MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 17 -- 18
Tulikumbatiana pale na Kaka yangu huku shangazi nae akitusii tunyamaze, shangazi akamkaribisha Kaka ndani , tuliingia ndani yaan tunaangaliana na Kaka hatumalizani kila mtu ana mengi kwa mwenzie, Kaka aliandaliwa chakula akala, mie sikutaka kula cha mtu, mjomba akatoka akakaa nae sebleni maongezi yanaendelea, nilipigiwa cm na Mahamood nikatoka nje kuongea nae, nikamwambia nipo kwa shangazi yangu na Kaka yangu amekuja, bc alifurahi sana akasema bora amepatikana mtu wa kupokea mahari yangu, nirirudi ndani, Kaka akaanza kunitania Amamu umekuwa mrembo, kweli dar haiongopi tulicheka pale yaan ilikuwa raha tu, mda ulifika nikawaaga niende kwangu, Kaka akashangaa Kwan hukai hapa? Shangazi akajibu c umesema amependeza sasa atakaaje hapa wakati amekuwa sasa? Mhhhh bc Kaka akasema twende nikupeleke hadi kwako, shangazi akarukia utampeleka vp wakati na yeye ana gari lake? Jmn shangazi anajibu kila kitu, Kaka akashangaa Amamu una gari?? Embu njoo nje kwanza tuongee vzr unipe Siri ya mafanikio yako,, tukatoka nje ila shangazi akili yake yote ipo kwetu,, akaniuliza hii ndio gari yako? Nikamwambia ndio, nikaifungua tukaingia ndani, akaniuliza vp ulimaliza kusoma hio kozi yako?? Nikamuuliza kozi gn tena? Wakati tangu afe Baba shule ilinishinda? Akasema kwan hukumaliza form 4?? Nikamwambia Kaka bhana usinichoshe kumaliza huko ananisomesha nani? Kaka alishangaa, akasema mbona aliambiwa na shangazi kuwa nimemaliza F4 na nipo tu nyumbani ndio Kaka kutoa hela niende chuo kumbe shangazi alichukua pesa kwa Kaka ili niende chuo niliumia sana nikamwambia Kaka elimu yangu ni ile ile aliyoniacha nayo Baba sina Zaid, bc akaniambia tutaongea vzr kesho maana shangazi alikuwa hana amani mara katoka nje mara kaingia ndani
Nikarudi ndani kuaga then nikaenda zangu kwangu,, tulihaidiana na Kaka atakuja kwangu mapema tu,, nilichukua namba ya cm ya Kaka, bc asbh nimeamka nikafanya zangu usafi, nikaenda buchani nikanunua samaki sato wangu ili nimpikie kaka ugali, kwetu chakula chetu kikubwa ni ugali tena wa mtama
Kaka alinipigia nimuelekeze kwangu nikamuelekeza akafika, yaan alifika mapema hata chai hakunywa nikamuuliza mbona mapema, akasema Amamu umenivuruga ulivyoniambia hujamaliza hata F4 , nikamwambia ndio ivo Kaka, nikamuuliza kwan shangazi ajakuambia chochote nilivyoondoka? Akasema aliongea kuwa ww umeamua kuhama nyumbani ila anahisi umepata mwanaume mwenye pesa, nikamwambia bc unywe kwanza chai, akaniuliza Amamu hapa unaishi na nani? Nikamwambia kunywa chai kwanza then tutaongea,, alikunywa tukamaliza tukaanza maongezi,, nilimuhadisia jinsi nilivyoondoka kwa shangazi na nilivyobakwa na mjomba Kaka angu alilia kwa sauti akaniambia Amamu, mbona hukunitafuta? Nikamwambia ningeanzia wapi? Nikamwambia hadi nilivyorudi kijijini, Baba mdogo alivyonipiga nusu kuniua eti kwann nimechelewa kufika nilikuwa wapi? Na walivyonigeuzia kesi eti mm ndio nilitaka kumbaka mjomba aisee Kaka alilia kama mwanamke , ikabidi nimnyamazishe Kaka yangu, akaniambia, kila cku nilikuwa nakuwaza mdogo wangu ila shangazi ananiambia upo chuo, nimemtumia milion mbili ya kukulipia ada ya chuo kumbe muongo,, bc tukanyamazishana na Kaka, akaniuliza kuhusu pale ikabidi nimwambie tu ukweli kuhusu Mahamood, ila kuhusu kutolewa marinda sikumwambia jmn hii ni aibu yangu mwenyewe ndio maana namwambia adimin furaha asiniweke hadharani ctaki, wamama mtanichamba Mamujee mm
Bc tuliongea mengi kunihusu na Kaka, ndipo na yeye akaanza kuniambia ya kwake,, kumbe Kaka yangu nae kapitia mazito ( wanawake muombeni Mungu awape maisha marefu mlee wanenu Uyatima mbaya sana ) Kaka yangu nae alichukuliwa na shangazi yangu mwengine, tulifanywa kugawanywa mie kuja dar yeye Arusha, alifika Arusha mwanzoni maisha yake yalikuwa mazuri tu, yeye mwenzangu alifanikiwa kumaliza F4 , bc aliishi kwa shangazi pale Arusha ila kama house boy shangazi wa Arusha nae ni mfugaji ko Kaka alikuwa anachunga mifugo,, Sasa cku moja kapeleka ngombe malishoni, cjui ikawaje ngombe mmoja akapotea, alitafuta kote, kwa wenzie wote anae chunga nao bila mafanikio, ndipo kumuambia shangazi, ila shangazi alishindwa kuelewa akampeleka Kaka polisi, akakaa sero wiki tatu hata wa kumuwekea dhamana hayupo, ndipo mapolisi kwa huruma wakamtoa, akawa hana pa kuishi anaishi stendi, ndipo akakutana na vijana wenzie wa mitaani wakaamua waende migodini kwenye machimbo,, Miaka miwili kasota machimboni ila Mungu si Mwanadamu, Kaka yangu katusua
Itaendelea
MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 18
Tuliongea mengi na Kaka yangu akaniambia kuhusu biashara zake na nyumba yake kubwa anayoishi Arusha Maeneo ya Unga limited, nikamwambia na mm nyumba yangu ya Salasala, kuhusu Mahamood Kaka hakuwa na shida aliniambia tu mm ni mtu mzima hawezi kunipangia maisha, wakati tupo tunaongea na Kaka, shangazi akampigia cm Kaka kumuuliza upo wp? Kaka akamjibu nipo mjini huku nitakuja huko muda c mrefu niwaage, naanza safari ucku huu, shangazi alikataa cm,, Kaka akaniambia sina hamu hata ya kwenda pale kwa shangazi, nitafute hotel nzuri nikae siku mbili tatu, nikamwambia kwann usikae hapa kwangu? Alikataa kata kata, bc tulitoka na gari yake hadi maeneo ya mwenge tukalipia hotel, akarudi kwa shangazi kuaga lkn shangazi akawa hataki Kaka aondoke pale, ilibidi kaka alazimishe tu, alimpa laki moja akasepa zake
Tulihaidiana na Kaka asbh atakuja kwangu ili nimpeleke kwenye ujenzi wa nyumba yangu Salasala, bc alinifata kwangu tukaelekea, tukakuta mafundi wanaendelea na kazi, Kaka alishangaa kuona Dada yake naenda kumiliki ghorofa, akaniambia Amamu hongera sana, nataka na mm nitoe mchango wangu hapa kwenye nyumba yako,, nikamwambia Kaka kwnn sasa? Akasema ww ni mdogo wangu wa damu nisipo kusaidia ww bc nitakuwa mchawi, ungekuwa huna gari bc ningekununulia ila gari unayo tena mpya kabisa, acha nichangie ujenzi,, nikamwambia Kaka asante sana na Mungu azidi kukufanikisha, akaniuliza nina akaunti benk gn, nikamjibu, nikampa namba za akaunti yangu, Kaka yangu aliniingizia milion kumi cash akaniambia nikikwama chochote bc nimjulishe, nilimshukuru sanaa,, hatimae cku zikaisha Kaka akasepa zake Arusha
Mawasiliano na Mahamood yalizidi kushamili cm kutwa kucha, mimba yangu inazidi kukua tu,, nilikuwa napendwa hadi naona kero, ilifika mahari akawa hataki niendeshe gari mwenyewe nikitaka kutoka bc niite uber au nimwambie yeye anitumie dereva
Nakumbuka siku hio nimeamka zangu asbh kama kawaida yangu lazima nitapike kwanza ndipo maisha yaendelee, nipo chooni, Cm yangu ikawa inaita, nikasema nikitoka nitaichukua acha iite tu, nikaendelea na yangu ila cm inazidi tu, nikasema nani huyo jmn? Nikatoka kwa hasira kuchukua cm kuangalia namba shangazi, mhhhh nikasema kulikoni tena?? Nikaipokea, shangazi akaanza kilio Amamu mwanangu nipo hospital hapa mjomba wako kapata ajari ya pikipiki hee!! Makubwa haya tena, nikamuuliza hospital gn akaniambia muhimbili,, nikamwambia sawa nakuja,, nikamcheki Mahamood watsp kumpa zile taarifa akaniambia anamtuma mfanyakazi wake anifate anipeleke, nikaamua kumcheki Kaka kumpa zile taarifa kumbe na yeye aliambiwa na shangazi tena akamuomba hela ila Kaka akamjibu sina, ndipo kunipigia mm,, Kaka akaniambia usiende popote achana nao, ila roho ya huruma ikaniingia nikamwambia Kaka ngoja nikaone tu,, bc tulimalizana na Kaka, nikajiandaa fasta nilivaa baibui langu hadi nikabu ukiniona hunijui Mamujee mm
Dereva akaja tukaenda hospital, nilivyofika kwanza hakunijua nilimkuta nje ya wodi ya Moi anatia huruma kajishika shavu nikasema ngoja nijifanye sijamuona nimpite nikakae mbele yke nimchore kwanza ila roho ya huruma ikaniingia, nikamfata nikamwita shangazi akaitika kwa sauti kubwa Abeee huku ananitazama usoni, maana naonekana macho tu nikaona isiwe shida nikatoa nikabu, hee Amamu mwanangu sijakujua Mama nikamuamkia sikutaka mambo mengi, nikamuuliza vp ilikuwaje, akaanza kuniambia chanzo cha ajari, mjomba alibebwa nyuma cjui ikawaje akajikuta yupo uvungu wa lory,. Na miguu hainyanyuki, hapo wameletwa tangu jana yake ila bado hajapelekwa Opareshen eti kuna foleni wagonjwa wa ajari wapo wengi kwa hiyo asubiri, au alipie Emmegency, nikamwambia sasa c walipie hio kuliko kuendelea kusubiri mguu c utaoza?? Akaniambia Amamu mwanangu hao wanataka hela cash na mm sina hio hela, nikamuuliza sh ngp?? Milion moja na laki saba,, nikamwambia sawa bc ngoja niende benk nikampe,, shangazi alibaki kaduwaa hata jibu hana,, nikavaa nikabu yangu nikatoka kumfata dereva anipeleke benk,, hatukuchelewa kurudi nikampa shangazi milion mbili cash, kisha nikamuaga, akaniuliza huingii ndani kumuona mgonjwa?? Nikamwambia nitakuja cku nyingine,, bc shangazi machozi yakamtoka huku kawa mdogo,, mie huyo nikasepa zangu
Nilikaa kama wiki iv shangazi akanipigia mumewe anaendelea vzr ila wamemuweka vyuma
Maisha yakaendelea nipo zangu kwangu huku mimba yangu inazidi kukua gafra tumbo likawa kubwa ajabu, mhh mbona tumbo linakuwa haraka iv,, sikuanza kliniki coz Mahamood hakuwepo na aliniambia nimsubiri yeye anipeleke, bc nakumbuka mimba yangu ilifika miez sita kwenda saba sijaanza kliniki,, cku hio Mahamood akanipigia akaniambia anakuja kesho kutwa nijiandae, kweli alifika nikampokea vzr zawad kibao zingine nimetumiwa na mke mkubwa, cheni ya gord, pete na kikukuu vyote gord, nirifurahi nikaongea nae kwa cm kumshukuru,, nikapelekwa kliniki pale kairuki wala hatukusemwa kwa nn tumechelewa Mahamood aliongea na doctor sababu ya kuchelewa kuanza clinic, bc nilifanyiwa vipimo vyote hadi ultrasound,, mhhhh niliogopa ultrasound ilionesha nina mapacha,,,,,,,
Itaendelea
Soma muendelezo kwa sh 1000
Njoo WhatsApp 0743433005
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni