Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  artist

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 35

15th Jun, 2025 Views 18

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 35

Mtoto wangu alizaliwa amekufa alikuwa ni mtoto wa kike iliniuma sn nikakumbuka yale maneno ya bi mdogo ndio yalizidi kuniumiza nilikaa hospital kwa muda wa siku tatu then nikarudi nyumbani tatizo la presha halikuniacha likazidi kunisumbua but sio kama wakati wa ujauzito, nilikosa amani nukimfikiria mtoto wangu kwann amekufa??

Bi mkubwa hakukaa sana tangu nimejifungua alihakikisha nipo vzr bc akaanza maandalizi ya safari kurudi nyumbani kwake

Muda mwingi Mahamod alikuwa akinipigia cm kunitia moyo sikutaka kumwambia chochote kama mke wake mdogo ameniambia kuhusu wao na mtoto wangu,,, bi mkubwa alisafiri kurudi nyumbani kwake nikabaki na familia yangu zilipita kama cku tatu tangu bi mkubwa aondoke bi mdogo wa kati alinipigia cm kunipa pole na kuniambia si nilikwambia Mamujee? Mbona hukunisikiza? Nilikwambia nenda kajifungulie nyumbani kwenu? Ona sasa umepoteza mtoto wako? Nikamwambia sawa ila kama binadamu ndio amenifanyia haya bc Mungu atamlipa ila kama ni kazi ya Mungu bc acha nishukuru akaniambia nakutumia hela ya pole ndugu yangu ila ipo cku nitakuja Tz ngoja tumalize mgogoro na Mume wangu nikamwambia nashukuru sn

Maisha yangu yaliendelea nikapata nguvu nikapona kabisa nikarudi kwenye mishe zangu watoto wangu wawili walifika miaka miwili na nusu nikaamua kuwapeleka shule

Nikajikita san kwenye kufanya biashara zangu bi mkubwa bado alikuwa ananigizia mzigo kutoka huko kwao nikaona nifungue duka lingine la nguo

Nikaongea na Mahamod aniongezee pesa nataka kufungua duka la nguo jumla na rejareja bc hakusita sana akaniambia subiri

Bc pale nyumbani kwangu zile fremu ziliisha nikaamua niweke duka la vyakula (Duka laMangi) kwakuwa nilikuwa na wasichana wa kazi wawili bc mmoja nikamuweka dukani hapo nje mmoja akabaki ndani na watoto wanashinda shule,,,, wasichana wangu nilikuwa naishi nao kama ndugu niliwafanya kuwa ndugu zangu na walikuwa waaminifu sana hata ukisahau pesa bc utaikuta

Niliamua nizidi kupambana nijisimamie mwenyewe kuhusu kuzaa niache kwanza

Mume wangu alinitumia pesa ya kuongeza mtaji wangu hapo ndio nikafungua duka kariakoo na mzigo wangu wa kwanza wa hapa dukani kwangu nilichukulia China, nakumbuka hii safari nilisafiri kimya kimya bila ya kumuaga Mume wangu nilifika china nikakaa kama wiki mbili nikarudi Tz niliwaaga wasichana wangu wa kazi wa nyumbani kwangu tu

Lkn nikiwa China Mahamod alinitumia msg Whtsp ukirudi huko ulipo utaniambia nije Tanzania nione watoto nilishangaa nikasema amejuaje kama mm sipo Tz?

Nilirudi Tz nikapumzika kama wiki nikaanza biashara kariakoo sikumtafuta Mahamod nikawa niko bize nashukuru Mungu nilianza biashara kariakoo kipindi sikukuu zinakalibia na nilikuwa na mzigo wa kutosha nauza jumla na rejareja biashara ikapamba moto

Mahamod alinipigia cm anataka kuja Tanzania nikamwambia sawa bc niliendelea na maisha yangu

Mahamod alifika Tz, alifurahi na watoto wake nilijiwahi nikenda kuweka vijiti vya uzazi wa mpango sikutaka kuzaa na Mahamod tena kila nikikumbuka nilivyoteseka na mimba then mwanangu kufariki nilikuwa nachukia kuzaa na Mahamod

Mahamod aliniuliza kwann umeenda China bila ruhusa yake? Nikamwambia nilifata mzigo wa biashara bc alikasirika akafoka kwamba kuniacha nifanye biashara kusinipe kiburi anauwezo wa kuniachisha hio biashara nikakaa nyumbani,, nikamwambia nisamehe Mume wangu bc alikubali yakaisha tulienda nae hadi kariakoo akaona biashara

Itaendelea

Mamujee

Furaha naomba nijibu baadhi ya comment, maana story yangu nakaribia kumaliza,, kuna watu wanacoment eti sina marinda, ni kweli kabisa ndio sababu nimeleta kisa mjifunze wengine, maana kuna baadhi ya wasichana wanavunja utu wao kwa makusudi kuingiliwa kinyume na maumbile bila ya kupata chochote, then wapo wengine wanadhani hii story ni ya kutungwa, wapenzi hii ni true story tena ni yangu mm mwenyewe, maisha yangu niliyopitia hadi sasa nilipo, leo ukiniona natembelea gari nzuri naishi nyumba nzuri unaweza ukatamani maisha yangu ila nilipotoka huwezi kupita,, then kuna mtu amecoment kuwa kwann naandika kwamba akanipeleka hadi kwenye hard yake ya magari?? Naandika ivo ili watu wote wanielewe maana uwelewa tumetofautiana, ningeweza kuandika TU akanipeleka kwenye hard yake,,, haya maisha nimepitia mm Amamu,, ni kama past tu, ila kwa Sasa nina maisha tofauti kabisa, wengi hawajui nilipotoka ila wakiniona naendesha prado wananiona mchawi

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 36

SEASON TWO,
Wapenzi wasomaji pole nimewachelewesha sana kupata msimu wa pili, nilikuwa naumwa kwa kipindi kirefu ila sasa alhamdulillah namshukuru Mungu naenderea vizuri.

Tuendelee
Mimi na Mahamood tuliendelea kuishi kwa kipindi kirefu huku akionekana hataki kwenda kwa wake zake wengine, ikafika kama miezi 3 nikamuomba aende kwa sababu sikutaka ugomvi mimi na wake wenza ambao walikuwa wamenitangulia, akasema hatokwenda ndio nikamuuliza kwanini
Mahamood aliniambia kwamba hataki kwenda kwa sababu kuna masharti mke mkubwa ameweza kuyavunua hivyo ingeweza kuleta matatizo kati yake na mizimu kwa sababu alikuwa amewakosea

Nikamuuliza kwanini unanificha mambo yako, si uniambie ni masharti gani hayo? Akasema mke mkubwa kaamua kushika mimba bila ridhaa yake wakati masharti kipindi anamuoa basi alikuwa anatakiwa asizae na mwanamke huyo.

Nilishangaa nikamuuliza kwa hiyo alivyokuwa ananiambia kwamba hana uzazi ilikuwa ni uongo? Akasema ndiyo ni masharti

Kwa hiyo mbona mimi ulinizalisha watoto akasema haikuwa kwenye mpango wake kuzaa lakini nilipokataa asiniingilie kinyume basi ilitokea kwa bahati mbaya na hata alivyojaribu kuongea na mizimu aliambiwa mimi ni mwanamke mwenye nyota kali hivyo asiniache kabisa

Kwa hiyo mkeo huyo utaacha kumfuata? Akaniambia ili aende lazima huyo mwanamke atoe kwanza hiyo mimba maana akienda kule na mwanamke yule ana mimba basi atapata matatizo makubwa sana.

Nilishangaa mno na niliogopa nikasema ile ni familia ya aina gani mbona ina mambo magumu kiasi hicho? Ghafla tukiwa tunaongea, mke mdogo wa kati ya bi Fatima ambaye alikuwa anaishi Uingereza, alimpigia simu Mahamood.

Mahamood akasema huyu vipi ananisumbua, anataka kuniambia nini? Mimi nilikaa kimya sikuongea lakini Mahamood alipokea simu na kuongea naye.
Walianza kuongea kiswahili kilichochanganyika na kiarabu na kiingereza humo humo, mwanamke akasema "Mahamood tafadhali nahitaji taraka yangu sasa, nimechoka kupoteza muda duniani
Mahamood akamuuliza kwanini mnanitesa hivi nyie wake zangu? Yaani hamniachi nipumue muda wote visa tu? Mbona huyu mdogo yeye hana mambo mengi

Huyo si ni mwafrika ni maskini unadhani ataweza kukuacha wakati una hela? Mimi nnahitaji talaka yangu nataka nikaanze maisha yangu nimechoka maisha ya kuishi miezi mitano bila mum
Maneno ya kwamba mimi mwafrika nina maisha magumu siwezi muacha yaliniuma, nikajikuta nalengwa na machozi.

Mahamood alinitazama machoni, alipogundua natokwa na machozi akakata simu na kuniwekea mkono begani akaniambia "mke wangu nakupenda sana, na ndio maana niliondoka Dubai badala niende uingereza nikaja kwako ni kwa sababu wewe ni mke bora" niliendelea kulia

Najua maneno ya Fatima yamekuudhi lakini naomba usilie piga moyo konde kumbuka tulipotoka
"Ameniita mimi maskini? Nilisema kwa uchungu huku kilio kikiongezeka"

Kwa hasira, Mahamood aliinuka akaenda chumbani na kutoka akiwa na kalamu na karatasi, akaanza kuandika talaka ya yule mwanamke, halafu akaipiga picha.

Nikamuuliza unafanya nini akasema anamtumia kweli talaka maana si kaitaka nikajaribu kumkataza lakini alimtumia kupitia whatsapp huku ikisindikizwa na voice note kwamba original copy atampelekea wiki inayofuata akiwa anaelekea uingereza kuzifuatilia biashara zake

Naam usijisubirishe kusoma muendelezo kama ununuavyo bando kila siku, leo nunua simulizi hii kwa sh 1000 uisome mpaka mwisho
Njoo WhatsApp 0743433005.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 35 https://gonga94.com/semajambo/mwarabu-huko-mi-sijazoea-35 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MARIA Sehemu 16

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MARIA Sehemu ya 10

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MARIA Sehemu ya 7

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

RATIFA sehemu ya 37

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

RATIFA sehemu ya 36

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

Obi's Pain Chapter 4.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

TAMU YA SAKINA 02.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DEAR DOCTOR 01

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MPANGAJI ... 01

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 15

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 14

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

TAMU YA SAKINA 01

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

Obi's Pain Chapter 1

mjukuu rewards 100 Comments 1
 

MSHANGAZI EPISODE 2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 14

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MSHANGAZI EPISODE 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 13

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 10

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

YAMENIKUTA

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 9

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINSI YA KUTUNZA UKE

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

PART 5 MY HEART

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest