MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 21
Cm ya Mahamood ikaingia, nikajiuliza nipokee au niachane nayo? Nikasema ngoja nipokee maana ni Mume wangu, halow Mamujee unaendeleaje? Nikamwambia cjambo, eti mke wangu naomba univumilie, najua unaumia sawa, ila nivumilie mama, huyu mwanamke ni mkorofi sana, amechukua namba yako kwenye cm yangu, ctaki kumwambia kuhusu swala la mimba, nahofia anaweza kufanya hata kitu kibaya, ndio sababu nipo kimya kwa sasa, nasubiri ujifungue kwanza,, nilimuoa huyu mwanamke sababu ya bi mkubwa kukosa uzazi , ckujua kama hata yeye atachelewa kuzaa, wakati namuoa yeye nilimuhakikishia kuwa sitaoa tena yeye ndio wa mwisho, Sasa ningefanya nn na yeye uzazi umekuwa wa shida kwake? Ina maana nikae bila mtoto kweli?! Hapana naomba univumilie,, kama unashida yeyote ya pesa bc nikutumie, naomba utulie, acha presha, ujifungue kwanza,
Aliongea mengi sana kunibembeleza nikamwambia sawa inatosha, maana tyr nilikuwa naona kabisa presha yangu iko juu
Nikamuuliza tu vp ujenzi wangu kule Salasala, maana alimuachia mtu ausimamie, akaniambia unaendelea vzr na wameanza kupaua,, bc nikamwambia sawa bye
Niliendelea kukaa pale kwa Kaka ila akawa amepunguza kidogo Mambo ya wanawake, anawaleta ila wawili, wenyewe hata hawajuani kila mtu anajijua yupo mwenyewe na mm nilikuwa hata siwaopoi maana mie kwangu tupo watatu maisha yaliendelea na cku zikazidi kuisha,, tulikubaliana na Mahamood kabla kuwa nisubiri uchungu niombe Opareshen coz tulihofia watoto wawili harafu marinda sina mhhhh, bc tukawa tyr tunajua mm ni Opareshen tu, hata wakati nipo dar doctor wangu aliniandikia ivo so kwenye fairi langu ilikuwa ipo wazi kuwa nataka opp, nazani mnajua hospital za kulipia hazina shida zinakusikiliza mteja unataka nn,, na nilivyofika Arusha tyr nilishatafuta hospital ya kujifungulia, trh yangu ya opp ilifika nikaenda hospital vzr nilipelekwa na Kaka pamoja na wifi mmoja, nilifika hospital nikalazwa ili kuandaliwa kwa opp,, Kaka alimtafuta Mahamood ila hakupatikana, nikafanyiwa opp vzr nikajifungia salama watoto wa kiume,, nilifurahi sana pamoja na Kaka yangu maana tyr tumeongezeka, tulikuwa wawili ila sasa tupo wanne bc nilikaa hospital kama cku tano iv nikaruhusiwa kurudi nyumbani, niliendelea kula uzazi pale kwa Kaka wala sikuwa na hofu tena kuhusu Mahamood nilisema akinitafuta sawa ila asiponitafuta pia sawa , nilikaa hadi namaliza 40 Mahamood kimya ukimtafuta pia hapatikani, nikasema mhhhh hii sio kawaida kulikoni? Namba ya bi mkubwa sina huwa naongea nae kupitia cm ya Mahamood, nikaona hii hali sio ya kawaida,, namtafuta vp sina njia nyingine? Ila namba ya bi mdogo ninayo aliyonitumia matusi, ila cwez mtafuta!! Nikaongea na Kaka kuhusu ile hali na wasiwasi wangu,, Kaka aliniuliza tu ile ghorofa hati yake jina la nani?? Yaan Kaka unaacha kufikilia wanangu kuhusu Baba yao unawaza ghorofa?? Akaniambia Amamu hao watoto ni wangu, Baba yao awepo au asiwepo wala usijali, niambie tu hati ya nyumba yako inajina la nani?? Nikamwambia inajina langu,, akaniuliza tena una uwakika?? Nikamwambia ndio, akasema bc achana nae yaaan Kaka mipombe imemuaribu jmn,, cjui na mirungi pia, maana anaongea kihuni tu, aliniuliza kuhusu gari yangu nimeacha wap nikamwambia pale pale kwangu ila usalama upo tu, huwa nampigiaga jirani yangu ananiangalizia, bc Kaka akasema kama huumpati huyo mumeo achana nae nikamwambia bc mm nikifikisha miezi mitatu narudi kwangu, akaniambia sawa, kula uzazi kwanza kwa Kaka yako,, bc niliendelea kukaa kwa Kaka ila ckuacha kumtafuta Mahamood ila mafanikio hakuna
Cku moja nipo zangu tu sina hili wala lile, nishaanza kupendeza uzazi umenipenda mwenyewe kuhusu mengine nimemuachia Mungu,, nashangaa mlinzi wa Kaka ambaye ndio house boy, anakuja kuniita eti kuna mgeni wangu,, nimetoka namuona Mahamood, alivyoniona alifurahi, akaniambia nilijua tu tyr umejifungua, nikamwambia kwahyo ulifanya makusudi?? Nikamwambia karibu ndani,, akasema hapana siingii ndani, naomba toa maelekezo kwa watu wako humo ndani tutoke mara moja,, bc nikawaaga madada nikatoka na Mahamood, tukaenda kwenye hotel moja iv, tukaagiza chakula na vinywaji hatukuchukua room,, wakati tunakula na kunywa ndipo akaanza kuniomba samahani, kumbe bi mdogo alivunja cm na alikata kata laini zote za cm, kwahyo alikosa mawasiliano kabisa, mhhhh nikaamua kumuelewa tu, ndipo akaniuliza umejifungua watoto gn?? Nikamwambia wa kiume, maana mda wote huo alikuwa hajauliza chochote kuhusu watoto, akaniambia naomba picha nikamuonyesha ,, Watoto wangu wote machotara nywele Sasa kama Baba yao Mahamood alifurahi akasema nilitegemea hili,, bc alikuwa na cm nyingine kweli tofauti na ile ya mwanzo, akampigia cm bi mkubwa,, yaan bi mkubwa alifurahi jmn yule mwanamke cjui ana roho gn jmn, nikaongea na bi mkubwa akanipa hongera,, Mahamood akamtumia bi mkubwa picha,, bc Mahamood akaweka status yake watoto wake akaandika inshallah, hatimae nimekuwa Baba,, nikamwambia huogopi?? Akasema nilikuwa nasubiri wazaliwe salama tu mm sio mjinga wa kupelekeshwa na wanawake he mara ananionyesha status ya bi mkubwa nae kawaweka watoto kaandika My babies , nikasema bi mdogo lazima aue mtu
Itaendelea
MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 22
Adimin sory sana pamoja na wajumbe, nilitamani kurudi ila bize sanaa walah! Hii sikukuu kwa sisi wafanya biashara ndio wakati wetu wa kupata chochote, sasa nimejikuta hata muda wa kushika cm sina kabisa!!! Natamani kuimaliza hii story......
Bc tulikaa pale Hotelini tukimaliza chakula chetu,,, tulirudi nyumbani ili Mahamood akawaone watoto wake, bc alifurahi sana kuwaona wanae akasema hii kweli damu yngu,, alikaa pale akimsubiri Kaka ili amshukuru,, akaniambia Mamujee naomba turudi dar, nikamwambia sawa ila tulipatana na Kaka watoto wafikishe miezi mitatu, akaniambia hapana, nataka tuwahi nikasimamie ile nyumba iishe kwa haraka, kabla sijarudi Dubai muwe mmehamia na watoto, nikamwambia sawa, MUDA uliisha Kaka hakurudi mapema cku hio, Mahamood aliondoka kulala Hotelini,, bc Kaka aliporudi nilimpa zile habari akakubali mm kurudi dar na Mahamood,, bc asbh tuliamka mapema sana tukajiandaa kuondoka, Kaka akanipa msichana wa kazi mmoja nije nae, Mahamood alitufata tukaanza safari ya kurudi
Tumefika dar vzr tukaanza maisha mapya ya ulezi wa mapacha ( Mtanisamehe majina ya watoto wangu sita yataja kurinda heshima ya familia yangu maana humu tupo wengi na tayari nishajitaja jina langu Mamujee so watu watanijua) bc Mahamood alinitafutia msichana mwengine kwa watu wa makampuni nikawa na wasichana wawili,, tuliishi vzr sana Mahamood alipenda sana watoto wake, nyumba yangu iliisha kabisa, namshukuru Mungu mnoo, nikahamia kwenye nyumba yangu na familia yangu,, kipindi hicho chote choko choko za bi mdogo zinaendelea, mara anitumie matusi, yaan shida tupu, Mahamood alinisisitiza sana nisimjibu kitu hadi pale atakapo yaweka sawa
Nipo zangu kwangu Salasala nishaanza kuzoea maisha yangu na Mahamood yupo anaenda kwenye biashara zake anarudi jioni,, nakumbuka cku moja shangazi yangu alinipigia cm nimuelekeze kwangu anataka aje anishukuru,, mumewe amepona,, nikamwambia shangazi usijali haina haja akasema hapana nielekeze kwako nije,, nikaongea na Mahamood kwanza akaniambia sawa mwache aje,, nikamwambia shangazi kwa sasa mm naishi Salasala, akasema sawa nitakuja jumapili nikitoka kanisani, bc jumapili ilifika kweli shangazi akaja na familia yake , amefika pale kwangu hakuamini akakosa furaha akawa mnyonge sana,, watoto wake wakawa wananiuliza Dada hapa ni kwako? Nikawaambia ndio,, shangazi alishangaa mm kujifungua bila kumjulisha, nikamwambia nilikwenda Arusha kwa Kaka, bc Mahamood alionana na shangazi yangu wakafahamiana ,. Ila shangazi alishikwa na butwaa sana hakuamini Amamu mm kuishi nyumba kama ile na Mume wangu Muarabu bc tuliongea mengi akanishukuru kwa ile pesa niliyompa kumuuguzia mumewe, nikamwambia shangazi usijali sisi ni ndugu uwe na amani,, muda wao wa kuondoka uliisha wakaondoka zao
Kumbe yale maisha yangu aliyoyaona shangazi yangu hapa kwangu yalimpa maswali sana na akaingia na chuki moyoni mwake, shangazi yangu ana mtoto wake wa kike mkubwa tu, tunalingana na mm kiumri ila mm ni mkubwa kama mwaka,(anaitwa Roby) pia na yeye alikuja nyumbani kwangu na mama yake, nashangaa Roby ananipigia cm Dada naomba nije kwako nina shida na ww,, hapo sijui chochote wala sifikirii kama anaweza kunifanyia jambo baya,, nikamwambia sawa njoo,, hapo Mahamood anajiandaa kusafiri kwenda Dubai,, alikuja kwangu vzr nilitegemea labda anakuja na kuondoka kumbe amekuja kuishi nashangaa amefika na begi kubwa, nikajiuliza kulikoni? Dada wa kazi akampokea vzr akaingiza room kwao,, hee kumbe mgeni kaenda kuoga kabadilisha na nguo kabisa Sasa nguo aliyoenda kuivaa jmn bora aliyovua,, kavaa kipensi kifupii na kisingrendi tumbo lote nje,, kaja kakaa sebleni hapo sebleni nimekaa na Mume wangu,, yaan mara ashushe mguu mara apandishe juu hadi Mahamood akashindwa kukaa akaenda chumbani,, kweli sikujua lengo lake ila kwa vitendo vile tu nilijua hapa ametumwa na Mama yaje anichukulie Mume
Itaendelea
Soma mpaka mwisho kwa Tsh 1000
Njoo WhatsApp 0743433005.