MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 38
Mume wangu! Niliita kwa mshangao mkubwa maana sikutarajia, nilikuwa nimesimama sehemu moja nimeigwa butwaa
Mahamood, niliita tena ndipo akageuka huku akifuta machozi, akanitazama na kusema "uko salama mke wangu?"
"Ndiyo" nilisema huku nikisogea na kuketi kitandani namtazama hata siamini "kuna tatizo gani?" Nilimuuliza "unaumwa?"
Akatikisa kichwa kumaanisha haumwi, nikamuuliza mbona umekonda sana halafu pia unalia, kuna tatizo gani niambie"
Nimepitia mengi sana magumu mke wangu, naomba umisamehe sijakutafuta kwa kipindi chote hiki, ndipo na mimi nikamuuliza "sasa kwani ulikuwa na shida gani huko ukashndwa kunitafuta
Akasema kule uingereza kuna sheria ngumu sana, mke wa pili, bi Fatima alinipeleka mahakamani talaka yake iliendana na kugawana mali zangu nusu kwa nusu nimeparangana na hiyo kesi miezi miwili baada ya kuimaliza tu nikapigiwa simu kutoka dubai, mke wangu mkubwa amechukua fedha na kupotea.
Mhhhh nilishtuka sana nikawaza mbona magumu yanatokea kwa wakati mmoja nikamuuliza kwani ulikuwa umegombana mke mkubwa akasema tatizo lilianzia kwenye ile mimba
Nikamuuliza mimba ilisababishaje? Akasema mle alitaka naye aitwe mama ndio maana aliamua kubeba mimba bila kumshirikisha
Niliduwaa kwanza, "kwa hiyo mke ushajua alipo?"
Alasema hajajua alipo, ndipo nikamuambia si atumie madawa yake kujua alipo, akasema mkewe mwenyewe alikuwa ashaujua uchawi hivyo amejisindika ili nisijue yuko wapi. Niliogopa sana
Sasa mbona umekonda? Akasema ni mateso yamenikondesha nimeteseka sana
"Basi kaa hapa nitahakikisha nakuhudumia hadi unenepe sawa? Akasema sawa, maisha yakaendelea vizuri yeye hakutaka tena kurudi dubai.
Siku ya kwanza niliamua kumpikia chakula mwenyewe, nilikuwa najua anapenda nini hivyo nikamuandalia vizuri kisha akaja tukala kwa pamoja huku nikimtia moyo.
Safari ya Dubai nikawa nimeshaiahirisha kwa sababu niliyekuwa namfuata amekuja mwenyewe. Ilipofika saa tatu tu tulienda kulala.
Tulijaribu kufanya mapenzi lakini Mahamood alishindwa kwa sababu alikuwa na msongo wa mawazo sana akaniambia tutafanya kesho, hivyo tukalala.
Usiku saa nane nikashtuka kutoka usingizini, nilipotazama kitandani niko peke angu, nikajiuliza vipi mwanaume yuko wapi, au yuko bafuni lakini kwa kuwa chumba kilikuwa ni masta, nilitazama bafun hakukuonekana kama kuna mtu.
Nikaendelea kujilaza huku nikisubiri arudi dakika zaidi ya kumi mtu harudi ikabidi niwashe taa nitazame simu na laptop vyote kaacha kitandani sasa kaenda wapi?
Nikashuka huku naita "Mahamood...Mahamood" nikafungua mlango
Nilipofungua nilichungulia nikatazama barazani nikamkuta Mahamood amejilaza chini kwenye sakafu, anajiviringisha huku akiweweseka kama mtu anayepitia maumivu makubwa sana
UNAJICHELEWESHA KUMALIZA, kwa sh 1000 unasoma mkasa huu mpaka mwisho
Soma kupitia WhatsApp 0743433005.