakula Mara mlango wangu ukagongwa nikafungua ni Edina tena daah huyu Dada jmn!!!

Itaendelea
Soma muendelezo kwa sh 1000
Njoo WhatsApp 0743433005.
   

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MY HEART 03--04

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

*MY HEART* *1---2 *

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 7

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

ANIPHA 6--7.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 05

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

side chick episode 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

SIDE CHICK EPisode 2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NIPE YOTE DADY???15

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 18

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 17

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 16

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 8

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

RATIFA Sehemu ya 32

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NAWASHWAA? Sehemu 13.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NIPE YOTE DADY ???11

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

BOYCHILD PART 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 4.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 29

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

LOVE Part 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 28

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NAWASHWAA Sehemu nne.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 26

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest