Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  artist

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 36 -- 37 SEASON TWO,

1st Jun, 2025 Views 41

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 36

SEASON TWO,
Wapenzi wasomaji pole nimewachelewesha sana kupata msimu wa pili, nilikuwa naumwa kwa kipindi kirefu ila sasa alhamdulillah namshukuru Mungu naenderea vizuri.

Tuendelee
Mimi na Mahamood tuliendelea kuishi kwa kipindi kirefu huku akionekana hataki kwenda kwa wake zake wengine, ikafika kama miezi 3 nikamuomba aende kwa sababu sikutaka ugomvi mimi na wake wenza ambao walikuwa wamenitangulia, akasema hatokwenda ndio nikamuuliza kwanini
Mahamood aliniambia kwamba hataki kwenda kwa sababu kuna masharti mke mkubwa ameweza kuyavunua hivyo ingeweza kuleta matatizo kati yake na mizimu kwa sababu alikuwa amewakosea

Nikamuuliza kwanini unanificha mambo yako, si uniambie ni masharti gani hayo? Akasema mke mkubwa kaamua kushika mimba bila ridhaa yake wakati masharti kipindi anamuoa basi alikuwa anatakiwa asizae na mwanamke huyo.

Nilishangaa nikamuuliza kwa hiyo alivyokuwa ananiambia kwamba hana uzazi ilikuwa ni uongo? Akasema ndiyo ni masharti

Kwa hiyo mbona mimi ulinizalisha watoto akasema haikuwa kwenye mpango wake kuzaa lakini nilipokataa asiniingilie kinyume basi ilitokea kwa bahati mbaya na hata alivyojaribu kuongea na mizimu aliambiwa mimi ni mwanamke mwenye nyota kali hivyo asiniache kabisa

Kwa hiyo mkeo huyo utaacha kumfuata? Akaniambia ili aende lazima huyo mwanamke atoe kwanza hiyo mimba maana akienda kule na mwanamke yule ana mimba basi atapata matatizo makubwa sana.

Nilishangaa mno na niliogopa nikasema ile ni familia ya aina gani mbona ina mambo magumu kiasi hicho? Ghafla tukiwa tunaongea, mke mdogo wa kati ya bi Fatima ambaye alikuwa anaishi Uingereza, alimpigia simu Mahamood.

Mahamood akasema huyu vipi ananisumbua, anataka kuniambia nini? Mimi nilikaa kimya sikuongea lakini Mahamood alipokea simu na kuongea naye.
Walianza kuongea kiswahili kilichochanganyika na kiarabu na kiingereza humo humo, mwanamke akasema "Mahamood tafadhali nahitaji taraka yangu sasa, nimechoka kupoteza muda duniani
Mahamood akamuuliza kwanini mnanitesa hivi nyie wake zangu? Yaani hamniachi nipumue muda wote visa tu? Mbona huyu mdogo yeye hana mambo mengi

Huyo si ni mwafrika ni maskini unadhani ataweza kukuacha wakati una hela? Mimi nnahitaji talaka yangu nataka nikaanze maisha yangu nimechoka maisha ya kuishi miezi mitano bila mum
Maneno ya kwamba mimi mwafrika nina maisha magumu siwezi muacha yaliniuma, nikajikuta nalengwa na machozi.

Mahamood alinitazama machoni, alipogundua natokwa na machozi akakata simu na kuniwekea mkono begani akaniambia "mke wangu nakupenda sana, na ndio maana niliondoka Dubai badala niende uingereza nikaja kwako ni kwa sababu wewe ni mke bora" niliendelea kulia

Najua maneno ya Fatima yamekuudhi lakini naomba usilie piga moyo konde kumbuka tulipotoka
"Ameniita mimi maskini? Nilisema kwa uchungu huku kilio kikiongezeka"

Kwa hasira, Mahamood aliinuka akaenda chumbani na kutoka akiwa na kalamu na karatasi, akaanza kuandika talaka ya yule mwanamke, halafu akaipiga picha.

Nikamuuliza unafanya nini akasema anamtumia kweli talaka maana si kaitaka nikajaribu kumkataza lakini alimtumia kupitia whatsapp huku ikisindikizwa na voice note kwamba original copy atampelekea wiki inayofuata akiwa anaelekea uingereza kuzifuatilia biashara zake

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 37
Ilikuwa kama masikhara lakini pale ndiyo talaka ilikuwa imeshatoka hivyo, akaniambia Mamujee nafanya hivi kwa sababu nataka uishi kwa amani sipendi mtu yeyote akuudhi wewe, napenda muda wote uwe na furaha sawa mke wangu

Sawa, ila usichukue maamuzi ya haraka sana nilisema akasema ni muda mrefu alikuwa akitamani kumuacha huyo mwanamke mwenye kiherehere

Basi tukawa tumeishia pale, sasa siku ziliposogea Mahamood aliniaga kwamba anaenda Uingereza ili akaziweke biashara zake vizuri maana yule hakuwa mke wake tena hivyo alihisi anaweza akamfilisi.

Mahamood alijiandaa akaondoka kuelekea Uingereza, sasa, akaniacha peke yangu nalea watoto pamoja na kuendeleza biashara zangu.

Cha kushangaza mawasiliano yangu mimi na Mahamood yalikosekana tangu alipokuwa ameondoka na kuelekea uingereza, zaidi ya miezi miwili nikawa simpati na hakuwahi kunitafuta

Nilipata wasiwasi sana kuhusiana na yule mwanaume, nikajiuliza au alifariki au amekumbwa na nini kwa huyo mke Fatima wa uingereza, sikupata jibu

Namba ya Fatima niliyokuwa naijua ilikuwa haipatikani kipindi chote, na hata mke mkubwa ambaye ni Shakira alikuwa hajibu message zangu kabisa kila nilipomtumia message alinipiga blue tick na kuendelea na maisha.

Nilijua dhahiri kuna tatizo kubwa limetokea ila sikuwa na cha kufanta, ndiyo ikabidi nimshirikishe dada wa kazi akaniambia kwamba ni heri nifunge safari niende Dubai kule nyumbani nikaone kinachoendelea.
Niliona ni wazo zuri hivyo nikamuuliza kaka yangu Mwita akaniambia niende nikajue kilichotokea, kwa kuwa nilikuwa napafahamu Dubai nilianza kujiandaa na safari kwa kukata tiketi na kuandaa vitu vyote vinavyohusika.

Ikiwa ni siku moja tu imebaki ili nisafiri, nilienda dukani nikafanya kazi tangu asubuhi mpaka jioni muda wa saa kumi na mbili na nusu nikasema niondoke nikajiandae ili kesho tuondoke.

Nilipofika nyumbani nilimkuta dada wa kazi akiwa anafundisha watoto sebuleni, mahesabu hesabu na kadhalika, nikawashika mikono kwa furaha nashangaa wananiambia
"Daddy daddy" mi najiuliza Daddy kafanya nini ndipo dada wa kazi akasema Mahamood amekuja yupo ndani, nilishtuka na kudhani ni masihara, nikaondoka haraka kuelekea chumbani kumuona Mahamood

Nilipofika nilishangaa kumuona Mahamood kalala kitandani kifua wazi, macho yake yanatazama juu darini, huku yakiwa yamejawa na machozi anaonekena mwenye huzuni kubwa moyoni mwake, kilichonishtua zaidi ni namna ambavyo Mahamood alikuwa amekonda yaani mwili wake umedhoofika sana ni mifupa tupu ilikuwa imeshabaki ikifunikwa na ngozi, nikaogopa kwanza
Full sh 1000
WhatsApp 0743433005.
   

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MY HEART 03--04

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

*MY HEART* *1---2 *

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 7

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

ANIPHA 6--7.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 05

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

side chick episode 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

SIDE CHICK EPisode 2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 18

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 17

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 16

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 8

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

RATIFA Sehemu ya 32

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

BOYCHILD PART 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 4.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 29

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

LOVE Part 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 28

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NAWASHWAA Sehemu nne.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 26

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest