SIMULIZI YA MAISHA: NILIMUUA MAMA YANGU MZAZI ILI NIOLEWE NA BABA.....06
Na Sam Darfur 0717255498
RECAP: SEHEMU ILIYOPITA
Baba naye alikuwa makini kutaka kujua ni jambo gani ambalo alitaka alifanye ili kunilinda, ilinibidi nimwambie nikasema.
“Njia pekee ya kunifanya niishi kwa amani ni kumuua Mama. Naondoka hapa nyumbani ila siku ambayo nitakuwa narudi basi ni katika mazishi ya Mama na sio vinginevyo” hivi ndivyo ambavyo nilimwambia Baba tena kwa msisitizo...
SEHEMU YA SITA
Tafadhari... ukimaliza kusoma tufollow.......Baba alikubaliana na mimi huku akiahidi kwamba atakamilisha kile ambacho nimemwambia hata kabla ya Mimi kumaliza shule, kauli za baba zilinipa matumaini huku nikiamini kwamba kila kitu kitaenda sawa.
Nimeamini kwamba mapenzi yanaweza kutengeneza uadui, sio tu kwa mpenzi wako ambaye amekuacha bali hata kwa ndugu au hata mzazi wako. Kwa jinsi ambavyo nilikuwa napendana na Mama nilikuwa namchukulia kama mtu ambaye sitakaa siku eti niwaze kukuua.
Lakini tangu nilipoingia katika mahusiano na Baba kisha tukaanza kufanya kwa kujiibia iba basi niliona napaswa kumsafirisha Mama kutoka duniani hadi kuzimu, huko angejua mwenyewe kama angejibu vizuri maswali ambayo angeuliwa na Mungu wake ama lah.
Hatimaye, nilifanikiwa kwenda shule, nikiwa huko nilifanya masomo yangu vizuri. Sikuacha kuwasilaiana na baba mara kwa mara naye aliniambia kwamba bado anakamilisha mission yake hivyo niendelee kusubiri.
Nakumbuka kwakati nikiwa shule kulikuwa na msichana mwenzangu ambaye alikuwa anaitwa Brandina. Huyu alikuwa ni shoga yangu kabisa na tulikuwa tunalala room moja pindi tuwapo hostel.
Brandina alikuwa ni mrefu kama mimi, umbo lake lilifanana na mimi hata muonekano pia kitu ambacho kilifanya watu wengi watuite mapacha yaani twins. Sababu tulikuwa tunatembea wote pamoja, tunalala chumba kimoja hata katika kukaa darasani dawati lake likukuwa mbele yangu hata kama nikisema nikuoneshe picha ya Brandina hapa sasa hivi basi utadhani ni mimi.
Kipindi ambacho tulikuwa tunatoka prepal sikuacha kumsimulia stori zangu za Maisha ya nyumbani kwetu, nilianza kumpa kila siri zangu kama unavyojua mtu ukimwamini maana hata yeye alikuwa ananipa siri zake kwa kifupi naweza sema tulikuwa tunapeana siri.
Nakumbuka, siku moja, wakati tukiwa tuchambani tunakaribia kulala, nilianza kusoma soma hivi kidogo katika kitanda changu cha juu ghafla aliingia Matron huku akiwa na hasira mno.
Nilishangaa kwanini Matron amekuwa na hasira kiasi kile.
“Kwanini mnawasha taa hadi muda huu?” aliuliza Matron
“Kuna ubaya gani kama tupo hapa kwa ajili ya kusoma tu?” Nami nilimtwanga swali
“Zimeni taa mlale muda ushaenda sasa hivi” alisema.
Hatukuona sababu ya kupingana naye, nilishuka katika kitanda na kwenda kuzima taa kisha nirudi tena kitandani na Matron aliondoka katika room yetu.
“Brandina weekend nataka twende tukaonane na Baba sijui upo tayari?” nilimwambia
Brandina
“Mh! Wapi atakuwa?”
“Baba yangu ni mtu wa kutoka sana, sio mbali ni hapo Dar es salaam Zoo! Tutaenda pale na kuangalia Wanyama wa kila aina kisha baadaye tutarudi hapa shule”
“Haitaleta madhara lakini?”
“Hapana, I know him hata hivyo akishampigia matron hakuna kitu ambacho kitaharibika” nilimhakikishia Brandika.
Kabla ya hapo haikuwa kawaida yangu kuondoka shule siku za weekend lakini tangu nilipoingia katika mahusiano na baba basi nilihakikisha kwamba nawasiliana naye na kumtaka kwa siku za weekend awe anakuja na kunitembelea kama sio kunichukua.
Ingawa shule yetu ilikuwa haina sheria inayoruhusu mwanafunzi anaweza kuondoka kwa siku hizo lakini kutokana na fedha ambayo Baba alikuwa nayo basi aliiacha izungumze mbele ya matroni ambaye alitoa go ahead ya mimi kuondoka.
Hatimaye, siku zilikwenda na weekend ilifika, tuliondoka mahala pale kama saa mbili asubuhi hivi huku Baba akija kutuchukua Mimi na Brandina. Tulianza kwenda Mall ambako huko tulichagua nguo zetu nzuri kisha baadaye ndio tukaenda rasmi katika zoo.
Tulipofika tulifurahia Maisha asikuambie mtu, kumbe kwa muda wote ambao tumeongozana na Baba. Brandina alikuwa anawaza raha ambazo baba alikuwa anazitoa yaani kule kutumia pesa bila mpangilio kwake alizitamani, aliona ana kila sababu ya kupindua meza kibabe nami sikulijua hilo.
Basi tulicheza, tukaangalia Wanyama na muda mwingine tulikula pia, hadi ilipofika majira ya saa ya kuondoka ndio tuliondoka katika eneo lile. Safari yetu ilitua katika geti la shule, Brandina alishuka huku akiniacha mimi na Baba tukipiga stori za hapa na pale.
“Huyu ndio Rafiki yako ambaye unamsemea kwamba mnaitwa mapacha?” Baba aliniuliza
“Yes, anaitwa Brandina. Ni mpole, charming hana mambo mengi kama unavyomuona”
“Anaonekana tu, vipi ana mwanaume?” Baba aliuliza
Kwanza nilipigwa na butwaa, nilijikuta namuonea wivu Brandina ghafla bin vuu. Nikamtazama Baba kisha nikasema
“Ndio, ndio yupo naye tena ni mwalimu, ndio anamsaidia kufaulu masomo yake”
“Ok, nilitaka kujua hilo tu maana naona kama ni mtu ambaye umechukia hivi”
“Ni kweli nilikuwa nimechukia sababu haiwezekani umuulizie kama ana mwanaume au hapana, anyways vipi kuhusu mpango ambao nilikuambia?” niliamua kubadilisha mada
Baba aliinamisha kichwa chini, alionekana kama mtu ambaye alikuwa anatafakari jambo hivi. Alipoinua alisema
“Bado”
“Kwanini? Kwanini hujafanya hadi muda huu?” nilikuwa mkali mno
“Love usijali, kitu kizuri hakihitaji haraka. Nawaza namna nzuri ya kufanya ili hata kama anakufa serikali isijue. Unajua hata mimi naumia pale ambapo nashindwa kuwa pamoja nawe kama wapenzi? Nateseka kuwa mbali na penzi unadhani kwamba napenda kukukosa baby?”
“Shaulako, only one month left (Mwezi mmoja umebakia) nitarudi tena mtaani sasa nina maana yangu ya kukuambia umuue ila kama hujui namna ya kufanya I’ll do it myself” niliwambia Baba huku nikimpa kitisho kwamba kama yeye hajui namna ya kuua basi nitafanya mwenyewe.
Sikuona kama nilikuwa na sababu ya kukaa katika gari, nilishuka huku nikijifanya kuwa hasira mno. Ni kweli nilikuwa na hasira maana niliona mambo mawili yakitokea ambayo yamenichanganya
Moja lilikuwa ni suala la baba kushindwa kumuua Mama eti kwa kigezo kwamba anatafuta njia nzuri na lingine lilikuwa ni kuhusu baba kumuulizia Brandina kama ana mwanaume. Sijui hata nisemaje lakini tambua kwamba nilikuwa na hasira ambazo hazikuwa na mfano wake.
Basi nilipoondoka katika gari, kituo cha kwanza kilikuwa kwa Brandina ambaye nilimchimba mkwara.
“Miss, Brand mwenye ndina yake mwenyewe. Najua unajua jinsi gani nakupenda na nakuchukulia kama sehemu ya familia yangu lakini usitake nikuchukie” nilisema huku nikiwa nimesimama katika mlango wa chumba chetu.
“Kuna nini Alvila mbona unanichanganya?” “Baba ameuliza kama una mwanaume au hauna na nimemwambia upo naye sasa hilo tisa. Kumi ni kwamba sitaki nione ukiwa na mazoea naye. Nimemaliza” nilisema kisha huyo nilijiangusha kitandani na sikutaka kuzungumza tena na Brandina.
Dalili ya mvua ni mawingu bwana, ni kama nilijua nini ambacho kilikuwa kinaendelea baina ya Brandina na Baba, kumbe wakati tupo Zoo. Baba alimwandikia namba Brandina ili wapate kuzungumza vizuri lakini haya yote sikuwa nayafahamu.
Kwangu niliimani kuwa bado Baba alikuwa na mapenzi ya dhati kwangu bila kujua kwamba nimekaribisha fataki katika eneo ambalo wanafunzi wapo wengi kupitiliza tena wote wakiwa na sketi za mtego, yule ambaye angejirahisisha basi angeliwa kama ilivyokuwa kwa Brandina.........
Nini kitafuatia...!? Weka Like yako na pia coment ili mzigo utoke mapema.
Jana kuna watu mlikosa ofa mkanunua kwa bei ya juu kabisa... Leo natoa ofa kwa watu 15 pekee. Nunua kwa nusu bei yaani 1500Tsh badala ya 3000Tsh. Nitext WhatsApp 0717255498..
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.