Huyu Baleke kapigwa na Kitu kizito sana..
Quality ya Jean Baleke yule kwenye Dimba Mohamed wa Tano pale Morroco kwenye robo Fainal ya CAF Champions League Siku Ile majukwaa ya Mashabiki wenye kelele nyingi Zaidi Africa wa Wydady Casablanca yamekaaa kimya,Siku Ile Baleke alikuwa kama Monita wa Darasa Kutuliza kelele za Mashabiki wa Wydady ,Siku Ile Baleke akiwa Katika Kiwango bora sana anaondoka na Mabeki watatu wanne kutokea Katikati anapunguza na Kutoa pasi,Siku ile Baleke anapiga short on target za kutosha.Mashabiki wanalia majukwaaani Vazi la Hijabu likitumika kufuta machozi,Siku Ile Simba Ilikuwa bora sana, Baleke Huyu unae muona Jukwaani hapo Ni Bonge la Mchezaji ,Toka nimjue Huyu Mchezaji hajawahi kupoteza nafasi tatu,Akikosa ya Kwanza,Ya Pili basi ya Tatu jiandaeni kushangilia
Nini kimemkuta Jean Baleke !!!.