*BíNTI MPELELEZI*
SEHEMU YA... 2
Na
Mamuh mohd
(0716730000)
Tulipoishia.....
Binti huyo nae alimtazama kosho kwa uwoga huku machozi yakimtoka....
SONGA NAYO.....
Kosho alijaribu kumsemesha Binti yule lengo ajue kama ataelewa kugha anayozungumza,
"Habari yako dada?"
"Habari mbaya kaka naomba nisaidie".
Ndipo akaona kuwa nae anaweza kuzungumza vizuri wakaelewana.
Kosho kwanza akamvuta binti yule ndani kabisa ya miti na kujifucha nyuma ya mti fulani nia wasionekane na watu.
"Umetokea wapi?"
"Nimetokea nchi ya mogoka"
Kosho alishangaa kusikia vile,
"Nchi hiyo si inasifika sana kwa vita na mauaji ya watu? "
" Ndio kaka Ndio maana nimekimbilia huku hauwezi kuamini nimeogelea baharini huku napumzika nchi kavu siku15 mpaka nimefika hapa tafadhali naomba nisaidie kaka nakuomba"
" Hata hii nchi yetu sio nzuri sana Sultan wetu ana roho mbaya sana akijua uwepo wako atakuua"
" Nilinde nakuomba nimekimbilia huku kwa sababu mama yangu alikuwa raia wa huku alitoroshwa na baba yangu alinisimulia na kaniambia hivyo ndio maana nimekuja huku naomba nisaidie".
Shoko alimuonea imani binti yule akamjibu,
" Sawa wacha nikakutafutie mavazi ubadili wakikuona umevaa hivi watakushtukia kama ni mkimbizi umekimbilia huku na wale wenye roho mbaya wataenda kumuambia Sultan"
" Vyovyote usemavyo kaka hakika nitakubali nisaidie nakuomba".
"Sasa baki hapa hapa mpaka nitakapokuja.
Najua hakuna mtu atakuja huku ukizingatia leo watu wote wapo Bize na maji nitakufuata hata kama ni usiku"..
Binti yule alikubali
Basi shoko akamficha Binti yule pale kwenye mti kisha akarudi kuchukua maji Yake na kuondoka.
Kosho aliuza maji pesa kidogo alizopata alienda kununua kitambaa kama nguo kwa ajili ya yule Binti kisha akasubiri mpaka usiku ndipo akachukua baskeli yake na kuanza safari kumfuata mrembo yule.
Alipofika aliwasha kitochi lakini kuangaza pale kwenye mti alipomuacha hakumuona Binti yule aliishangaa na kumulika mbele nyuma kulia na kushoto lakini hakumuona, shoko alipata wasiwasi kuwa huwenda amekamatwa na watu wamemuona na kumpeleka kwa Sultani huko watamuua.
"Daaa!.. sijui nini kimekupata rafiki uko wapi?"
Sasa shoko alipouliza vile ndipo Binti akamjibu,
" Nipo juu ya mti".
Kosho alisikia sauti ile na alipomulika tochi juu ya mti kweli alimuona Binti amejikunja kule kisha akaanza kuteremka,
"Nilidhani umeniacha hautorudi tena kunichukua asante maana pale ulipoondoka niliona kundi la watu walikielekea huku na ulivyoniambia kuwa watanipeleka kwa Sultani wakigundua mimi sio raia wa hapa sikuwa na jinsi nikapanda juu ya mti huku nikiomba wasinione".
" Pole umefanya vizuri sana haya badili nguo jifunge hivi chini na juu".
Binti yule alikubali Hivyo akajifunga nia afanane na wanawake wanaoishi himaya ya pale kisha zile nguo zake alizokuja nazo wakazitupilia mbali na kupanda baskeli kuondoka tayari Binti yule ataanza maisha ya kuishi katika himaya hiyo.
Kosho alimfikisha mpaka nyumbani kwake akapika chakula wakala na Binti huyo alionekana kuwa na njaa kwelikweli hivyo alikula sana,
"Jina Langu naitwa kosho je wewe unaitwa nani?"
"Naitwa Yenah"
" Ohhh sawa karibu sana" .
Basi walianza kusimulia kila mmoja akimueleza mwenzake historia yake mpaka pale walipofikia japo kosho historia yake y kumpoteza mdogo wake na mama yake kuuliwa kinyama ilimgusa sana binti yenah.
na Yenah alimpa pole nyingi kosho kwa kuuliwa mama Yake.
Basi kesho yake Asubuhi Yenah alikuwa akitoka zake kuoga maana alikuwa mchafu lakini alipotoka watu walimuona kwani eneo la Kuogea lilijengewa nnje.
Baasi majirani wakaanza kuitana,
"Heee jamani hawa ebu ona kosho ameoa au? Mbona mwanamke yule Katoka kuoga kisha kaingia ndani kwake".
" Mhhh mwezangu hili jipya kaoa lini? atakuwa kimada chake lakini tumjue ni nani maana wanawake wa hapa wengi nawajua"
" Umeonaee tumfuatilie".
Yalikuwa ni mazungumzo kati mabinti wawili Hawa na Zena jirani zake na kosho.
Basi upande wa nyumbani katika jumba kubwa la Sultani mke wa Sultani bi Zunaifa alikuwa akilia bado tokea mumewe amfokee tena mbele za watu aliishia kulia kwani alikuwa ni mpole sana.
Mala mama mzazi wa Sultan Harid alimfuata malkia huyo katika chumba chake alichokuwepo,
"Mwanangu pole najua unasononeka msamehe bule mumewako ni hasira tu"
" Mama kumsamehe nimeshamsamehe zamani sana lakini roho inaniuma anachoongea ni kweli ni Sultani anahitaji kuwa na watoto na mimi mpaka sasa nimeshindwa kutimiza hili anahitaji kupata watoto"
" Mhhh kwaiyo unamaana gani? "
" Nawaza apatikane mwanamke mrembo amzalie mumewangu nitampanga pesa atakazo kisha mtoto atabaki kuwa wa kwetu"
" Hapo umeongea sikutegemea useme eti unataka kumuacha mumeo na wala kuoa mke mwingine hilo suala halipo na katika Nchi hii sijaona mwanamke mrembo kukuzidi wewe zunaifah nani atazaa na mwanangu nahitaji alie mzuri ili mpate watoto wazuri"
" Wacha nitazungumza na vijakazi wetu wakatafute mwanamke mrembo Kisha wanikutanishe nae nifunge nae mkataba na Sultan sitomuambia hili bali nitamuandalia mazingira atashuhudia hiyo siku moja tu"
" Sawa mwanangu nawaombea mfanikiwe ila makubaliano ni azae tu wewe ndie utakuwa mama japo sidhani kama atapatikana mwanamke mrembo ila sawa akikosekana bola tuache kuliko kupata wanawake wabaya wakatubaribia mbegu".
Aliongea ivyo mama wa sultan halid.
Basi zunaifah alianza hiyo Kazi akawaita vijakazi wakiume na kuwataka wakamtafute Binti mzuri kisha wakimpata waje kumpa jibu lakini aliwasihi iwe siri yao walikubaliana na msako ukaanza.
*****
Basi Upande wa mabinti wale wawili Zena na Hawa uzalendo uliwashnda wakaenda nyumbani kwa kosho na wakati huo kosho alikuwa ametoka hivyo yupo yenah pekee.
"Hodiiii kaka koshooo weee hodiioo... Au ametoka? Lakini mbona mlango upo wazi?"
Yenah kusikia vile akaamua kwenda kuitikia,
"Karibuni"
"Heee habari yako dada"
"Salama"
"Wewe ni mgeni hapa?"
" Ndio ni mgeni kwa mitaa hii ila nimwenyeji wa kule chini panaitwa mfenesini ndo kwetu"
" Anhaaa kwaiyo kosho ni ndugu yako ama?"
" Hapana ni mke wake"
" Heee jamani kaoa kimya kimya haya karibu wifi"
" Asante".
Mabinti wale wakaondoka.
Yenah alirudi ndani ndipo akakumbuka asubuhi kosho wakati anatoka alimwambia,
"Kuna jirani zetu hapa mabinti ni wambea sana ikitokea wamekuona wakaja waambie nimekuoa kwenu panaitwa mfenesini hivyo Binti alishapangwa ndio maana alijibu bila kubabaika.
Sasa vijakazi wa Sultan wawili kolini na huliyo mwenzake walikuwa wakianza kazi waoiyopewa na malkia japo ni ngumu wanawake wa hapo walikuwa wa kawaida sana mzuri alikuwa ni Malkia zunaifah ndio maana akaolewa na Sultan.
Sasa wakati wanatembea vijakazi hao wakakutana uso kwa uso na mabinti wale zena na hawa kumbe walikuwa wakifahamiana zena alikuwa ni mpenzi wa Koloni na Hawa mpenzi wa Huliyo.
"Jamani mpo bize sana hatupati Muda wa kwenda kupunga upepo baharini".
" Msijali wapenzi ipo siku tutakuwa karibu hapa kuna Kazi ngumu tumepewa"
" Kazi gani?"
" Acheni tu tunatafuta Binti mrembo malkia ametutuma sijui kwanini na tumezunguka bila mafanikio sijui tuende kule chini kabisa".
Zena na hawa wakatizamana na kugonga mikono kwa umbea.
" Mnahangaika mmemuona mke wa kosho?"
"Kosho kwani ameoa?"
"Kaoa nakwambia kimya kimya mke mke kwelikweli jeupeeeeee"
Koloni na Mwenzie wakatazamana.....
Full 1000
Whatsapp no 0716730000.
Sijui itakuwaje?
Tukutane Sehemu ya.....3.